Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Adabu za Dua.

Hadithi 5

Hujibiwa mmoja wenu anapokuwa hajafanya haraka: anasema: Nimemuomba Mola wangu, na wala sijaona ananijibu mimi

عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: يُستجاب لأحدكم ما لم يَعْجَلْ: يقول: قد دعوت ربي، فلم يستجب لي». وفي رواية لمسلم: «لا يزال يُستجاب للعبد ما لم يَدْعُ بإثم، أو قطيعة رحم، ما لم يَسْتَعْجِلْ» قيل: يا رسول الله ما الاستعجال؟ قال: «يقول: قد دعوت، وقد دعوت، فلم أر يستجب لي، فَيَسْتَحْسِرُ عند ذلك ويَدَعُ الدعاء».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- hadithi Marfu'u: "Hujibiwa mmoja wenu anapokuwa hajafanya haraka: anasema: Nimemuomba Mola wangu, na wala sijaona ananijibu mimi" Na katika riwaya ya Muslim: "Hatoacha kuendelea kujibiwa mja madam tu hajaomba dhambi, au kukata ukoo na madam hajafanya haraka" pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kufanya haraka? akasema: "Anasema: Nimeomba, hakika nimeomba, wala sijaona ananijibu, akakata tamaa na wakati huo akaacha kuomba".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwamba hujibiwa mja dua zake madam tu hajaomba kutenda maasi au kukata ukoo, na madam hajafanya haraka, pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kufanya haraka kunakoambatana na kuzuiliwa kujibiwa dua?, akasema: ni mtu kusema: Hakika nimeomba, na nimeomba, na nimerudia rudia kuomba, lakini hajanijibu; akafanya haraka wakati huo na akaacha kuomba.

Marejeo

- صحيح البخاري، للإمام محمد بن إسماعيل البخاري، تحقيق محمد الناصر، دار طوق النجاة. - صحيح مسلم، للإمام مسلم بن الحجاج النيسابوري، تحقيق محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي. - بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، تأليف سليم بن عيد الهلالي، دار ابن الجوزي، الطبعة الأولى، 1418ه. - نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، تأليف د. مصطفى سعيد الخِن وغيره، مؤسسة الرسالة، بيروت، الطبعة الرابعة عشرة، 1407هـ. - كنوز رياض الصالحين، لحمد بن ناصر العمار، دار كنوز إشبيليا، الطبعة الأولى، 1430ه. - دليل الفالحين لطرق رياض الصالحين، لمحمد علي بن محمد بن علان البكري الصديقي، اعتنى بها: خليل مأمون شيحا، دار المعرفة. - شرح رياض الصالحين، للشيخ محمد بن صالح العثيمين، مدار الوطن، الرياض، 1426هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakuna muislamu yeyote ataomba maombi yasiyokuwa ndani yake na kuomba dhambi wala kukata udugu, isipokuwa Allah atampa kwa maombi hayo moja kati ya mambo matatu: Moja ima amuharakishie maombi yake, au amlimbikizie ili amlipe siku ya Kiyama, au amuondoshee katika mabaya mfano wake" Wakasema: (Maswahaba) kwa hiyo tuzidishe? Akasema: "Allah ni mwenye kuzidisha mara dufu

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَدْعُو بِدَعْوَةٍ لَيْسَ فِيهَا إِثْمٌ، وَلَا قَطِيعَةُ رَحِمٍ، إِلَّا أَعْطَاهُ اللهُ بِهَا إِحْدَى ثَلَاثٍ: إِمَّا أَنْ تُعَجَّلَ لَهُ دَعْوَتُهُ، وَإِمَّا أَنْ يَدَّخِرَهَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ، وَإِمَّا أَنْ يَصْرِفَ عَنْهُ مِنَ السُّوءِ مِثْلَهَا» قَالُوا: إِذنْ نُكْثِرُ، قَالَ: «اللهُ أَكْثَرُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna muislamu yeyote ataomba maombi yasiyokuwa ndani yake na kuomba dhambi wala kukata udugu, isipokuwa Allah atampa kwa maombi hayo moja kati ya mambo matatu: Moja ima amuharakishie maombi yake, au amlimbikizie ili amlipe siku ya Kiyama, au amuondoshee katika mabaya mfano wake" Wakasema: (Maswahaba) kwa hiyo tuzidishe? Akasema: "Allah ni mwenye kuzidisha mara dufu".
Imepokelewa na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa muislamu atakapomuomba Mwenyezi Mungu na akamuomba maombi ambayo si dhambi, kama kumuomba amrahisishie maasi na dhulma, na wala akawa hakuomba kukata udugu; kama kuwaombea dua mbaya watoto wake au ndugu zake wa karibu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa kwa dua yake hiyo moja kati ya mambo matatu: Ima amharakishie dua yake na ampe alichoomba. Na ima Mwenyezi Mungu amcheleweshee mpaka siku ya Kiyama kwa kumpa daraja za juu zaidi, na rehema na msamaha kutokana na madhambi. Na ima amkinge katika dunia na mabaya mfano wake kwa kiwango cha dua. Maswahaba wakasema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kwa hivyo tukithirishe dua; ili tuweza kupata moja kati ya fadhila hizi? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni mengi na ni makubwa kuliko mnavyoviomba, kipawa chake hakimaliziki, na wala hakiishi.

