Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Muunga udugu si mlipa fadhila, bali muunga udugu ni yule ambaye udugu wake ukikatwa anauunga

عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «لَيْسَ الْوَاصِلُ بِالْمُكَافِئِ، وَلَكِنِ الْوَاصِلُ الَّذِي إِذَا قُطِعَتْ رَحِمُهُ وَصَلَهَا».
Imepokelewa Kutoka kwa Abdillah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Muunga udugu si mlipa fadhila, bali muunga udugu ni yule ambaye udugu wake ukikatwa anauunga".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Kuwa mwanadamu kamili katika kuunga udugu na kuwatendea wema ndugu wa karibu si yule mtu mwenye kulipa wema aliotendewa, Bali muunga udugu halisi na kamili katika kuunga udugu ni yule ambaye ukikatwa udugu wake anauunga, hata wakimtendea ubaya; basi yeye huwalipa wema.

Mafunzo
  1. Kuunga udugu kunakozingatiwa kisheria ni kumuunga aliyekukata miongoni mwao, na kumsamehe aliyekudhulumu, na kumpa aliyekunyima, na si kuunga udugu kwa kubadilishana (wakiniunga nitawaunga wakikata nawakata) au kulipa wema uliotendewa.
  2. Kuunga udugu kunakuwa kwa kufikisha kheri kwa kadiri ya uwezo, kwa kutumia mali na dua na kuamrishana mema na kukatazana maovu na mfano wake, na kuzuia yawezekanayo katika shari juu yao.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 6) (5991). منار القاري شرح مختصر صحيح البخاري، لحمزة محمد قاسم (5/ 242). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (1/ 397). نزهة المتقين، لمصطفى الخن وغيره (1/ 311). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 190).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Jamii ya Kiislamu

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com