عن عمران بن حصين رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رسولُ اللَّه -صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم-: «الحَيَاءُ لاَ يَأْتِي إِلاَّ بِخَيرٍ».
وفي رواية : «الحَيَاءُ خَيرٌ كُلُّهٌ» أو قال: «الحَيَاءُ كُلُّهُ خَيرٌ».
Kutoka kwa Imrani bin Huswain -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Haya (Aibu) haiji ila kwa kheri". na katika riwaya nyingine: "Haya ni kheri yote" Au alisema: "Haya yote ni kheri".
Imepokelewa na Imamu Muslim - Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Haya(Aibu) ni sifa iliyoko katika nafsi inayomsukuma mtu kufanya mazuri au yanayopendeza, na kuacha yanayochafua na kuharibu, na ndio maana haiji isipokuwa kwa kheri, na sababu ya kuja kwa hadithi hii nikuwa mtu mmoja alikuwa akimnasihi ndugu yake kuhusu haya, na akimkataza kuhusu haya, Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akasema kumwambia maneno haya.
Marejeo
رياض الصالحين للنووي، ط1، تحقيق: ماهر ياسين الفحل، دار ابن كثير، دمشق، بيروت، 1428هـ.
شرح رياض الصالحين للشيخ ابن عثيمين، دار الوطن للنشر، الرياض، 1426هـ.
صحيح البخاري، ط1، تحقيق: محمد زهير بن ناصر الناصر دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم: محمد فؤاد عبد الباقي)، 1422هـ.
صحيح مسلم، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي، بيروت.
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين لمجموعة من الباحثين، ط14، مؤسسة الرسالة، 1407هـ.
عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسعودٍ رضي الله عنه عن رَسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال: «الطِّيَرَةُ شِرْكٌ، الطِّيَرَةُ شِرْكٌ، الطِّيَرَةُ شِرْكٌ، -ثلاثًا-»، وَمَا مِنَّا إِلَّا، وَلَكِنَّ اللهَ عَزَّ وَجَلَّ يُذْهِبُهُ بِالتَّوَكُّلِ.
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, alisema hivyo mara tatu", Na hakuna yeyote miongoni mwetu isipokuwa ana chembe ya hilo, isipokuwa Mwenyezi Mungu huliondoa kwa kumtegemea.
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Ametahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokana na imani ya mikosi: Nayo ni kuamini mikosi ya chochote chenye kusikika au chenye kuonekana, kama ndege au wanyama au walemavu au namba au siku au kinginecho, Na bila shaka ametaja ndege kwa sababu ndio ilikuwa maarufu kipindi cha zama za ujinga, na asili yake ni kumuachia ndege aruke katika jambo kama safari au biashara au kinginecho, akiruka pande wa kulia anajipa bishara na anatekeleza anachotaka kukifanya, na akirukia upande wa kushoto, anaamini ni mkosi na anaacha kufanya alichotaka kukifanya. Na akaeleza kuwa kitendo hicho ni ushirikina, na mikosi imekuwa ni ushirikina kwa sababu hakuna aletaye kheri ila Mwenyezi Mungu, na wala hazuii shari ila Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika.
Na ametaja bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake kuwa inaweza kuingia katika moyo wa muislamu kiasi kidogo cha imani ya mkosi, lakini anatakiwa akizuie kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, ikiwa ni pamoja na kufanya sababu.
Mafunzo
Mikosi ni ushirikina; kwa sababu ndani yake kuna kuufungamanisha moyo kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
Umuhimu wa kurudia mambo muhimu, ili yahifadhike na yakite ndani ya moyo.
Mikosi huondolewa kwa kutegemea kwa Allah Mtukufu.
Amri ya kutegemea kwa Allah pekee na moyo kufungamana naye Mtukufu.
Marejeo
سنن أبي داود (6/ 54) (3915).
سنن ابن ماجه (4/ 560) (3538).
سنن الترمذي (3/ 258) (1614).
مسند أحمد (6/ 213) (3687).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص259).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص233).