Mafunzo
  1. Dua ya muislamu hujibiwa hairejeshwi lakini kwa sharti zake na adabu zake; ndio maana inampasa mja akithirishe dua na wala asitake haraka ya kujibiwa.
  2. Kujibiwa dua hakufungamani na kupata kilichoombwa; kwani anaweza kumfutia madhambi kwa dua yake, au akamlimbikizia Akhera.
  3. Amesema bin Bazi: Kung'ang'ania, na kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu, na kutokata tamaa, hizi ni miongoni mwa sababu kubwa za kujibiwa, ni juu ya kila mtu kung'ang'ania katika dua, na awe na dhana nzuri na Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka, na ajue kuwa yeye ni mwenye hekima na mjuzi, anaweza kuharakisha majibu kwa hekima, na anaweza kuyachelewesha kwa hekima, na anaweza kumpa muombaji kitu bora kuliko alichoomba.
Marejeo

مسند أحمد (17/ 213) (11133). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 592). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص805). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 54). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، للقاري (4/ 1537). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1020).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye haya Mkarimu, anamuonea haya mja wake atakapo nyanyua mikono yake kumuelekezea kisha amrejeshe patupu

عَنْ سَلْمَانَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ رَبَّكُمْ حَيِيٌّ كَرِيمٌ، يَسْتَحْيِي مِنْ عَبْدِهِ إِذَا رَفَعَ يَدَيْهِ إِلَيْهِ أَنْ يَرُدَّهُمَا صِفْرًا».
Na kutoka kwa Salmani -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye haya Mkarimu, anamuonea haya mja wake atakapo nyanyua mikono yake kumuelekezea kisha amrejeshe patupu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ibn MajahDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Anahimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kunyanyua mikono wakati wa dua, na akaeleza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu "huona haya" mwingi wa haya, na haachi kutoa, anamfanyia mja yenye kumfurahisha, na anaacha yenye kumdhuru, "Ni Mkarim" hutoa pasina kuombwa, je hali huwaje baada ya kuombwa! anamuonea haya mja wake muumini kuirejesha patupu mikono yake baada ya kuinyanyua kwa ajili ya dua ikiwa imefeli haina kitu kwa kutojibiwa.

Mafunzo
  1. Kila anapodhihirisha mwanadamu unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumuabudu, ndivyo inavyotarajiwa kwake kuwa na ukaribu wa kujibiwa.
  2. Himizo la kuomba dua, na kupendeza kunyanyua mikono ndani yake, nakuwa kufanya hivyo ni katika sababu za kujibiwa.
  3. Kumebainishwa upana wa ukarimu wa Mwenyezi Mungu na rehema yake kwa waja wake .
Marejeo

سنن أبي داود (2/ 609) (1488). سنن الترمذي (5/ 521) (3556). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، لعبد الله البسام (7/ 552). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 423). فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 483).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua fupi yenye kukusanya, na anaacha mengine yasiyokuwa hiyo

عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَسْتَحِبُّ الْجَوَامِعَ مِنَ الدُّعَاءِ، وَيَدَعُ مَا سِوَى ذَلِكَ.
Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua fupi yenye kukusanya, na anaacha mengine yasiyokuwa hiyo.
Imepokelewa na Abu Daud na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua zenye kukusanya kheri za dunia na Akhera ambazo matamshi yake ni machache na maana yake ni nyingi, na kunakuwa ndani yake na kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu, na malengo mazuri, na anaachana na yasiyokuwa hayo.

