عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللهِ رضي الله عنهما أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إِذَا دَخَلَ الرَّجُلُ بَيْتَهُ، فَذَكَرَ اللهَ عِنْدَ دُخُولِهِ وَعِنْدَ طَعَامِهِ، قَالَ الشَّيْطَانُ: لَا مَبِيتَ لَكُمْ، وَلَا عَشَاءَ، وَإِذَا دَخَلَ، فَلَمْ يَذْكُرِ اللهَ عِنْدَ دُخُولِهِ، قَالَ الشَّيْطَانُ: أَدْرَكْتُمُ الْمَبِيتَ، وَإِذَا لَمْ يَذْكُرِ اللهَ عِنْدَ طَعَامِهِ، قَالَ: أَدْرَكْتُمُ الْمَبِيتَ وَالْعَشَاءَ».
ImepokelewaKutoka kwa Jabir radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, hakika yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Anapoingia mtu nyumbani kwake akamtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake na wakati wa chakula chake, Shetani husema: Hakuna malazi kwenu, wala chakula cha usiku, na anapoingia na hakumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake, Shetani husema: Mmepata malazi, na asipomtaja Mwenyezi Mungu wakati wa chakula chake, husema: Mmepata malazi na chakula cha usiku".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumtaja Allah wakati wa kuingia nyumbani na kabla ya kupata chakula, nakuwa mtu akimtaja Mwenyezi Mungu kwa kusema: (Bismillaah) -Naanza kwa jina la Mwenyezi Mungu- wakati wa kuingia nyumbani kwake na wakati wa chakula chake, Shetani husema kuwaambia wasaidizi wake: Hamna bahati leo ya kupata malazi wala chakula cha usiku ndani ya nyumba hii ambayo mwenye nyumba kajilinda kutokana nanyi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na ama mtu akiingia nyumbani kwake na akawa hakumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake wala wakati wa kupata kwake chakula, Shetani huwaeleza wasaidizi wake kuwa wamepata mahali pa kulala, na chakula cha usiku ndani ya nyumba hii.
Mafunzo
- Ni sunna kumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia nyumbani na wakati wa chakula, kwani Shetani hulala ndani ya majumba, na hula katika chakula cha wenye nyumba ikiwa hawatomtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Shetani humfuatilia mwanadamu katika matendo yake na harakati zake na katika mambo yake yote, akijisahau kumtaja Allah papo hapo hupata lengo lake kwake.
- Kumtaja Allah humfukuza Shetani.
- Kila Shetani anawafuasi na ana vipenzi ambao huchukua ushauri wake na kufuata amri yake.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1598) (2018).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 50).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل المبارك (ص467).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 190).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 700).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضيَ اللهُ عنهما أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَقُولُ: «اللهُمَّ لَكَ أَسْلَمْتُ، وَبِكَ آمَنْتُ، وَعَلَيْكَ تَوَكَّلْتُ، وَإِلَيْكَ أَنَبْتُ، وَبِكَ خَاصَمْتُ، اللهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِعِزَّتِكَ، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ أَنْ تُضِلَّنِي، أَنْتَ الْحَيُّ الَّذِي لَا يَمُوتُ، وَالْجِنُّ وَالْإِنْسُ يَمُوتُونَ».
Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako nimejisalimisha, na kwako nimeamini, na juu yako nimetegemea, na kwako nimejisogeza, na kwa ajili yako napambana. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kwa utukufu wako hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe najikinga kwa kuto nipoteza, wewe ndiye uliye hai ambaye hafi, na majini na watu wanakufa".
Hadithi hii imepokelewa na Bukhari na Muslim, na matamshi haya ni ya Muslim, na akaipokea Bukhari kwa ufupiDarajaSahihi
Maelezo
Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako nimejisalimisha" na nimenyenyekea, "na kwako nimeamini" na nimesadikisha na nimekiri, "Na juu yako nimetegemea" na nimekabidhi na nimetegemea, "na kwako nimetubia" na nimerejea na nimekuja, "na kwako ninapambana" na ninajibizana kwa hoja na maadui zako, "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajilinda kwako" Ninajiegemeza, "kwa utukufu wako" na ngome yako na ushindi wako, "hapana mola wa haki isipokuwa wewe" na wala hakuna muabudiwa wa haki zaidi yako, "unipoteze" kutoka katika uongofu na taufiki ya kupata radhi zako, "Wewe ndiye uliye hai ambaye hafi" na wala hamaliziki, "na majini na watu wote wanakufa".
Mafunzo
- Sheria ya kutanguliza sifa katika kila mahitaji.
