عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ لِي النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «اقْرَأْ عَلَيَّ»، قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَأَقْرَأُ عَلَيْكَ، وَعَلَيْكَ أُنْزِلَ؟ قَالَ: «نَعَمْ» فَقَرَأْتُ سُورَةَ النِّسَاءِ حَتَّى أَتَيْتُ إِلَى هَذِهِ الآيَةِ: {فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِنْ كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهِيدٍ، وَجِئْنَا بِكَ عَلَى هَؤُلاَءِ شَهِيدًا} [النساء: 41]، قَالَ: «حَسْبُكَ الآنَ» فَالْتَفَتُّ إِلَيْهِ، فَإِذَا عَيْنَاهُ تَذْرِفَانِ.
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Soma", Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Nikusomee vipi, na hali yakuwa Qur'ani iliteremka juu yako? Akasema: "Ndiyo" Nikasoma suratun Nisaai mpaka nikafika katika aya hii: "Basi itakuwaje pindi tukiwaletea kutoka kila Umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi wa hawa" [An-Nisaai: 41], Akasema: "Inatosha sasa" Nikamgeukia, ghafla nikaona macho yake yakibubujika machozi.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuomba Abdallah bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake amsomee chochote katika Qur'ani, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, vipi nikusomee na hali yakuwa Qur'ani iliteremshwa juu yako?! Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika mimi ninapenda kuisikia kutoka kwa mtu mwingine, akamsomea kutoka katika Suratun-Nisaai, alipofikia kauli yake Mtukufu: "Basi itakuwaje pindi tukiwaletea kutoka kila Umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi wa hawa". Yaani: Itakuwa vipi hali yako na hali ya Umma wako pindi tutakapokuleta kama shahidi juu ya Umma wako yakuwa wewe umewafikishia ujumbe wa Mola wako Mlezi, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Sasa, simama hapo katika kisomo chako, anasema bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake: Nikamgeukia ghafla nikaona macho yake yakibubujika machozi kwa hofu ya tukio hilo, na kwa kuuhurumia Umma wake.
Mafunzo
- Amesema Nawawi: Sunna ya kusikiliza Qur'ani na kuitegea sikio na kulia wakati ikisomwa, na kuizingatia, na sunna ya kuomba kusomewa na mtu mwingine ili umsikilize, na hii ni njia bora zaidi ya kuielewa na kuizingatia kuliko mtu kusoma mwenyewe.
- Kuisikiliza Qur'ani kuna malipo sawa na kuisoma.
- Ubora wa Abdallah bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake, kiasi kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipenda kusikia kutoka katika kinywa chake, na hii inaonyesha pupa ya bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake juu ya kuitafuta Qur'ani na kuihifadhi na kuidhibiti vizuri.
- Fadhila ya kulia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu wakati wa kusikia aya zake, ikiwa ni pamoja na kuzingatia kunyamaza, na kimya kizuri, na kutopiga makelele.
Marejeo
صحيح البخاري (6/ 196) (5050).
صحيح مسلم (1/ 551) (800).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (7/ 133).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 515).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 402).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 342).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّمَا مَثَلُ صَاحِبِ القُرْآنِ كَمَثَلِ صَاحِبِ الإِبِلِ المُعَقَّلَةِ، إِنْ عَاهَدَ عَلَيْهَا أَمْسَكَهَا، وَإِنْ أَطْلَقَهَا ذَهَبَتْ».
Imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema: "Hakika mfano wa mtu wa Qur'ani ni sawa na mfano wa mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa, akimuangalia kila mara atamzuia (kutoroka), na akimuachilia atatoroka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amemfananisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliyesoma Qur'ani na akakizoea kisomo chake sawa iwe kwa kutazama katika msahafu au kuhifadhi kwa moyo, na mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa kwa kamba ambazo hufungiwa wanyama, akimtazama mara kwa mara ataendelea kumshika na kumzuia, na akiacha kumfunga na kumtazama basi ataondoka na kutoroka, akianza kusoma Qur'ani msomaji wa Qur'ani basi huikumbuka, na asipoisoma basi ataisahau; madam kudumu kuisoma kutaendelea basi hifdhi yake itaendelea kubakia.
Mafunzo
- Himizo la kushikamana na Qur'ani na kuisoma, na tahadhari ya kutumbukia katika kuisahau.
- Kudumu kuisoma Qur'ani huudhalilisha ulimi na huurahisishia kuisoma kwake, akiihama inakuwa nzito kwake na inampa tabu.
- Amesema Kadhi: Na maana ya "Mwenye Qur'ani" Yaani: Aliyeizoea, na kusuhubiana: Ni kuzoea, na hukusudiwa: Fulani ni jamaa wa fulani, na watu wa peponi na watu wa motoni.
- Miongoni mwa njia za ufundishaji ni kupiga mifano.