Mafunzo
  1. Kupendeza kuomba dua kwa matamshi machache yenye kukusanya maana nyingi za kheri, na karaha ya kujikalifisha na kujitia tabu katika kuomba, jambo ambalo ni kinyume na muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  2. Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipendelewa kwa kuwa na maneno machache yenye kukusanya maana pana.
  3. Kupupia yaliyothibiti kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliomba kwa maombi hayo; hata kama dua ikiwa ndefu, na maneno yake yakawa mengi, yote ni katika dua zilizokusanya maana pana.
Marejeo

سنن أبي داود (2/ 605) (1482). مسند أحمد (42/ 76) (25151). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 542). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1003). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 15). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 349).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Asiseme mmoja wenu: Ewe Mwenyzi Mungu nisamehe ukitaka, nirehemu ukitaka, niruzukua ukitaka, na adhamirie maombi yake, kwani yeye anafanya ayatakayo, hakuna wa kumlazimisha

عَن أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: «لاَ يَقُلْ أَحَدُكُمْ: اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي إِنْ شِئْتَ، ارْحَمْنِي إِنْ شِئْتَ، ارْزُقْنِي إِنْ شِئْتَ، وَليَعْزِمْ مَسْأَلَتَهُ، إِنَّهُ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ، لاَ مُكْرِهَ لَهُ». ولمسلم: «وَلَكِنْ لِيَعْزِمِ الْمَسْأَلَةَ وَلْيُعَظِّمِ الرَّغْبَةَ، فَإِنَّ اللهَ لَا يَتَعَاظَمُهُ شَيْءٌ أَعْطَاهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Asiseme mmoja wenu: Ewe Mwenyzi Mungu nisamehe ukitaka, nirehemu ukitaka, niruzukua ukitaka, na adhamirie maombi yake, kwani yeye anafanya ayatakayo, hakuna wa kumlazimisha". Na katika Sahihi Muslim: "Lakini adhamirie kuomba, na shauku yake iwe kubwa, kwa sababu Mwenyezi Mungu hakuna kinachofanywa kuwa kikubwa kwake ila hutoa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuitundika dua na chochote hata ikiwa kwa matashi ya Mwenyezi Mungu; kwa sababu hilo ni jambo linalojulikana na ni la uhakika kuwa hasamehi mpaka atake Mtukufu, na haina maana kuweka sharti la matashi; kwa sababu huwekwa sharti hilo kwa yule ambaye anaweza kufanya pasina kutaka kwa kulazimishwa na vinginevyo ambavyo Mwenyezi Mungu ametakasika navyo Mtukufu, na amelibainisha hilo rehema na amani ziwe juu yake mwisho wa hadithi kwa kauli yake kuwa hakuna wa kumlazimisha, kama Mwenyezi Mungu hakuna kinachokuzwa kwake ila anakitoa na wala hakuna kinachomshinda au kikawa kikubwa kwake chochote mpaka tuseme: Ukitaka, na kuutundika msamaha na matashi ni aina ya kutokuuhitaji msamaha wake, kauli ya mtu kusema: Ukitaka kunipa kadhaa basi nipe, huwa haitumiki kauli hiyo ila pale mtu anapokuwa hana haja au kwa asiyeweza, ama kwa anayeweza na pamoja na uhitaji wake basi anatakiwa kudhamiria kuomba, na aombe maombi ya masikini aliyedhikika mwenye uhitaji, na ajiweke karibu na Mwenyezi Mungu; kwa sababu yeye ndiye tajiri kamili, muweza juu ya kila kitu.

Mafunzo
  1. Katazo la kutundika dua na matashi.
  2. Kumtakasa Mwenyezi Mungu na yale asiyostahiki, na upana wa fadhila zake, na ukamilifu wa utajiri wake, na ukarimu wake na ukwasi wake Aliyetakasika na kutukuka.
  3. Kuthibitisha ukamilifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  4. Kukuza shauku kwa yale yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu na dhana nzuri kwake Mtukufu.
  5. Baadhi ya watu huingia katika kuitundika dua pasina wao kujua, mfano kama kauli: Allah akulipe kheri In shaa Allah, Allah amrehemu In shaa Allah, hii haifai kwa mujibu wa hadithi ya mlango huu.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 140) (7477). صحيح مسلم (4/ 2063) (2679). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص410). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص368). القول المفيد على كتاب التوحيد، لابن عثيمين (2/ 331).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com