Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Adabu za kumtembelea mgonjwa.

Hadithi 2

Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni tano: Kujibu salamu, na kumtembelea mgonjwa, na kufuata jeneza, na kuitika wito, na kumuombea dua mwenye kupiga chafya

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «حَقُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ خَمْسٌ: رَدُّ السَّلَامِ، وَعِيَادَةُ الْمَرِيضِ، وَاتِّبَاعُ الْجَنَائِزِ، وَإِجَابَةُ الدَّعْوَةِ، وَتَشْمِيتُ الْعَاطِسِ».
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni tano: Kujibu salamu, na kumtembelea mgonjwa, na kufuata jeneza, na kuitika wito, na kumuombea dua mwenye kupiga chafya".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baadhi ya haki za muislamu juu ya ndugu yake muislamu, Haki ya kwanza katika hizi ni kujibu salamu kwa atakayekutolea salamu. Haki ya pili: Kumtembelea mgonjwa na kumzuru. Haki ya tatu: Kulifuata jeneza kutoka nyumbani kwake mpaka mahali pa kuswalia mpaka makaburini mpaka kuzika. Haki ya nne: Kuitika wito anapomuita kuja katika walima wa harusi na mengineyo. Haki ya tano: Kumuombea dua mwenye kupiga chafya, nako ni kumwambia -Yarhamukallaah- (Akuhurumie Mwenyezi Mungu) atakapomhimidi Allah kwa kusema (Al-hamdulillah): kisha mpiga chafya amjibu: -Yahdiikumullaahu wayuslih baalakum- (Akuongozeni Allah na akutengenezeeni mambo yenu).

Mafunzo
  1. Utukufu wa Uislamu katika kuzitilia mkazo haki baina ya waislamu na kuupa nguvu udugu na mapenzi kati yao.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 71) (1240). صحيح مسلم (4/ 1704) (2162). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (4/ 512). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 327). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 253). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 591). بهجة قلوب الأبرار، لابن سعدي (ص81).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ondosha tatizo, ewe Mola wa watu, na ponya kwani wewe ndiye mponyaji, hakuna ponyo ila ponyo lako, ponyo lisiloacha ugonjwa

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمنينَ رَضيَ اللهُ عنها قَالَت: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا أَتَى الْمَرِيضَ يَدْعُو لَهُ قَالَ: «أَذْهِبِ الْبَاسَ، رَبَّ النَّاسِ، وَاشْفِ أَنْتَ الشَّافِي، لَا شِفَاءَ إِلَّا شِفَاؤُكَ، شِفَاءً لَا يُغَادِرُ سَقَمًا».
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapomuendea mgonjwa basi anamuombea dua, anasema "Ondosha tatizo, ewe Mola wa watu, na ponya kwani wewe ndiye mponyaji, hakuna ponyo ila ponyo lako, ponyo lisiloacha ugonjwa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapomtembelea mgonjwa anamuombea dua kwa kusema: Ewe Mwenyezi Mungu "Ondoa" ondosha "ugumu" na ukali wa maradhi, "Ewe Mola wa watu" na Muumba wao na Mlezi wao, "na ponya" maradhi haya "wewe" Mtukufu "Ndiye mponyaji" na ninaomba kupitia jina lako Mponyaji, "hakuna ponyo" linaloweza kupatikana kwa mgonjwa "isipokuwa ponyo lako" na afya yako, "ponyo" la moja kwa moja "lisiloacha" na kubakisha na kuacha "ugonjwa" na maradhi mengine.

Mafunzo
  1. Mponyaji ni Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na daktari na dawa hivyo vyote ni sababu, havinufaishi wala havidhuru isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
  2. Kumtembelea mgonjwa ni katika haki zilizoko baina ya waislamu, nayo kwa familia inakuwa ni haki zaidi.
  3. Himizo kwa mwenye kumtembelea mgonjwa amuombee dua hii yenye baraka na iliyonukuliwa kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  4. Miongoni mwa muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kujitibu kwa kisomo (cha Ruqya) ya kisheria kwa Qur'ani na dua nzuri, alikuwa rehema na amani ziwe juu yake akijisomea mwenyewe anapougua, na vile vile alikuwa akimsomea yeyote mwenye kuhisi maumivu katika familia yake na watu wengine pia.
  5. Amesema bin Hajari: Na imewatatiza baadhi ya watu dua ya kumuombea mgonjwa kupona hali yakuwa katika maradhi kuna kufutiwa madhambi na kupata thawabu kama zilivyokuja hadithi kwa wingi kuhusu hilo, na jawabu la hilo: Nikuwa dua ni ibada, na wala haiondoi thawabu na kufutiwa makosa; kwa sababu hayo hupatikana mwanzoni mwa ugonjwa na pale mtu anaposubiri juu ya maradhi, na muombaji anakuwa kati ya neema mbili: Ima apate lengo lake, au apewe badala kwa kuletewa manufaa au kuzuiliwa madhara, na yote hayo ni kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 134) (5750). صحيح مسلم (4/ 1721) (2191). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 162). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 477). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (11/ 539). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 687).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com