Imepokewa Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Nuuman akashusha vidole vyake masikioni mwake-" "Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi na kati ya halali na haramu kuna mambo yenye kutatiza, hawayajui mambo hayo wengi miongoni mwa watu, atakaye yaepuka mambo yenye kutatiza, basi atakuwa kaihifadhi dini yake na heshima yake, na atakayeingia katika mambo yenye kutatiza atakuwa kaingia katika haramu, ni kama mfano wa mchunga mifugo mwenye kuchungia kando kando ya mipaka wanahofiwa (mifugo wake) kuingia humo, tambueni na hakika kila Mfalme ana mipaka yake, na tambueni kuwa mipaka ya Mwenyezi Mungu ni makatazo yake, na tambueni kuwa katika mwili kuna kipande cha nyama, kikitengemaa mwili mzima unatengemaa, na kikiharibika, mwili mzima unaharibika, tambueni kipande hicho ni moyo."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kanuni kuu katika mambo, nakuwa zinagawanyika sehemu tatu katika sheria: Halali ya wazi, na haramu ya wazi, na mambo yenye kutatiza, hukumu yake haiko wazi upande wa uhalali na uharamu, watu wengi hawajui hukumu yake.
Atakayeacha mambo hayo yenye kutatiza kwake, dini yake itasalimika kwa kuwa mbali na kuingia katika haramu, na heshima yake itasalimika kutokana na maneno ya watu, kwa yale wanayoweza kumuaibisha kwa kuyafanya kwake haya yenye kutatiza. Na asiyeyaepuka yenye kutatiza atakuwa kaitumbukiza nafsi yake, ima katika haramu, au watu kumkosea heshima yake. Na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kapiga mfano ili abainishe hali ya mwenye kuyafanya mambo yenye kutatiza, nakuwa yeye ni sawa na mchunga mifugo, mwenye kuchunga karibu na ardhi ambayo kaihifadhi mwenye ardhi hiyo, inahofiwa mifugo yake kulisha katika mipaka hii kwa sababu ya ukaribu wake, na hivyo hivyo mwenye kufanya mambo yenye utata ndani yake, basi kwa kufanya hivyo anakuwa karibu na haramu na anahofiwa kutumbukia ndani yake. Na baada yake akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama (Nacho ni moyo) mwili hutengemaa kwa kutengemaa kwake, na huharibika kwa kuharibika kwake.
Mafunzo
Himizo la kuacha yenye kutatiza, ambayo hukumu yake haijabainika.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 20) (52).
صحيح مسلم (3/ 1219) (1599).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثا النووية (ص18).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص105).
فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص41).
فتح الباري لابن حجر (4/ 291).
شرح النووي على مسلم (11/ 28).
عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قال: إنه سمع نبي الله صلى الله عليه وسلم يقول: «لَو أَنَّكُمْ تَتَوَكَّلُونَ عَلَى اللهِ حَقَّ تَوَكُّلِهِ، لَرَزَقَكُمْ كَمَا يَرْزُقُ الطَّيْرَ، تَغْدُو خِمَاصًا وَتَرُوحُ بِطَانًا».
imepokewa Kutoka kwa Omari bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Hakika yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Lau kama nyinyi mngelimtegemea Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni kama anavyomruzuku ndege, anatoka asubuhi akiwa na njaa anarudi mchana akiwa kashiba".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Anatuhimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuleta manufaa na kuzuia madhara katika mambo ya Dunia na Akhera, kwani hakuna yeyote mwenye kutoa wala kunyima wala kudhuru wala kunufaisha isipokuwa Yeye Aliyetakasika na Kutukuka, Na tufanye sababu zinazoleta manufaa na kuzuia madhara, pamoja na kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa dhati, wakati wowote tutakapofanya hivyo, Mwenyezi Mungu ataturuzuku kama anavyowaruzuku ndege wanaotoka asubuhi wakiwa na njaa, kisha wanarudi jioni matumbo yakiwa yamejaa, na kitendo hiki kwa ndege ni aina ya kufanya sababu za kutafuta riziki, bila kubweteka wala uvivu.
Mafunzo
Ubora wa kumtegemea Mwenyezi Mungu, nakuwa ni katika sababu kubwa ambazo huvuta riziki.