- Amesema bin Hajari: Na amemtaja ngamia pekee; kwa sababu ndio mnyama pekee anayetoroka haraka zaidi katika wanyama wafugwao na binadamu, na kumkamata kwake baada ya kutoroka ni kazi ngumu sana.
Marejeo
صحيح البخاري (6/ 193) (5031).
صحيح مسلم (1/ 543) (789).
شرح صحيح مسلم، للنووي (6/ 77).
فيض القدير شرح الجامع الصغير، لعبدالرؤوف المناوي (3/ 3).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (13/ 12).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ السُّلَمي رحمه الله قَالَ: حَدَّثَنَا مَنْ كَانَ يُقْرِئُنَا مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُمْ كَانُوا يَقْتَرِئُونَ مِنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَشْرَ آيَاتٍ، فَلَا يَأْخُذُونَ فِي الْعَشْرِ الْأُخْرَى حَتَّى يَعْلَمُوا مَا فِي هَذِهِ مِنَ الْعِلْمِ وَالْعَمَلِ، قَالُوا: فَعَلِمْنَا الْعِلْمَ وَالْعَمَلَ.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Abdulrahman Al-Sulamiy- Mwenyezi Mungu amrehemu amesema: Ametusimulia mmoja miongoni mwa waliokuwa wakitusomea Qur'ani katika Maswahaba wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- walikuwa wakitusomea Aya kumi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hivyo hawakuwa wakichukua Aya kumi zingine mpaka wawe wamekwishayafanyia kazi yaliyo ndani ya aya hizo kumi kwa kujifunza na kuyafanyia kazi, wakasema: Basi tukajifunza elimu na kuifanyia kazi.
Imepokelewa na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Walikuwa Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- wakipokea Aya kumi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na hawakuwa wakihama kwenda Aya zingine mpaka wawe wamekwishajifunza elimu liyopo kwenye hizo Aya kumi, na wanazifanyia kazi, hivyo wakajifunza elimu pamoja na kuifanyia kazi.
Mafunzo
- Ubora wa Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, na pupa yao ya kujifunza Qur'ani.
- Kujifunza Qur'ani kunakuwa kwa kujifunza na kufanyia kazi yaliyopo ndani yake na kuyafanyia kazi, na siyo kuisoma na kuihifadhi peke yake.
- Elimu inakuwa kabla ya maneno na vitendo.
Marejeo
مسند أحمد (38/ 466) (23482).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ جُنْدُبِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَنَحْنُ فِتْيَانٌ حَزَاوِرَةٌ، فَتَعَلَّمْنَا الإِيمَانَ قَبْلَ أَنْ نَتَعَلَّمَ القُرْآنَ، ثُمَّ تَعَلَّمْنَا القُرْآنَ، فَازْدَدْنَا بِهِ إِيمَانًا.
Imepokelewa kutoka kwa Jundubu bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Tulikuwa pamoja Mtume rehema na amani ziwe juu yake nasi tukiwa vijana karibu na balehe, tukajifunza imani kabla ya kujifunza Qur'ani, kisha tukajifunza Qur'ani, tukaongeza imani kupitia Qur'ani.
Imepokelewa na Ibnu MaajahDarajaSahihi
Maelezo
Amesema Jundubu bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake nasi tukiwa vijana tuliokaribia kubalehe, wenye nguvu na wakali, tukajifunza kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake imani kabla ya kujifunza Qur'ani, kisha tukajifunza Qur'ani; tukazidisha imani kupitia Qur'ani.
Mafunzo
- Kumebainishwa kuwa imani inazidi na kupungua.
- Kupangilia vipaumbele wakati wa kumlea kijana anaekua, na pupa ya kuwajaza imani.
- Qur'ani huzidisha imani, na moyo hung'aa kupitia hiyo, na kifua hukunjuka.
Marejeo
سنن ابن ماجه (1/ 42) (61).
مشارق الأنوار الوهاجة ومطالع الأسرار البهاجة في شرح سنن الإمام ابن ماجه (2/ 255).
مرشد ذوي الحجا والحاجة إلى سنن ابن ماجه والقول المكتفى على سنن المصطفى (1/ 227).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُقْرِئُنَا القُرْآنَ عَلَى كُلِّ حَالٍ مَا لَمْ يَكُنْ جُنُبًا.
Kutoka kwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitusomesha Qur'ani katika kila hali madamu hana janaba.
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwafundisha Maswahaba zake Qur'ani na akiwasomesha yeye mwenyewe katika hali zote madam hajawa katika hali ya janaba litokanalo na tendo la ndoa kwa wakeze.
Mafunzo
- Kutofaa kusoma Qur'ani kwa mwenye janaba mpaka aoge.
- Kufundisha kwa vitendo.
Marejeo
سنن الترمذي (1/ 214) (146).
سنن أبي داود (1/ 164) (229).
سنن النسائي (1/ 144) (265).
سنن ابن ماجه (1/ 375) (594).
مسند أحمد (2/ 61) (627).
النهاية في غريب الحديث والأثر (917-167).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com