- Ulazima wa kutegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake na kuomba hifadhi kutoka kwake; kwa sababu yeye ndiye mwenye kusifika kwa sifa kamilifu, basi yeye peke yake yake ndiye mwenye kutegemewa, na viumbe wote hawajiwezi na mwisho wao ni kifo, hivyo wao hawastahiki kutegemewa.
- Kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika dua kwa maneno haya yaliyokusanya kila kitu, na yenye kuzuia kingenecho kuingia humo, yanayoelezea kwa imani ya kweli na yakini ya kiwango cha juu.
- Amesema As-Sa'diy: Kauli yake: "Wewe ndiye uliye hai" Yaani: Wewe pekee ndiye unayestahiki kuombwa kinga na si mwingine zaidi yako.
Marejeo
صحيح البخاري (9/ 117) (7383).
صحيح مسلم (4/ 2086) (2717).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص72).
فتح رب البرية بتلخيص الحموية، لابن عثيمين (ص79).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 109).
مرعاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، عبيد الله المباركفوري (8/ 223).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن الْأَغَرِّ رضي الله عنه، وَكَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يَا أَيُّهَا النَّاسُ تُوبُوا إِلَى اللهِ، فَإِنِّي أَتُوبُ فِي الْيَوْمِ إِلَيْهِ مِائَةَ مَرَّةٍ».
Kutoka kwa Agharri radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Enyi watu, tubieni kwa Mwenyezi Mungu, kwani mimi ninatubia kwa siku mara mia moja".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu kukithirisha kuomba toba na msamaha, na anajielezea mwenyewe kuwa yeye hutubia kwa Mwneyezi Mungu Mtukufu na kumuomba msamaha kwa siku zaidi ya mara mia moja, na haliyakuwa alikwisha samehewa yaliyotangulia katika madhambi yake na yajayo, na katika hilo kuna ukamilifu wa kujidhalilisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
Mafunzo
- Kila mmoja vyovyote itakavyokuwa nafasi yake na daraja lake katika imani, basi anahitaji kurejea kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na kuikamilisha nafsi yake kwa toba, nakuwa kila mmoja hakosi mapungufu katika kutimiza haki za Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka: "Na tubieni kwa Mwenyezi Mungu nyote enyi waumini".
- Toba ni kwa mambo yote, sawa sawa kwa kufanya maharamisho au madhambi au uzembe katika kutimiza wajibu.
- Ikhlasi (kutakasa nia) katika toba ni sharti la kukubaliwa kwake, atakayeacha dhambi kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu huyo bado hajatubia.
- Amesema Nawawi: Toba ina masharti matatu: Ajivue katika maasi, na ajute kwa kuyafanya, na atie dhamira ya kweli ya kutorudi katika maasi mfano wake kabisa, na ikiwa maasi yanahusiana na haki ya binadamu basi kuna sharti la nne, nalo: Kurudisha haki aliyodhulumu kwa mwenye nayo, na kujivua nayo.
- Tahadhari: Kuomba msamaha kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuna maana kuwa kuna madhambi aliyafanya, lakini ni kwa sababu ya ukamilifu wa utumwa wake na kufungamana kwake na kumtaja Aliyetakasika na kutukuka, na kuvuta kwake taswira ya utukufu wa haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na upungufu wa mja kwa namna yoyote atakayofanya katika kushukuru neema zake, nayo inakuwa ni sehemu ya kuwawekea sheria umma wake baada yake, na hukumu zinginezo.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2075) (2702).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 33).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 97).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 52).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه: أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَقُولُ فِي سُجُودِهِ: «اللهُمَّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي كُلَّهُ دِقَّهُ، وَجِلَّهُ، وَأَوَّلَهُ وَآخِرَهُ وَعَلَانِيَتَهُ وَسِرَّهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema katika sijida yake: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe mimi dhambi zangu ndogo zake na kubwa zake za mwanzo wake na mwisho wake, za wazi zake na za siri zake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiomba katika sijida yake akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe madhambi yangu" Kwa kuyasitiri, na unikinge na madhara yake; uyasamehe na usiyatazame na uyafute, "yote", nakusudia: "Za ndani" ndogo zake, na chache zake, "pana zake" kubwa zake na nyingi zake, "za mwanzo wake" dhambi ya kwanza, "na za mwisho zake", na zilizo kati yake, "za wazi zake na siri zake" miongoni mwa zile asizozijua yeyote ila wewe Uliyetakasika.
Mafunzo
- Amesema bin Qayyim: Na kuomba kusamehewa madhambi madogo na makubwa, ya ndani na ya juu, ya mwanzo na ya mwisho, ya siri na ya wazi, kukusanya huku na kueneza huku kwa sababu anataka ikija toba ije kwa yote anayoyajua mja miongoni mwa madhambi, na yale asiyoyajua.