Kumtegemea Mwenyezi Mungu hakupingani na kufanya sababu, kwani kaeleza kuwa kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa uhakika hakupingani na kutoka asubuhi na kurudi jioni katika kutafuta riziki.
Sheria kutilia umuhimu matendo ya moyo; kwa sababu kutegemea ni katika matendo ya moyo.
Kutegemea sababu pekee ni mapungufu katika dini, na kuacha kufanya sababu ni mapungufu ya akili.
Marejeo
سنن الترمذي (4/ 166) (2344).
سنن ابن ماجه (5/ 266) (4164).
مسند أحمد (1/ 332) (205).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية (ص103).
فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص152).
الأحاديث الأربعون النووية وعليها الشرح الموجز المفيد، لعبد الله المحسن (ص91).
Imepokelewa kutoka kwa Khuraimu Bin Faatik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Matendo yapo ya aina sita na watu wapo wako aina nne, basi kuna watu wa aina mbili wanaostahiki malipo, na malipo yao huwa sawa na matendo yao, na jema moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na jema moja huzidishwa mpaka kufikia mema mia saba, Basi wawili wenye kustahiki malipo ni: Yeyote atakaye kufa hali yakuwa hajamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia Peponi, na atakaye kufa hali ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote basi ataingia Motoni, na ama yule ambaye atalipwa kwa namna alivyokusudia ni yeyote atakaye kusudia kufanya jambo jema mpaka moyo wake ukahisi kuwa umetenda na Mwenyezi Mungu akajua kutenda kwake huko basi mtu huyo ataandikiwa jema moja, na atakaye fanya kosa ataandikiwa kosa moja, na atakaye fanya jema moja basi hulipwa kwa kumi mfano wake, na mwenye kutoa chochote katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi atalipwa kwa kila kimoja kwa mara mia saba, ama watu walivyogawanyika kuna miongoni mwao waliokunjuliwa mambo yao hapa Duniani na wakawa na maisha duni huko Akhera, na kuna wenye maisha Duni hapa duniani na wakakunjuliwa maisha yao huko Akhera, na kuna wenye maisha duni hapa duniani na pia Akhera, na wakakunjuliwa maisha yao hapa duniani na kesho Akhera."
Imepokelewa na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Alieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa matendo yapo aina sita, na watu wamegawanyika katika makundi manne, nayo ni:
Kundi la kwanza: Yeyote atakaye kufa na hakumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote anastahiki kuingia peponi.
Kundi la pili: Yeyote atakaye kufa hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu kingine anastahiki kuingia motoni na atakaa humo milele.
Na matendo hayo mawili ndiyo haki mbili za msingi.
Kundi la tatu: Kukusudia kufanya wema, basi yeyote atakaye kusudia kufanya jema na akawa mkweli katika makusudio yake mpaka akahisi kweye moyo wake kuwa hili ndilo kusudio langu, kisha likamtokea jambo la kumzuia asifanye alichokikusudia katika wema huu, basi huandikiwa thawabu za wema kamili.
Kundi la nne: Kufanya tendo baya; Yeyote atakaye fanya tendo baya basi huandikiwa kosa moja.
Na matendo hayo mawili: Ndiyo hulipwa sawa sawa bila ya kuzidisha.
Kundi la Tano: Jema moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na malipo hayo ni kwa mwenye kukusudia kufanya wema na akaufanya wema huo, basi huandikiwa mema kumi.
kundi la sita: Jema moja hulipwa sawa na mema mia saba, na malipo hayo ni kwa mwenye kutoa kitu kimoja katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hulipwa kwa kitu hiki kimoja kwa mema mia saba, na haya ni kutokana na fadhila za Mwenyezi Mungu aliyetakasika na Kutukuka, na ukarimu wake kwa waja wake.
Ama aina Nne ya watu ni hawa:
Aina ya kwanza: Ni mtu ambaye amekunjuliwa mambo yake hapa Duniani kwa upande wa riziki, ananeemeka humo na hupata akitakacho, lakini ni mwenye dhiki na tabu kubwa Akhera na mwisho wake ni kuingia motoni, na huyo ni tajiri wa kikafiri.
