Maswahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hivi hawezi mmoja wenu kupata katika kila siku mema elfu moja?! Akasema mmoja kati ya waliokaa naye: Ni vipi atapata mtu mema elfu moja kwa siku kwa wepesi? Akasema: Aseme: "Sub-haana llaah" Yaani: Ametakasika Mwenyezi Mungu, mara mia moja; basi hapo ataandikiwa mema elfu moja; kwa sababu jema moja hulipwa mara kumi mfano wake, au yatafutwa kwake makosa elfu moja.
- Himizo la kufanya mazuri; kwa sababu ndio ngazi ya kumfikisha mtu katika utiifu.
- Ubora wa kufanya tasbihi (kusema: Sub-haana llaah) na kumtaja Mwenyezi Mungu, na kwamba kazi hii nyepesi ambayo haimgharimu mtu chochote, anapata malipo makubwa kupitia amali hiii.
- Hima ya Maswahaba katika kuziendea kheri pasina kuchelewa.
- Kuzidishwa kwa mema mpaka mara kumi mfano wake, na hiyo ni kama kauli yake Mtukufu: "Yeyote atakayekuja na jema moja basi atalipwa mara kumi mfano wake" [Al-An'aam:160], na hii ndio daraja ya chini kabisa ya kuzidishiwa, kwani imekuja kuwa ziada hufika mpaka mia saba mara dufu.
- Imekuja katika baadhi ya riwaya badala ya (Au) imekuja (Na) katika kauli yake: Au amfutie kwake...Anasema Al-Qaari: Herufi (Wau/na) inaweza kuja ikimaanisha (Au) na riwaya zote hazipingani, maana yake ni kana kwamba: Atakayelisema neno hilo, ataandikiwa mema elfu moja, na asipoandikiwa basi anafutiwa baadhi ya makosa na anachuma malipo kwa sehemu nyingine, na inawezekana kuwa kwa maana ya (Wau/na) au kwa maana ya (Bal/bali) basi hapo atakusanyiwa mambo yote, na fadhila za Mwenyezi Mungu ni pana mno, mwisho wa kunukuu, yaani: Maana yake nikuwa ataandikiwa mema elfu moja na atafutiwa kwake madhambi elfu moja.
صحيح مسلم (4/ 2073) (2698). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 507). مرقاة المفاتيح، لعلي القاري (4/ 1594). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 980). مرعاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعبيد الله المباركفوري (7/ 454).