Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Adabu za kuona Ndoto

Hadithi 4

Atakapoota mmoja wenu ndoto anayoipenda basi ndoto hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo, amshukuru Mwenyezi Mungu kwa ndoto hiyo na aisimulie, na akiota ndoto kinyume na hiyo katika yale anayoyachukia, basi ndoto hiyo inatokana na Shetani, basi aombe kinga kutokana na shari yake, na wala asiisimulie kwa yeyote, kwani haitomdhuru

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رضي الله عنه أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إِذَا رَأَى أَحَدُكُمُ الرُّؤْيَا يُحِبُّهَا فَإِنَّهَا مِنَ اللَّهِ، فَلْيَحْمَدِ اللَّهَ عَلَيْهَا وَلْيُحَدِّثْ بِهَا، وَإِذَا رَأَى غَيْرَ ذَلِكَ مِمَّا يَكْرَهُ، فَإِنَّمَا هِيَ مِنَ الشَّيْطَانِ، فَلْيَسْتَعِذْ مِنْ شَرِّهَا، وَلاَ يَذْكُرْهَا لِأَحَدٍ، فَإِنَّهَا لَنْ تَضُرَّهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakapoota mmoja wenu ndoto anayoipenda basi ndoto hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo, amshukuru Mwenyezi Mungu kwa ndoto hiyo na aisimulie, na akiota ndoto kinyume na hiyo katika yale anayoyachukia, basi ndoto hiyo inatokana na Shetani, basi aombe kinga kutokana na shari yake, na wala asiisimulie kwa yeyote, kwani haitomdhuru".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema amani ziwe juu yake kuwa ndoto njema yenye kufurahisha usingizini hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na akaeleza amshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo, na akiota yanayomchukiza na kumhuzunisha basi hayo yanatokana na Shetani; aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake, na wala asimsimulie yeyote; kwani ndoto hiyo haitomdhuru, kwani Mwenyezi Mungu ameyafanya hayo yaliyotajwa kuwa ni sababu ya kusalimika na kero zinazoambatana na ndoto.

Mafunzo
  1. Migawanyiko ya ndoto: 1- Ndoto njema, nayo ni ndoto ya kweli na ni habari njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu anayoiona mtu au ikaonwa na mtu mwingine. 2- Mawazo: Nayo ni yale ambayo mtu huwaza mwenyewe akiwa macho. 3- Kutiwa huzuni na hofu na Shetani na vitisho kutoka kwake ili amuhuzunishe mwanadam.
  2. Uhalisia wa haya yaliyotajwa katika mlango wa ndoto njema ni mambo matatu: Amshukuru Mwenyezi Mungu juu ya ndoto hiyo, na ajipe habari njema, na aihadithie, lakini asimueleze ila yule anayempenda nasi anayemchukia.
  3. Na uhalisia wa hayo yaliyotajwa katika adabu za ndoto zenye kuchukiza ni mambo matano: Ajikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake, na kutokana na shari ya Shetani, na ateme kushoto mara tatu pale anaposhituka kutoka usingizini mwake, na wala asiisimulie kamwe kwa yeyote, na anapotaka kurejea katika usingizi wake basi ageukie ubavu mwingine tofauti na ule aliokuwa mwanzo; kwani ndoto hiyo wala haitomdhuru.
  4. Amesema bin Hajari: Hekima na lengo la kukatazwa kumsimulia asiyempenda nikuwa endapo atamsimulia huenda akamfasiria kwa mambo yenye kumchukiza, ima kwa sababu ya chuki au husuda, na huenda ikatokea kwa namna ile ile aliyomfasiria au akajiwahi mwenyewe kwa kuanza kuhuzunika na kukosa furaha, akaamrisha kuacha kumhadithia asiyempenda kwa sababu hiyo.
  5. Kushukuru pale zinapotokea neema, na kujirudiarudia kwa mazuri, hilo ni sababu ya kuyadumisha mazuri hayo.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 43) (7045). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (11/ 181). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 370). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص510). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 124). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 657).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ndoto njema hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ndoto mbaya hutoka kwa Shetani, atakapoota mmoja wenu ndoto mbaya anayoiogopa basi na ateme kushotoni kwake, na aombe ulinzi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari zake, kwani ndoto hiyo haitomdhuru

عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ مِنَ اللَّهِ، وَالحُلُمُ مِنَ الشَّيْطَانِ، فَإِذَا حَلَمَ أَحَدُكُمْ حُلُمًا يَخَافُهُ فَلْيَبْصُقْ عَنْ يَسَارِهِ، وَلْيَتَعَوَّذْ بِاللَّهِ مِنْ شَرِّهَا، فَإِنَّهَا لاَ تَضُرُّهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Katada -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Ndoto njema hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ndoto mbaya hutoka kwa Shetani, atakapoota mmoja wenu ndoto mbaya anayoiogopa basi na ateme kushotoni kwake, na aombe ulinzi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari zake, kwani ndoto hiyo haitomdhuru".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ndoto nzuri yenye kufurahisha usingizini hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na mtu kuota anayoyachukia na kumhuzunisha hutoka kwa Shetani. Atakayeota yanayomchukiza basi ateme kushotoni kwake, na aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake; kwani haitomdhuru, kiasi ambacho Mwenyezi Mungu amefanya hayo yaliyotajwa kuwa ni sababu ya kusalimika na hayo yenye kuchukiza yanayoambatana na ndoto.