Aina ya pili: Ni mtu mwenye dhiki hapa Duniani upande wa riziki, lakini amekunjuliwa huko Akhera, na mwisho wake ni kuingia Motoni, na huyo ni muumini fakiri.
Aina ya tatu: Ni mtu mwenye dhiki hapa Duniani na Akhera, naye ni kafiri fukara.
Aina ya nne: Ni mtu aliyekunjuliwa mambo yake hapa Duniani na Akhera, naye ni muumini tajiri.
Mafunzo
Ukubwa wa fadhila za Mwenyezi Mungu kwa waja wake na kuwazidishia mambo mema.
Uadilifu wa Mwenyezi Mungu na ukarimu wake, pale alipo amiliana nasi kwenye makosa kwa uadilifu, hivyo basi akafanya malipo ya kosa moja ni moja hivyo hivyo.
Ukubwa wa dhambi ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu, katika hilo kunapelekea kuharamishiwa kuingia peponi.
Kumewekwa wazi utukufu na ubora wa kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Ongozeko la thawabu za kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, linaanzia ziada ya mia saba; Kwa sababu kutoa kunasaidia kuliinua neno la Mwenyezi Mungu.
Kumewekwa wazi aina za watu na tofauti zao.
Mwenyezi Mungu humkunjulia muumini na asiyekuwa mumini hapa Duniani, na wala hamkunjulii Akhera isipokuwa muumini tu.
Marejeo
مسند أحمد (31/ 196) (18900)، (31/ 384)، الفتح الرباني لترتيب مسند أحمد بن حنبل الشيباني (19/198).
عن عُقبة بن عامر الجُهني رضي الله عنه قال: قال رسولُ الله صلَّى الله عليه وسلم: «الجاهِرُ بالقرآن كالجاهِرِ بالصَّدَقَةِ، والمُسِرُّ بالقرآن كالمُسِرِّ بالصَّدَقَة».
Imepokelewa kutoka kwa Uqbah Bin Aamir Al-juhaniy-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake: "Mwenye kuisoma Qur'ani kwa sauti ya wazi ni kama mwenye kutoa sadaka hadharani, na mwenye kuisoma Qur'ani kwa siri ni kama mwenye kuficha sadaka."
Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na NasaaiDarajaSahihi
Maelezo
Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kuweka wazi kusoma Qur'ani ni sawa na mwenye kuweka wazi anapotoa sadaka, na mwenye kuficha kisomo cha Qur'ani ni sawa na mwenye kuificha sadaka.
Mafunzo
Kuficha usomaji wa Qur'ani ni bora, kama ilivyo kuficha sadaka ni bora zaidi, kwa kuwa kufanya hivyo ni katika utakasifu wa nia na kujiweka mbali na kujionesha na kujisikia, isipokuwa itakapohitajika, na maslahi ya kuisoma kwa wazi ni katika kuifundisha.
Marejeo
سنن أبي داود (2/ 494) (1333)، سنن الترمذي (5/ 40) (2919)، سنن النسائي (5/ 80) (2561)، الكاشف عن حقائق السُّنن (5/1688)، شرح أبي داود للعيني (5/238)، تحفة الأحوذي (8/ 191)، التنوير في شرح الجامع الصغير (5/286).
Kutoka kwa Abuu Umama Al-Bahiliy radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake akasema: Wasemaje kuhusu mtu aliyepigana vita akitaka malipo kwa Allah na kusemwa vizuri na watu, ana lipi? Akasema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Hana malipo yoyote" Akalirudia hilo mara tatu, akimwambia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Hana malipo yoyote" Kisha akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu hakubali amali yoyote isipokuwa ile itakayokuwa imetakasiwa nia, na ikakusudiwa kupata radhi za Allah (na kwenda kuuona uso wake)".
