Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Vita alivyoshiriki na Ambavyo hajashiriki Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake:

Hadithi 2

Ninamuapa Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako, hilo ni bora zaidi kwako kuliko ngamia wekundu

عَنْ سَهْلُ بْنُ سَعْدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ يَوْمَ خَيْبَرَ: «لَأُعْطِيَنَّ هَذِهِ الرَّايَةَ غَدًا رَجُلًا يَفْتَحُ اللَّهُ عَلَى يَدَيْهِ، يُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيُحِبُّهُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ»، قَالَ: فَبَاتَ النَّاسُ يَدُوكُونَ لَيْلَتَهُمْ أَيُّهُمْ يُعْطَاهَا، فَلَمَّا أَصْبَحَ النَّاسُ غَدَوْا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كُلُّهُمْ يَرْجُو أَنْ يُعْطَاهَا، فَقَالَ: «أَيْنَ عَلِيُّ بْنُ أَبِي طَالِبٍ؟» فَقِيلَ: هُوَ يَا رَسُولَ اللَّهِ يَشْتَكِي عَيْنَيْهِ، قَالَ: «فَأَرْسِلُوا إِلَيْهِ»، فَأُتِيَ بِهِ فَبَصَقَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي عَيْنَيْهِ وَدَعَا لَهُ، فَبَرَأَ حَتَّى كَأَنْ لَمْ يَكُنْ بِهِ وَجَعٌ، فَأَعْطَاهُ الرَّايَةَ، فَقَالَ عَلِيٌّ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أُقَاتِلُهُمْ حَتَّى يَكُونُوا مِثْلَنَا؟ فَقَالَ: «انْفُذْ عَلَى رِسْلِكَ حَتَّى تَنْزِلَ بِسَاحَتِهِمْ، ثُمَّ ادْعُهُمْ إِلَى الإِسْلاَمِ، وَأَخْبِرْهُمْ بِمَا يَجِبُ عَلَيْهِمْ مِنْ حَقِّ اللَّهِ فِيهِ، فَوَاللَّهِ لَأَنْ يَهْدِيَ اللَّهُ بِكَ رَجُلًا وَاحِدًا، خَيْرٌ لَكَ مِنْ أَنْ يَكُونَ لَكَ حُمْرُ النَّعَمِ».
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema siku ya vita vya Khaibari: "Kesho nitampa bendera hii mtu ambaye Mwenyezi Mungu ataleta ushindi kupitia mikononi mwake, ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda." Akasema: Watu wakalala usiku kucha wakijadili hilo, ni nani kati yao atakayepewa! Palipopambazuka watu walikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake wote wakitaraji kuwa atapewa, akasema: “Yuko wapi Ally bin Abi Twalib?" pakasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, anaumwa macho, akasema: “Basi mtumieni mtu akamuite.” Akaletwa, Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akamtemea mate machoni mwake na akamuombea, akapona kana kwamba hakuwa na maradhi, hivyo akampa bendera, na Ally akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nipigane nao mpaka wawe kama sisi? Akasema: “Songa mbele, mpaka utue kwenye uwanja wao, kisha uwaite kuja katika Uislamu, na uwafahamishe yale yaliyo wajibu juu yao katika haki za Mwenyezi Mungu kwake, Ninamuapa Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako, hilo ni bora zaidi kwako kuliko ngamia wekundu."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwaeleza Maswahaba kuhusu ushindi wa Waislamu dhidi ya Mayahudi wa Khaibar siku ya kesho, na hilo litakuwa mikononi mwa mtu atakayempa bendera, nayo ni bendera ambayo hutumiwa na jeshi kama nembo yake. Na mtu huyu miongoni mwa sifa zake ni pamoja na kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda. Kwa hiyo Maswahaba walipitisha usiku kucha wakijadiliana na kuzungumza juu ya nani atapewa bendera? Kwa kutamani kuipata heshima hii kubwa, Ilipofika asubuhi walikwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake wote wakiwa na matumaini ya kupata heshima hii. Basi Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuulizia Ally bin Abi Twalib Allah amuwie radhi? Pakasemwa: Ni mgonjwa na analalamika kuhusu macho yake. Basi rehema na amani zimshukie, akamtumia watu wakamlete, akamtemea Ally machoni katika mate yake matukufu na akamuombea, akapona ugonjwa wake kana kwamba hakuwa na maradhi, akampa bendera na akamwamuru aende kwa upole mpaka aikaribie ngome ya maadui na awaite katika Uislamu, ikiwa watamjibu; Awaambie ni wajibu gani wanapaswa kufanya. Kisha rehema na amani ziwe juu yake, akamueleza Ally ubora wa kumuita mtu kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba ikiwa mlinganiaji atakuwa ni sababu ya kuongoka kwa mtu mmoja, hiyo ni bora zaidi kwake kuliko kuwa na ngamia wekundu ambao ndio utajiri wa thamani zaidi kwa Waarabu, azimiliki au azitoe sadaka.