Mafunzo
  1. Ndoto nzuri na mbaya ni yale mambo anayoyaona mtu aliyelala, lakini ndoto nzuri nyingi ni zile anazoota mtu katika mambo ya kheri au mambo mazuri, na ndoto nyingi mbaya huwa katika yale anayoyaona mtu katika mambo ya shari na mabaya, kila moja kati ya hayo hukaa mahala pa lingine.
  2. Migawanyiko ya ndoto: 1- Ndoto njema, nayo ni ndoto ya kweli na ni bishara kutoka kwa Mwenyezi Mungu anayoiona au ikaonwa na mtu mwingine kwake, 2- Mazungumzo ya nafsi, nayo ni yale ambayo mtu huzungumza na nafsi yake akiwa macho (kisha yanajirudia akiwa usingizini), 3- Huzuni na hofu ya Shetani na vitisho vyake ili tu amhuzunishe mwanadamu.
  3. Jambo la msingi katika mambo yaliyotajwa katika milango ya ndoto ni mambo matatu: Amshukuru Mwenyezi Mungu kwa ndoto hiyo, na ajipe bishara njema kwayo, na aihadithie lakini kwa yule anayempenda na si kwa anayemchukia.
  4. Na la msingi katika yale yaliyotajwa katika adabu za ndoto mbaya ni mambo matano: Ajilinde kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake, na kutokana na shari ya Shetani, na ateme pale tu anashituka kutoka usingizini upande wa kushoto mara tatu, na kamwe asiisimulie kwa yeyote, na akitaka kurudi katika usingizi wake basi abadili ubavu aliokuwa awali; kwani ndoto hiyo haitomdhuru.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 125) (3292). صحيح مسلم (4/ 1771) (2261). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (11/ 190). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 125). بهجة قلوب الأبرار، لعبد الرحمن آل سعدي (ص149). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 170). منار القاري، لحمزة محمد قاسم (1/ 44). المنهاج شرح صحيح مسلم، للنووي (15/ 18).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Haijabakia katika utume isipokuwa viashiria vya habari njema

عن أبي هريرة ـ رضي الله عنه ـ قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «لم يبقَ من النُّبُوَّةِ إلا المُبَشِّرَاتُ» قالوا: وما المُبَشِّرَاتُ ؟ قال: «الرؤيا الصالحة».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akisema: "Haijabakia katika utume isipokuwa viashiria vya habari njema" wakasema: ni vipi hivyo viashiria? Akasema: "Ni ndoto njema".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anaashiria Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa ndoto njema ndio viashiria, nazo ndiyo athari za utume zilizobakia baada ya kukatika kwa wahyi, na hayajabakia yanayoweza kutumika kujua mambo yatakayotokea isipokuwa ndoto njema.

Marejeo

- صحيح البخاري، للإمام محمد بن إسماعيل البخاري، تحقيق محمد الناصر، دار طوق النجاة. - بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين؛ تأليف سليم الهلالي، دار ابن الجوزي- الطبعة الأولى 1418ه. - نزهة المتقين شرح رياض الصالحين؛ تأليف د. مصطفى الخِن وغيره، مؤسسة الرسالة-بيروت، الطبعة الرابعة عشر، 1407هـ. - كنوز رياض الصالحين»، لحمد بن ناصر العمار، دار كنوز إشبيليا- الطبعة الأولى1430ه. - دليل الفالحين لطرق رياض الصالحين، لمحمد علي بن محمد بن علان بن إبراهيم البكري الصديقي الشافعي اعتنى بها: خليل مأمون شيحا، دار المعرفة - شرح رياض الصالحين؛ للشيخ محمد بن صالح العثيمين، مدار الوطن، الرياض، 1426هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayeniona mimi ndotoni basi ataniona akiwa macho -au ni kana kwamba kaniona akiwa macho- hajifananishi shetani na mimi