Imepokelewa na An-nasaiyDarajaSahihi
Maelezo
Alikuja mtu kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake kumuuliza na kumuuliza juu ya hukumu ya mtu anayetoka kwa ajili ya vita na jihadi kutafuta malipo kwa Mwenyezi Mungu na kutaka sifa na pongezi kwa watu, je anapokea thawabu? Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, akajibu: Huyo hana malipo yoyote. Alipochanganya kitu kisichokuwa Mwenyezi Mungu katika nia yake, yule bwana akarudia swali lake mara tatu kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake na akamjibu na akathibitisha jibu lile lile kwake kwamba hana malipo, basi Mtume -rehema na amani ziwe juu yake, akampa kanuni ya kukubalika amali kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwamba Mwenyezi Mungu haikubali amali isipokuwa yote iwe ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu bila ya yeyote kuhusishwa nayo, na iwe ni kwa ajili ya kutaka radhi za Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
Mwenyezi Mungu hakubali amali yoyote isipokuwa ile iliyotakaswa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa kulingana na muongozo wa Mtume wake -rehema na amani ziwe juu yake.
Ni kuwa katika uzuri wa majibu ya mtoaji wa Fat'wa yatosheleze swali la muulizaji na zaidi.
Kulitia mkazo jambo kubwa kwa kurudia swali.
Mpiganaji wa kweli ni yule atakayepigana ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu, na kwa kutafuta malipo na thawabu za Akhera pamoja na kutakasa nia, ili kupigana kwake kusiwe ni kwa ajili ya dunia.
Marejeo
سنن النسائي (6/ 25) (3140)، الترغيب والترهيب (2/194)، جامع العلوم والحكم (1/75)، نيل الأوطار (7/245)، ذخيرة العقبى في شرح المجتبى (26/205).
Kutoka kwa Abdallah bin Nu'man bin Bashiri -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi na kati ya halali na haramu kuna mambo yenye kutatiza, hawayajui mambo hayo wengi miongoni mwa watu, atakaye yaepuka mambo yenye kutatiza, basi atakuwa kaihifadhi dini yake na heshima yake, na atakayeingia katika mambo yenye kutatiza atakuwa kaingia katika haramu, ni kama mfano wa mchunga mifugo mwenye kuchungia kando kando ya mipaka wanahofiwa (mifugo wake) kuingia humo, tambueni na hakika kila Mfalme ana mipaka yake, na tambueni kuwa mipaka ya Mwenyezi Mungu ni makatazo yake, na tambueni kuwa katika mwili kuna kipande cha nyama, kikitengemaa mwili mzima unatengemaa, na kikiharibika, mwili mzima unaharibika, tambueni kipande hicho ni moyo."
Imepokelewa na Bukhari na MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kanuni kuu katika mambo, nakuwa zinagawanyika sehemu tatu katika sheria: Halali ya wazi, na haramu ya wazi, na mambo yenye kutatiza, hukumu yake haiko wazi upande wa uhalali na uharamu, watu wengi hawajui hukumu yake.
Atakayeacha mambo hayo yenye kutatiza kwake, dini yake itasalimika kwa kuwa mbali na kuingia katika haramu, na heshima yake itasalimika kutokana na maneno ya watu, kwa yale wanayoweza kumuaibisha kwa kuyafanya kwake haya yenye kutatiza. Na asiyeyaepuka yenye kutatiza atakuwa kaitumbukiza nafsi yake, ima katika haramu, au watu kumkosea heshima yake. Na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kapiga mfano ili abainishe hali ya mwenye kuyafanya mambo yenye kutatiza, nakuwa yeye ni sawa na mchunga mifugo, mwenye kuchunga karibu na ardhi ambayo kaihifadhi mwenye ardhi hiyo, inahofiwa mifugo yake kulisha katika mipaka hii kwa sababu ya ukaribu wake, na hivyo hivyo mwenye kufanya mambo yenye utata ndani yake, basi kwa kufanya hivyo anakuwa karibu na haramu na anahofiwa kutumbukia ndani yake. Na baada yake akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama (Nacho ni moyo) mwili hutengemaa kwa kutengemaa kwake, na huharibika kwa kuharibika kwake.
Mafunzo
Hadithi hii ni kanuni katika kuepuka mambo yenye utata.
Himizo la kuacha yenye kutatiza, ambayo hukumu yake haijabainika.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 20) (52).
صحيح مسلم (3/ 1219) (1599).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثا النووية (ص18).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص105).
فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص41).
فتح الباري لابن حجر (4/ 291).
شرح النووي على مسلم (11/ 28).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com