Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Alisema kuniambia mimi Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Soma

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ لِي النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «اقْرَأْ عَلَيَّ»، قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَأَقْرَأُ عَلَيْكَ، وَعَلَيْكَ أُنْزِلَ؟ قَالَ: «نَعَمْ» فَقَرَأْتُ سُورَةَ النِّسَاءِ حَتَّى أَتَيْتُ إِلَى هَذِهِ الآيَةِ: {فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِنْ كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ، وَجِئْنَا بِكَ عَلَى هَؤُلاَءِ شَهِيدًا} [النساء: 41]، قَالَ: «حَسْبُكَ الآنَ» فَالْتَفَتُّ إِلَيْهِ، فَإِذَا عَيْنَاهُ تَذْرِفَانِ.
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Soma", Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Nikusomee vipi, na hali yakuwa Qur'ani iliteremka juu yako? Akasema: "Ndiyo" Nikasoma suratun Nisaai mpaka nikafika katika aya hii: "Basi itakuwaje pindi tukiwaletea kutoka kila Umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi wa hawa" [An-Nisaai: 41], Akasema: "Inatosha sasa" Nikamgeukia, ghafla nikaona macho yake yakibubujika machozi.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuomba Abdallah bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake amsomee chochote katika Qur'ani, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, vipi nikusomee na hali yakuwa Qur'ani iliteremshwa juu yako?! Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika mimi ninapenda kuisikia kutoka kwa mtu mwingine, akamsomea kutoka katika Suratun-Nisaai, alipofikia kauli yake Mtukufu: "Basi itakuwaje pindi tukiwaletea kutoka kila Umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi wa hawa". Yaani: Itakuwa vipi hali yako na hali ya Umma wako pindi tutakapokuleta kama shahidi juu ya Umma wako yakuwa wewe umewafikishia ujumbe wa Mola wako Mlezi, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Sasa, simama hapo katika kisomo chako, anasema bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake: Nikamgeukia ghafla nikaona macho yake yakibubujika machozi kwa hofu ya tukio hilo, na kwa kuuhurumia Umma wake.

Mafunzo
  1. Amesema Nawawi: Sunna ya kusikiliza Qur'ani na kuitegea sikio na kulia wakati ikisomwa, na kuizingatia, na sunna ya kuomba kusomewa na mtu mwingine ili umsikilize, na hii ni njia bora zaidi ya kuielewa na kuizingatia kuliko mtu kusoma mwenyewe.
  2. Kuisikiliza Qur'ani kuna malipo sawa na kuisoma.
  3. Ubora wa Abdallah bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake, kiasi kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipenda kusikia kutoka katika kinywa chake, na hii inaonyesha pupa ya bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake juu ya kuitafuta Qur'ani na kuihifadhi na kuidhibiti vizuri.
  4. Fadhila ya kulia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu wakati wa kusikia aya zake, ikiwa ni pamoja na kuzingatia kunyamaza, na kimya kizuri, na kutopiga makelele.
Marejeo

صحيح البخاري (6/ 196) (5050). صحيح مسلم (1/ 551) (800). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (7/ 133). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 515). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 402). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 342).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adabu za Usomaji Qur'ani na Ubebaji wa Qur'ani.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com