Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Ubora wa kuunga udugu.

Hadithi 2

Ikiwa kama utakuwa kama ulivyosema, basi ni kana kwamba unawalisha majivu ya moto (dhambi wanazozipata ni kama mtu anayekula majivu ya moto), na bado anaendelea kuwa pamoja nawe msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi yao, madam bado uko katika hali hiyo

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه: أَنَّ رَجُلًا قَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ إِنَّ لِي قَرَابَةً أَصِلُهُمْ وَيَقْطَعُونِي، وَأُحْسِنُ إِلَيْهِمْ وَيُسِيئُونَ إِلَيَّ، وَأَحْلُمُ عَنْهُمْ وَيَجْهَلُونَ عَلَيَّ، فَقَالَ: «لَئِنْ كُنْتَ كَمَا قُلْتَ، فَكَأَنَّمَا تُسِفُّهُمُ الْمَلَّ وَلَا يَزَالُ مَعَكَ مِنَ اللهِ ظَهِيرٌ عَلَيْهِمْ مَا دُمْتَ عَلَى ذَلِكَ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba mtu mmoja alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi nina ndugu wa karibu, ninawaunga lakini wao wananitenga, ninawafanyia wema lakini wao wanatendea ubaya, na ninakuwa mpole kwao lakini wao wananifanyia ujeuri, basi akasema: "Ikiwa kama utakuwa kama ulivyosema, basi ni kana kwamba unawalisha majivu ya moto (dhambi wanazozipata ni kama mtu anayekula majivu ya moto), na bado anaendelea kuwa pamoja nawe msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi yao, madam bado uko katika hali hiyo".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Mtu mmoja alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ana ndugu wa karibu wa ukoo anaamiliana nao kwa wema ila wao wanaamiliana naye kinyume na hivyo; anawaunga na kuwatembelea ila wao wanamtenga, na anawatendea ihisani kwa wema na uadilifu ila wao wanamtendea ubaya kwa ujeuri na ukaidi, na anakuwa mpole kwao na kuwasamehe ila wao wanampuuza kwa kumfanyia mabaya katika kauli na vitendo, je, aendelee kuwaunga udugu pamoja na hayo yote yaliyotajwa? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Ikiwa ni hivyo kama ulivyoeleza basi wewe unawafedhehesha na kuwadharaulisha katika nafsi zao, ni kana kwamba unawalisha majivu ya moto; kwa wingi wa wema wako na kwa ubaya wa matendo yao mbele ya nafsi zao, na bado anaendelea kuwa pamoja nawe msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi yao, na wao waendelee katika kukutendea ubaya.

Mafunzo
  1. Kuukabili ubaya kwa wema ni sehemu ya kumfanya muovu arejee katika haki, kama alivyosema Mtukufu: "Zuia (ubaya) kwa lile lililo jema, punde yule ambaye baina yako na yeye kuna uadui atakuwa kama rafiki mwandani"
  2. Kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu hata kama kutatokea maudhi ni sababu ya kupata msaada wa Mwenyezi Mungu kwa mja muumini.
  3. Kukata udugu ni maumivu na ni adhabu katika dunia, na ni madhambi na hesabu siku ya Kiyama.
  4. Ni wajibu kwa muislamu ataraji malipo katika amali yake njema, na wala yasimkatishe maudhi ya watu na kumtenga kwao kukamuachisha ibada yake nzuri.
  5. Si muunga udugu yule anayelipa wema wa yule aliyemuunga udugu, lakini muunga udugu wa kweli ni yule ambaye ukikatwa udugu wake yeye anauunga.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 1982) (2558). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (9/ 220). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (1/ 698). نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (1/ 539). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 188).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Haingii peponi mkata udugu

عن جُبَير بن مُطْعِم رضي الله عنه أنه سمع النبي صلى الله عليه وسلم يقول: «لَا يَدْخُلُ الْجَنَّةَ قَاطِعُ رَحِمٍ».
Kutoka kwa Jubairi bin Mutwim -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haingii peponi mkata udugu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayewakatia ndugu zake wa karibu zile haki za wajibu kwao, au akawaudhi au kuwafanyia ubaya, basi anastahiki asiingie peponi.

Mafunzo
  1. Kukata udugu ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.
  2. Kuunga udugu kunakuwa kulingana na desturi za watu, na kutatofautiana kulingana na mazingira na zama na jamii pia.
  3. Kuunga udugu kunakuwa kwa kutembeleana, na kwa sadaka, na kuwatendea wema, na kuwatembelea wagonjwa, na kuwaamrisha mema, na kuwakataza maovu, na mengineyo.
  4. Kila ambavyo kukata udugu kunavyozidi kuwa kwa ndugu wa karibu zaidi ndivyo ambavyo madhambi yanavyokuwa makubwa.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 1981) (2556). صحيح البخاري (8/ 5) (5984). شرح النووي على مسلم (16/ 113). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 90). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 277).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com