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «من رآني في المنام فَسَيَرَانِي في اليَقظة -أو كأنما رآني في الْيَقَظَةِ- لا يَتَمَثَّلُ الشيطان بي».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayeniona mimi ndotoni basi ataniona akiwa macho -au ni kana kwamba kaniona akiwa macho- hajifananishi shetani na mimi".
Imepokelewa na Imamu Muslim - Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Wametofautiana wanachuoni katika kubainisha maana ya hadithi hii, katika mitazamo mingi: Wa kwanza: Nikuwa makusudio yake: ni wale watu wa zama zake, na maana yake nikuwa atakayemuona usingizini na akawa hakuhama, hajawezeshwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kuhama na kumuona yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiwa macho wazi. Na ya pili: Nikuwa anayeonekana kwake usingizini ndiye Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- halisi, yaani katika ulimwengu wa roho, na kuwa kumuona kwake ni kweli, lakini sharti iwe kwa sifa yake inayojulikana-. Ya tatu: Nikuwa yeye ataona uhakika wa hiyo ndoto akiwa macho akhera; ni kumuona maalumu kwasababu ya kuwa karibu naye na kupata utetezi wake na mfano wa hayo. Kauli yake: "Au ni kana kwamba kaniona akiwa macho" Hii ni riwaya ya Imamu Muslim kaipokea ikiwa na shaka katika mapokezi yake: Je alisema -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Ataniona akiwa macho?" au alisema: "Ni kana kwamba kaniona akiwa macho". Na maana yake: nikuwa atakayemuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika ndoto kwa sifa zake ambazo yeye yuko nazo basi ni kana kwamba kamuona akiwa macho, hii ni kama kauli yake -Rehema na Amani ziwe juu yake-, kama ilivyokuja katika sahihi mbili (yaani kitabu cha sahihi Bukhariy na sahihi Muslim): "Atakayeniona ndotoni, basi atakuwa kaniona" na katika riwaya nyingine ndani ya sahihi mbili pia: "Atakayeniona ndotoni, basi atakuwa kaniona mimi kweli". kauli yake: "Hajifananishi shetani na mimi", na katika tamko jingine: "Atakayeniota mimi usingizini atakuwa kaniona mimi, kwani hakika haimpasi shetani kujifananisha kwa sura yangu". Na maana yake: nikuwa shetani haiwezekani kwake kujifananisha na Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika umbile lake halisia, na vinginevyo anaweza kuja shetani na akasema kuwa yeye ndiye Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na anakuwa katika umbile ambalo si umbile lake -Rehema na Amani ziwe juu yake-, huyu si Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- mtu atakapomuota mtu ndotoni na ikaingia hisia nafsini mwake kuwa huyu ndiye Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake-, basi hebu atafute sifa za huyu aliyemuona, je zinaendana na sifa za Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake au la? Ikiwa zitaendana: Basi atakuwa kamuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Na zisipoendana basi huyo si Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- bali hizi ni dhana toka kwa shetani kaziingiza katika nafsi ya huyu aliyelala kwamba ndiye Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na wala si yeye Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, Na amepokea Imamu Ahmadi na Tirmidhiy katika shamaail: kutoka kwa Yazidi Al faarisiy amesema: Nilimuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ndotoni, nikasema kumwambia bin Abbas: Hakika mimi nimemuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ndotoni, akasema bin Abbasi: hakika Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa akisema: "Hakika shetani hawezi kujifananisha na mimi, basi atakayeniona mimi usingizini hakika atakuwa kaniona mimi", Je unaweza kueleza sifa za huyo bwana uliyemuota? Nikasema: Ndiyo: alipoeleza sifa zake, akasema bin Abbas: lau kama ungemuona ukiwa macho usingeweza kumsifia juu ya hapo" Na maana yake: nikuwa lau kama ungemuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ukiwa macho isingewezekana kumsifia zaidi ya hayo uliyomsifia, na hii maana yake nikuwa yeye alimuona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake kweli.

Marejeo

كنوز رياض الصالحين، تأليف: حمد بن ناصر العمار، الناشر: دار كنوز أشبيليا، الطبعة الأولى: 1430هـ. بهجة الناظرين، تأليف: سليم بن عيد الهلالي، نسخة الكترونية، لا يوجد بها بيانات نشر. صحيح البخاري، تأليف: محمد بن إسماعيل البخاري، تحقيق: محمد زهير الناصر، الناشر: دار طوق النجاة، الطبعة الأولى، 1422هـ. صحيح مسلم، تأليف: مسلم بن الحجاج النيسابوري، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي الناشر: دار إحياء التراث العربي – بيروت. شرح رياض الصالحين، تأليف: محمد بن صالح العثيمين، الناشر: دار الوطن للنشر، الطبعة: 1426هـ. رياض الصالحين، تأليف: محيي الدين يحيى بن شرف النووي، تحقيق: د. ماهر بن ياسين الفحل، الطبعة الأولى، 1428هـ. التنوير شرح الجامع الصغير، تأليف: محمد بن إسماعيل الصنعاني، تحقيق: د. محمد إسحاق محمد إبراهيم، الناشر: مكتبة دار السلام، الطبعة الأولى، 1432هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com