Mafunzo
  1. Ubora wa Ally bin Abi Twalib – Mwenyezi Mungu amuwie radhi – na ushahidi wa Mtume – Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani – juu yake, wa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake juu yake, na mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.
  2. Maswahaba walikuwa na shauku ya kufanya kheri na kulikimbilia kwao hilo.
  3. Sheria ya adabu wakati wa vita na kuacha kutojali na kelele zenye kuudhi yasiyokuwa ya lazima.
  4. Miongoni mwa dalili za utume wake, rehema na amani ziwe juu yake, ni kutoa habari ya ushindi dhidi ya Mayahudi, na kumponya kwake macho Ally bin Abi Twalib mikononi mwake, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
  5. Madhumuni makubwa ya Jihadi ni watu kuingia katika Uislamu.
  6. Nikuwa wito wa kuwaita watu katika Uislamu hutolewa taratibu taratibu, kwanza kafiri ataombwa kusilimu kwa kutamka Shahada mbili, kisha ataamrishwa kutekeleza faradhi za Uislamu baada ya hapo.
  7. Fadhila za kuwaita watu katika Uislamu na kheri zilizomo kwa mlinganiwaji na mlinganiaji, mlinganiwaji anaweza kuongoka, na mlinganiaji kwa hilo atalipwa malipo makubwa.
Marejeo

صحيح البخاري (5/ 134) (4210). صحيح مسلم (4/ 1872) (2406). فتح المجيد شرح كتاب التوحيد، (ص88). القول المفيد على كتاب التوحيد، (1/ 134). الملخص في شرح كتاب التوحيد، (ص57). الجديد في شرح كتاب التوحيد، (ص67). التمهيد لشرح كتاب التوحيد، (ص59).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Laiti wangeingia wasingelitoka humo mpaka siku ya Kiyama; Utiifu unakuwa katika jambo jema

عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: بَعَثَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَرِيَّةً فَاسْتَعْمَلَ رَجُلًا مِنَ الأَنْصَارِ، وَأَمَرَهُمْ أَنْ يُطِيعُوهُ، فَغَضِبَ، فَقَالَ: أَلَيْسَ أَمَرَكُمُ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ تُطِيعُونِي؟ قَالُوا: بَلَى، قَالَ: فَاجْمَعُوا لِي حَطَبًا، فَجَمَعُوا، فَقَالَ: أَوْقِدُوا نَارًا، فَأَوْقَدُوهَا، فَقَالَ: ادْخُلُوهَا، فَهَمُّوا، وَجَعَلَ بَعْضُهُمْ يُمْسِكُ بَعْضًا، وَيَقُولُونَ: فَرَرْنَا إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنَ النَّارِ، فَمَا زَالُوا حَتَّى خَمَدَتِ النَّارُ، فَسَكَنَ غَضَبُهُ، فَبَلَغَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: «لَوْ دَخَلُوهَا مَا خَرَجُوا مِنْهَا إِلَى يَوْمِ القِيَامَةِ؛ الطَّاعَةُ فِي المَعْرُوفِ».
Imesimuliwa kutoka kwa Ali, Mwenyezi Mungu amridhie, kwamba alisema: Alituma kikosi Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuweka kiongozi bwana mmoja katika Maanswari (watu wa Madina), na akawaamrisha wamtii, akachukia, akasema: Hivi hakukuamrisheni Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mnitii? Wakasema: Ndivyo, akasema: Nikusanyieni kuni, wakakusanya, akasema: Niwashieni moto, wakauwasha, akasema: Ingieni humo, wakataka kuuingia, baadhi yao wakaanza kuwashika wenzao, huku wakisema: Tumeukimbia moto tukaelekea kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, waliendelea katika hali hiyo mpaka moto ukazima, zikatulia hasira zake, habari zikamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Laiti wangeingia wasingelitoka humo mpaka siku ya Kiyama; Utiifu unakuwa katika jambo jema".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alituma Jeshi Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akamfanya bwana mmoja katika Maanswari kuwa kiongozi wao, na akawaamrisha wamtii, yule kiongozi akawakasirikia na akasema kuwaambia: Hivi hakuwaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mnitii? Wakasema: Hasa! akasema: Basi nimekuamrisheni nikusanyieni kuni na muwashe moto kisha muingie humo, wakakusanya kuni na wakawasha moto, walipotaka kuingia humo, wakaanza kutazamana wao kwa wao. Na wakasema: Hakika sisi hatukumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake ila ni kwa sababu ya kuukimbia moto, je, tuuingie? wakiwa bado wako katika hali hiyo muwako wa moto ukazimika, na ikatoweka kwa kiongozi ghadhabu yake. Akaelezwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hilo akasema: Lau wangelimtii na wakaingia katika moto waliouwasha basi wangeliadhibiwa humo na wasingetoka kamwe kwa muda wa kubakia dunia, hakuna kumtii kiumbe katika kumuasi muumba; bali utiifu ni wajibu katika mambo mema na si katika maasi.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa kuwa utiifu unakuwa katika mema na wala hauwi katika maasi, hata kama amri itatoka kwa mtu ambaye ni wajibu kumtii.
  2. Mtenda maasi mwenye tauhidi ameahidiwa moto, lakini pia Mwenyezi Mungu anaweza kumsamehe.
  3. Sheria ya kuweka kiongozi vitani, na vile vile safarini.
Marejeo

صحيح البخاري (5/ 161) (4340). صحيح مسلم (3/ 1469) (1840). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (10/ 220).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com