- Imesemekana kuwa: Alitanguliza "Ya ndani" kabla ya " juu"; kwa sababu muombaji huanza na cha chini kisha anakwenda anapanda, yaani anapanda juu, kwa sababu madhambi makubwa mara nyingi hutokea kwa sababu ya kuendelea na madhambi madogo na kutojali, ni kana kwamba ni njia ya kuyaendea madhambi makubwa, na kinachokuwa ni sababu kina haki ya kutangulizwa kwa ajili ya kuthibitisha na kupandia kwenda juu.
- Kujinyenyekeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumuomba msamaha kutokana na madhambi yote, madogo na makubwa.
- Amesema Nawawi: Hapa kuna msisitizo wa dua na kukithirisha matamshi yake hata kama baadhi yake yatatosheleza mengine.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 350) (483).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 506).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص780).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 509).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 111).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 979).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ سَعْدٍ رضي الله عنها قَالَ: جَاءَ أَعْرَابِيٌّ إِلَى رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: عَلِّمْنِي كَلَامًا أَقُولُهُ، قَالَ: «قُلْ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، اللهُ أَكْبَرُ كَبِيرًا، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثِيرًا، سُبْحَانَ اللهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ، لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ» قَالَ: فَهَؤُلَاءِ لِرَبِّي، فَمَا لِي؟ قَالَ: «قُلْ: اللهُمَّ اغْفِرْ لِي وَارْحَمْنِي وَاهْدِنِي وَارْزُقْنِي».
Kutoka kwa Sa'di radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuja bedui kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: Nifundishe maneno nitakayoyasema. Akasema "Sema: Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiyekuwa na mshirika, Mwenyezi Mungu mkubwa mno, na kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu kwa wingi, na ametakasika Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu, na hapana ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu mwenye nguvu na hekima" Akasema: Haya ni kwa ajili ya Mola wangu, yako wapi ya kwangu? Akasema: "Sema: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe mimi na unihurumie na uniongoze na uniruzuku".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Mtu mmoja miongoni mwa watu wa kijijini alimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amfundishe dhikiri atakayokuwa akiisema, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Sema: "Laa ilaaha illa llaah wahdahu laa shariika lahu" (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika wake) Ameanza kwa shahada ya tauhidi, na maana yake hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, "Allaahu Akbaru kabiira" Yaani: Mwenyezi Mungu ni mkubwa kuliko kila kitu na ni Mtukufu, "Na Alhamdulillaahi kathira" Yaani: Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu kwa wingi, kwa sifa zake na vitendo vyake na neema zake zisizohesabika, "Sub-haanallaahi rabbil Aalamiin" Yaani: Ametukuka na kutakasika na kila mapungufu, "Laa haulaa walaa quwwata illaa billaahil Azizil Hakiim" Yaani: Hakuna namna ya kugeuka kutoka hali moja kwenda hali nyingine isipokuwa kwa uweza wa Allah na msaada wake na taufiki yake, Yule bwana akasema: Maneno haya ni kwa ajili ya Mola wangu Mlezi, kwa kumtaja yeye na kumtukuza, ya kwangu mimi ya kujiombea mwenyewe yako wapi? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Sema: "Ewe Mola wangu nisamehe" Kwa kuyafuta madhambi na kuyasitiri, "Na unihurumie" Kwa kuniletea manufaa na masilahi ya dini na dunia kwangu, "Na uniongoze" Kwenda katika hali nzuri na katika njia iliyonyooka, "Na uniruzuku" Mali ya halali na siha na kila aina ya kheri na afya.
Mafunzo
- Kuna himizo la kumtaja Mwenyezi Mungu kwa neno 'Laa ilaaha illa llaah, na Allaahu Akbar, na Alhamdulillaah, na Sub-haanallaah.
- Ni sunna kumtaja Mwenyezi Mungu na kumsifu kabla ya kumuomba.
- Ni suuna mtu kuomba kwa dua nzuri, na kwa dua zilizopokelewa toka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, ambazo zimekusanya kila aina ya kheri za Dunia na Akhera, na ana uhuru wa kuomba akitakacho.
- Inampasa mja apupie kujifunza yale yenye kumnufaisha katika Dunia na Akhera.
- Himizo la kuomba msamaha na huruma na riziki, kwani mambo haya yamekusanya kheri zote.
- Huruma yake rehema na amani ziwe juu yake katika kuufundisha umma wake yale yenye kuwanufaisha.
- Imetajwa huruma baada ya msamaha ili usafi ukamilike,na msamaha ni kusitiriwa makosa na kufutwa kwake na kuepushwa na moto, na huruma ni kufikishiwa kheri na kuingia peponi, na huku ndiko kufaulu kukubwa.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2072) (2696).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 498).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 972).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (4/ 1606).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com