Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Adabu za mjuzi na mwenye kujifunza.

Hadithi 4

Nijulishe juu ya amali ambayo nikiifanya nitaingia peponi. Akasema: "Umuabudu Mwenyezi Mungu na wala usimshirikishe na chochote, na usimamishe swala na utoe zaka ya wajibu, na ufunge mwezi wa ramadhani

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: أَنَّ أَعْرَابِيًّا أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ دَخَلْتُ الجَنَّةَ، قَالَ: «تَعْبُدُ اللَّهَ لاَ تُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا، وَتُقِيمُ الصَّلاَةَ المَكْتُوبَةَ، وَتُؤَدِّي الزَّكَاةَ المَفْرُوضَةَ، وَتَصُومُ رَمَضَانَ» قَالَ: وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لاَ أَزِيدُ عَلَى هَذَا، فَلَمَّا وَلَّى قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ سَرَّهُ أَنْ يَنْظُرَ إِلَى رَجُلٍ مِنْ أَهْلِ الجَنَّةِ، فَلْيَنْظُرْ إِلَى هَذَا».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba mtu wa kijijini alimjia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akasema: Nijulishe juu ya amali ambayo nikiifanya nitaingia peponi. Akasema: "Umuabudu Mwenyezi Mungu na wala usimshirikishe na chochote, na usimamishe swala na utoe zaka ya wajibu, na ufunge mwezi wa ramadhani" Akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, sitozidisha zaidi ya hapo, basi alipoondoka, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayependezwa na kumtazama mtu miongoni mwa watu wa peponi basi na amtazame huyu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikuja mtu mmoja miongoni mwa watu wa vijijini kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili amjulishe kuhusu amali itakayomuingiza peponi, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamjibu kuwa kuingia peponi na kuokoka na moto yote haya yanasimama katika nguzo za Uislamu, kuanzia kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na usimshirikishe na kitu chochote katika ibada. Na usimamishe swala tano alizoziwajibisha Mwenyezi Mungu kwa waja wake katika kila usiku na mchana. Na utoe zaka ya mali aliyoiwajibisha Mwenyezi Mungu juu yako, na uitoe kuwapa wastahiki wake. Na uhifadhi na kudumu nayo swaumu ya ramadhani katika wakati wake. Yule bwana akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, sitozidisha chochote zaidi ya amali hizo za faradhi nilizozisikia toka kwako katika ibada, na wala sitopunza chochote katika hizo. Alipoondoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Yeyote atakayependezwa na kumuangalia mtu miongoni mwa watu wa peponi basi na amtazame bedui (Mtu wa kijijini) huyu.

Mafunzo
  1. Kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa ibada ndio jambo la kwanza ambalo huanzwa nalo katika kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu.
  2. Kutosheka na mafunzo ya wajibu pekee kwa mgeni katika Uislamu.
  3. Kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu lazima kuanza ngazi kwa ngazi.
  4. Pupa ya mtu kujifunza swala la dini yake.
  5. Muislamu akitosheka na ibada za wajibu pekee basi atafaulu, lakini hii haimaanishi kufanya uzembe katika ibada; kwa sababu sunna hukamilisha mapungufu ya faradhi.
  6. Kuzitaja baadhi ya ibada pasina zingine, ni dalili ya umuhimu wake na himizo juu ya ibada hizo, na haimaanishi kuwa hakuna zingine zaidi yake.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 105) (1397). صحيح مسلم (1/ 44) (14). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (15/ 588). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 349). نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 861). منار القاري، لحمزة قاسم (3/ 5). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (1/ 82).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema?

عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لَيْلَى قَالَ: لَقِيَنِي كَعْبُ بْنُ عُجْرَةَ، فَقَالَ: أَلاَ أُهْدِي لَكَ هَدِيَّةً؟ إِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَرَجَ عَلَيْنَا، فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَدْ عَلِمْنَا كَيْفَ نُسَلِّمُ عَلَيْكَ، فَكَيْفَ نُصَلِّي عَلَيْكَ؟ قَالَ: «فَقُولُوا: اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ، كَمَا صَلَّيْتَ عَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ، إِنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ، اللَّهُمَّ بَارِكْ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ، كَمَا بَارَكْتَ عَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ، إِنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ».
Kutoka kwa Abdul Rahman Bin Abii Laila amesema: Alikutana nami Ka'bu bin Ujza, akasema: Hivi wataka nikupe zaidi? Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema? Akasema: "Basi semeni: Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammadi na juu ya watu wa Muhammadi, kama ulivyompa rehema Ibrahim na juu ya watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa, ewe Mwenyezi Mungu shusha baraka juu ya Muhammad na juu ya watu wa Muhammad, kama ulivyoteremsha baraka kwa watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Masahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu namna ya kumtakia rehema? baada ya kujua kwao namna kumuombea amani (salam) katika kikao cha tahiyatu ndani ya swala: "Amani iwe juu yako ewe Nabii na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake...?" Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akawaeleza namna ya kumtakia rehema, na maana yake: "Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammad na juu ya watu wa Muhammad" Yaani: Mtaje kwa sifa nzuri kwa Malaika walioko juu mbinguni, na juu ya wafuasi wake katika dini yake, na waumini katika ndugu zake wa karibu. "Kama ulivyoteremsha rehema juu ya watu wa Ibrahim" Kama ulivyotoa takrima juu ya watu wa Ibrahim amani iwe juu yake, nao ni Ibrahim na Ismail na Is'haka na kizazi chake na wafuasi wao miongoni mwa waumini, basi zipeleke fadhila zako kwa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake. "Hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa". Yaani: Mwenye kuhimidiwa katika dhati yako na sifa zako na vitendo vyako, mpana katika utukufu wako na ugawaji riziki wako. "Ewe Mwenyezi Mungu teremsha baraka kwa Muhammad na juu ya watu wa Muhammad kama ulivyoteremsha baraka juu ya watu wa Ibrahim" Yaani: Mpe katika kheri na karama zile zilizo kubwa zaidi na uzizidishe na umdumishie kheri hizo.

Mafunzo
  1. Wema waliotangulia walikuwa wakizawadiana kuhusu mambo ya elimu.
  2. Uwajibu wa kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika tashahudi ya mwisho katika swala.
  3. Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwafundisha Masahaba wake kumtakia amani na rehema juu yake.
  4. Namna hii ya kuomba ndio namna sahihi zaidi katika kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 77) (6357). صحيح مسلم (1/ 305) (406). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص208). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 270). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 170).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayejifunza elimu katika yale yanayo ambayo hutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hajifunzi isipokuwa kwa ajili ya kupata masilahi ya kidunia, basi hatoipata harufu ya Pepo siku ya Kiyama

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ تَعَلَّمَ عِلْمًا مِمَّا يُبْتَغَى بِهِ وَجْهُ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ لَا يَتَعَلَّمُهُ إِلَّا لِيُصِيبَ بِهِ عَرَضًا مِنَ الدُّنْيَا لَمْ يَجِدْ عَرْفَ الْجَنَّةِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ» يَعْنِي رِيحَهَا.
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayejifunza elimu katika yale yanayo ambayo hutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hajifunzi isipokuwa kwa ajili ya kupata masilahi ya kidunia, basi hatoipata harufu ya Pepo siku ya Kiyama" Yaani: Upepo yake.
Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba atakayejifunza elimu ya kisheria ambayo asili yake ni kutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hajifunzi isipokuwa apate heshima na starehe za kidunia miongoni mwa mali au cheo, basi hatoipata harufu ya Pepo siku ya Kiyama.

