Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Adabu za usomaji wa Qur'ani.

Hadithi 3

Hakika mfano wa mtu wa Qur'ani ni sawa na mfano wa mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa, akimuangalia kila mara atamzuia (kutoroka), na akimuachilia atatoroka

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّمَا مَثَلُ صَاحِبِ القُرْآنِ كَمَثَلِ صَاحِبِ الإِبِلِ المُعَقَّلَةِ، إِنْ عَاهَدَ عَلَيْهَا أَمْسَكَهَا، وَإِنْ أَطْلَقَهَا ذَهَبَتْ».
Imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema: "Hakika mfano wa mtu wa Qur'ani ni sawa na mfano wa mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa, akimuangalia kila mara atamzuia (kutoroka), na akimuachilia atatoroka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amemfananisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliyesoma Qur'ani na akakizoea kisomo chake sawa iwe kwa kutazama katika msahafu au kuhifadhi kwa moyo, na mmiliki wa ngamia aliyeachwa pasina kufungwa kwa kamba ambazo hufungiwa wanyama, akimtazama mara kwa mara ataendelea kumshika na kumzuia, na akiacha kumfunga na kumtazama basi ataondoka na kutoroka, akianza kusoma Qur'ani msomaji wa Qur'ani basi huikumbuka, na asipoisoma basi ataisahau; madam kudumu kuisoma kutaendelea basi hifdhi yake itaendelea kubakia.

Mafunzo
  1. Himizo la kushikamana na Qur'ani na kuisoma, na tahadhari ya kutumbukia katika kuisahau.
  2. Kudumu kuisoma Qur'ani huudhalilisha ulimi na huurahisishia kuisoma kwake, akiihama inakuwa nzito kwake na inampa tabu.
  3. Amesema Kadhi: Na maana ya "Mwenye Qur'ani" Yaani: Aliyeizoea, na kusuhubiana: Ni kuzoea, na hukusudiwa: Fulani ni jamaa wa fulani, na watu wa peponi na watu wa motoni.
  4. Miongoni mwa njia za ufundishaji ni kupiga mifano.
  5. Amesema bin Hajari: Na amemtaja ngamia pekee; kwa sababu ndio mnyama pekee anayetoroka haraka zaidi katika wanyama wafugwao na binadamu, na kumkamata kwake baada ya kutoroka ni kazi ngumu sana.
Marejeo

صحيح البخاري (6/ 193) (5031). صحيح مسلم (1/ 543) (789). شرح صحيح مسلم، للنووي (6/ 77). فيض القدير شرح الجامع الصغير، لعبدالرؤوف المناوي (3/ 3). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (13/ 12).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mwenye kuisoma Qur'ani kwa sauti ya wazi ni kama mwenye kutoa sadaka hadharani, na mwenye kuisoma Qur'ani kwa siri ni kama mwenye kuficha sadaka

عن عُقبة بن عامر الجُهني رضي الله عنه قال: قال رسولُ الله صلَّى الله عليه وسلم: «الجاهِرُ بالقرآن كالجاهِرِ بالصَّدَقَةِ، والمُسِرُّ بالقرآن كالمُسِرِّ بالصَّدَقَة».
Imepokelewa kutoka kwa Uqbah Bin Aamir Al-juhaniy-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake: "Mwenye kuisoma Qur'ani kwa sauti ya wazi ni kama mwenye kutoa sadaka hadharani, na mwenye kuisoma Qur'ani kwa siri ni kama mwenye kuficha sadaka."
Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na NasaaiDarajaSahihi
Maelezo

Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kuweka wazi kusoma Qur'ani ni sawa na mwenye kuweka wazi anapotoa sadaka, na mwenye kuficha kisomo cha Qur'ani ni sawa na mwenye kuificha sadaka.

Mafunzo
  1. Kuficha usomaji wa Qur'ani ni bora, kama ilivyo kuficha sadaka ni bora zaidi, kwa kuwa kufanya hivyo ni katika utakasifu wa nia na kujiweka mbali na kujionesha na kujisikia, isipokuwa itakapohitajika, na maslahi ya kuisoma kwa wazi ni katika kuifundisha.
Marejeo

سنن أبي داود (2/ 494) (1333)، سنن الترمذي (5/ 40) (2919)، سنن النسائي (5/ 80) (2561)، الكاشف عن حقائق السُّنن (5/1688)، شرح أبي داود للعيني (5/238)، تحفة الأحوذي (8/ 191)، التنوير في شرح الجامع الصغير (5/286).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Tambueni kuwa kila mmoja kati yenu ananong'ona na Mola wake, msiudhiane baadhi yenu kwa baadhi

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: اعْتَكَفَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي المَسْجِدِ، فَسَمِعَهُمْ يَجْهَرُونَ بِالقِرَاءَةِ، فَكَشَفَ السِّتْرَ، فَقَالَ: «أَلَا إِنَّ كُلَّكُمْ مُنَاجٍ رَبَّهُ، فَلَا يُؤْذِيَنَّ بَعْضُكُمْ بَعْضًا، وَلَا يَرْفَعْ بَعْضُكُمْ عَلَى بَعْضٍ فِي القِرَاءَةِ»، أَوْ قَالَ: «فِي الصَّلَاةِ».
Kutoka kwa Abuu Saidi -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikaa itikafu Mtume rehema na amani ziwe juu yake msikitini, akawasikia wakidhihirisha kisomo, akafunua pazia, akasema: "Tambueni kuwa kila mmoja kati yenu ananong'ona na Mola wake, msiudhiane baadhi yenu kwa baadhi, na wasinyanyue sauti baadhi yenu kwa wenzao katika kisomo", au alisema: "Katika swala".
Imepokelewa na Abu DaudDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekaa itikafu katika kuba (hema) ndani ya msikiti wake kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, akasikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake wakidhihirisha kisomo chao cha Qur'ani kwa sauti kubwa inayowaudhi baadhi yao. Akafunua pazia la hema, na akamlaumu aliyefanya hivyo na hakupendezwa, na akasema: Nyinyi wote mnazungumza na Mola wenu kwa kusoma kwenu Qur'ani, basi mmoja wenu asimuudhi mwenzake kwa sauti yake katika kusoma kwake, au ndani ya swala yake.

Mafunzo
  1. Katazo la kunyanyua sauti kwa kusoma Qur'ani, ikiwa inamuudhi mtu.
  2. Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwafundisha Maswahaba zake adabu za kusoma Qur'ani.
Marejeo

سنن أبي داود (2/ 494) (1332). شرح سنن أبي داود للعباد (162/ 18). شرح أبي داود للعيني (5/238). شرح سنن ابي داود لابن رسلان (6/515). ذخيرة العقبى (11/669).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com