Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa hakatai marashi
عن أنس بن مالك رضي الله عنه: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ لَا يَرُدُّ الطِّيبَ.
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa hakatai marashi.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Ilikuwa katika muongozo wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa hakatai marashi na anayapokea; kwa sababu ni mepesi kubebeka na yana harufu nzuri.
Mafunzo
- Inapendeza kukubali zawadi ya marashi; kwa sababu hakuna tabu kuyabeba kwake na wala hakuna masimango ikiwa mtu atayakubali.
- Ukamilifu na tabia njema za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kutokataa marashi, na kukubali zawadi ya yeyote mwenye kumzawadia.
- Himizo la kutumia marashi.
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 157) (2582). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 560). منار القاري شرح مختصر صحيح البخاري، لحمزة قاسم (4/ 9). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخن وغيره (2/ 1213).