Mafunzo
  1. Uwajibu wa kutakasa nia katika kutafuta elimu, na himizo juu ya hilo.
  2. Tahadhari kubwa ya kuichukua elimu ya kisheria kwa kujionyesha au daraja la kuifikia dunia, na kwamba hilo ni katika madhambi makubwa.
  3. Nikuwa atakayeitafuta elimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na ikamuijia dunia yenyewe inafaa kwake kuichukua, na hilo halitomdhuru.
  4. Amesema Assanadi: Kauli yake: "Harufu ya Pepo" Neno harufu limetumika likiashiria kupita kiasi katika kuharamishwa Pepo; kwa sababu asiyeweza kupata harufu ya kitu hawezi kukipata.
  5. Atakayejifunza elimu katika yale ambayo hutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu kwayo, kwa ajili ya kupata ajira, au kwa ajili ya malengo mengine; basi anatakiwa kutubia kwa Mwenyezi Mungu kutokana na hilo, na Mwenyezi Mungu atamfutia yaliyojitokeza miongoni mwa nia mbaya, kwani Yeye anafadhila kubwa Aliyetakasika na kutukuka.
  6. Tahadhari hii ni kwa mwenye kutafuta elimu ya kisheria, ama atakayetafuta elimu yoyote katika elimu za kidunia kwa ajili ya starehe za dunia, kama uhandisi, na kemia, na mengineyo kwa ajili ya masilahi ya dunia, hakuna shaka atalipwa kwa nia yake.
Marejeo

سنن أبي داود (5/ 504) (3664). سنن ابن ماجه (1/ 169) (252). مسند أحمد (14/ 169) (8457). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 477). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (16/ 507). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 957). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 447). عون المعبود شرح سنن أبي داود، العظيم آبادي (10/ 70). حاشية السندي على سنن ابن ماجه، لمحمد التتوي (1/ 110).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Allah amng'arishe mtu aliyesikia kutoka kwangu chochote akakifikisha kama alivyo sikia, huenda mfikishiwa akawa mwerevu zaidi kuliko aliye sikia

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «نَضَّرَ اللَّهُ امْرَأً سَمِعَ مِنَّا شَيْئًا فَبَلَّغَهُ كَمَا سَمِعَ، فَرُبَّ مُبَلِّغٍ أَوْعَى مِنْ سَامِعٍ».
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Allah amng'arishe mtu aliyesikia kutoka kwangu chochote akakifikisha kama alivyo sikia, huenda mfikishiwa akawa mwerevu zaidi kuliko aliye sikia".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Aliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kung'arisha na muonekano na uzuri katika dunia, na amfikishe Mwenyezi Mungu katika mng'ao wa peponi na neema zake na mng'ao wake katika Akhera; kwa yule atakayesikia hadithi yake akaihifadhi ili amfikishie mwingine, huenda aliyenukuliwa hadithi akawa mwerevu na muelewa na akawa na uwezo wa kuchambua hukumu kuliko hata aliyeinukuu hadithi, akawa wa kwanza anahifadhi vizuri, na wa pili akawa anauelewa na uchambuzi mzuri.

Mafunzo
  1. Himizo la kuhifadhi mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kuyafikisha kwa watu.
  2. Kumebainishwa fadhila za watu wa hadithi, na heshima ya kuitafuta kwake.
  3. Fadhila ya wanachuoni, ambao wanastahiki kuchambua na kuzielewa hadithi.
  4. Ubora wa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, wao ndio waliosikia hadithi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wakatufikishia.
  5. Amesema Al-Munaawi: Amebainisha kuwa mpokezi wa hadithi kuwa na uelewa si katika sharti zake, bali sharti lake ni kuhifadhi, na kwa msomi kuelewa na kuzingatia.
  6. Amesema bin Uyaina: Hakuna yeyote anayetafuta hadithi isipokuwa kuna mng'ao katika uso wake kwa hadithi hii.
  7. Kuhifadhi kwa wasomi wa hadithi kuna aina mbili: Kuhifadhi kwa moyo na kifua, na kuhifadhi kwa kitabu na mwandiko, na aina zote mbili zinakusanywa na dua iliyoko katika hadithi.
  8. Ufahamu wa watu unatofautiana, huenda mfikishiwa akawa muelewa zaidi kuliko aliyesikia, na huenda aliyebeba maarifa ya sheria akawa si muelewa.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 394) (2657). سنن ابن ماجه (1/ 157) (232). مسند أحمد (7/ 221) (4157). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 476). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 446). فيض القدير شرح الجامع الصغير، لعبدالرؤوف المناوي (3/ 206). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (16/ 496). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 956).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com