عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «لَيْسَ الْوَاصِلُ بِالْمُكَافِئِ، وَلَكِنِ الْوَاصِلُ الَّذِي إِذَا قُطِعَتْ رَحِمُهُ وَصَلَهَا».
Imepokelewa Kutoka kwa Abdillah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Muunga udugu si mlipa fadhila, bali muunga udugu ni yule ambaye udugu wake ukikatwa anauunga".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Kuwa mwanadamu kamili katika kuunga udugu na kuwatendea wema ndugu wa karibu si yule mtu mwenye kulipa wema aliotendewa, Bali muunga udugu halisi na kamili katika kuunga udugu ni yule ambaye ukikatwa udugu wake anauunga, hata wakimtendea ubaya; basi yeye huwalipa wema.
Mafunzo
- Kuunga udugu kunakozingatiwa kisheria ni kumuunga aliyekukata miongoni mwao, na kumsamehe aliyekudhulumu, na kumpa aliyekunyima, na si kuunga udugu kwa kubadilishana (wakiniunga nitawaunga wakikata nawakata) au kulipa wema uliotendewa.
- Kuunga udugu kunakuwa kwa kufikisha kheri kwa kadiri ya uwezo, kwa kutumia mali na dua na kuamrishana mema na kukatazana maovu na mfano wake, na kuzuia yawezekanayo katika shari juu yao.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 6) (5991).
منار القاري شرح مختصر صحيح البخاري، لحمزة محمد قاسم (5/ 242).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (1/ 397).
نزهة المتقين، لمصطفى الخن وغيره (1/ 311).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 190).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «انْصُرْ أَخَاكَ ظَالِمًا أَوْ مَظْلُومًا». فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَنْصُرُهُ إِذَا كَانَ مَظْلُومًا، أَفَرَأَيْتَ إِذَا كَانَ ظَالِمًا كَيْفَ أَنْصُرُهُ؟ قَالَ: « تَحْجُزُهُ -أَوْ تَمْنَعُهُ- مِنَ الظُّلْمِ؛ فَإِنَّ ذَلِكَ نَصْرُهُ».
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Msaidie ndugu yako akiwa amedhulumu au kudhulumiwa", Akasema mtu mmoja: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unaonaje ikiwa ndugu yangu kadhulumu, vipi nitamsaidia? Akasema: "Unamuhama au unamzuia asifanye dhulma, kwa kufanya hivyo ndiyo kumnusuru".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemuamrisha Muislamu kumsadia ndugu yake Muislamu sawa sawa awe kadhulumu au kadhulumiwa, mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimnusuru atakapokuwa emedhulumiwa kwa kumuondolea dhuluma, wasemaje ikiwa kadhulumu nitamsaidia vipi? Akasema: Utamzuia, na kumshika mkono na umkinge na umzuie na dhuluma; kwa kufanya hivyo ndiko kumnusuru dhidi ya Shetani wake na nafsi yake yenye kuamrisha maovu.
Mafunzo
- Hapa kuna tahadhari juu ya haki miongoni mwa haki za udugu wa kiimani baina ya Waislamu.
- Kumzuia dhalimu, na kumkataza dhidi ya dhuluma.
- Uislamu unakwenda kinyume na uelewa wa zama za ujinga, kiasi ambacho walikuwa wakisaidizana sawa sawa wawe wamedhulumiwa wao wamemdhulumu mwingine.
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 128) (2443).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 589).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 326).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللهَ يَرْضَى لَكُمْ ثَلَاثًا، وَيَكْرَهُ لَكُمْ ثَلَاثًا، فَيَرْضَى لَكُمْ: أَنْ تَعْبُدُوهُ، وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا، وَأَنْ تَعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا، وَيَكْرَهُ لَكُمْ: قِيلَ وَقَالَ، وَكَثْرَةَ السُّؤَالِ، وَإِضَاعَةِ الْمَالِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwenu mambo matatu, na anachukia kwenu mambo matatu, basi anaridhia kwenu: Mumuabudu yeye, na wala msimshirikishe na chochote, na mshikamane katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala msifarakane, na anachukia kwenu mambo matatu: Umbeya, na kuuliza uliza sana, na kupoteza mali".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu anapenda kwa waja wake mambo matatu, na anachukia kutoka kwao mambo matatu, anapenda kutoka kwao: Wampwekeshe yeye pekee na wala wasimshirikishe na chochote, na washikamane na ahadi ya Mwenyezi Mungu na Qur'ani na mafundisho ya Nabii wake wote, na wala wasifarakane katika umoja wa Waislamu. Na anachukia kwao: Upuuzi na maneno yasiyokuwa na faida katika yale yasiyowahusu, na kuuliza jambo ambalo bado halijatokea, au kuwaomba watu mali zao, na vile wanavyovimiliki, na yale yasiyokuwa na ulazima wa kuyaomba, na kupoteza mali na kuzitumia katika njia zisizokuwa za kisheria, na kuziweka katika uharibifu.
Mafunzo
- Anapenda Mwenyezi Mungu Mtukufu kutoka kwa waja wake utakasifu katika ibada zake, na anachukia kumkufuru.
- Himizo la kushikana katika kamba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwakuwa ndani yake kuna umoja na maelewano.
- Himizo la umoja, na amri ya kushikamana nao na kuziweka pamoja safu zake, na katazo la kinyume chake kama kufarakana na kuhitilafiana.
- Katazo la kukithirisha maneno kwa yale yasiyomuhusu; kwa sababu yakiwa ni ya halali basi ndani yake kuna kupoteza wakati, na yakiwa ya haramu basi kutakuwa na madhambi mengi.
- Katazo la kujiingiza katika habari za watu na kufuatilia hali zao na kusimulia kauli zao na matendo yao.
- Katazo la kukithirisha maswali katika mambo ya watu.
- Uharamu wa kupoteza mali, na himizo la kuzihifadhi na kuzitumia katika yale yanayofaa.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1340) (1715).
البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (30/ 85).
إكمال المعلم بفوائد مسلم (5/ 568).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَلاَ أُخْبِرُكُمْ بِأَفْضَلَ مِنْ دَرَجَةِ الصِّيَامِ وَالصَّلاَةِ وَالصَّدَقَةِ؟» قَالُوا: بَلَى، قَالَ: «صَلاَحُ ذَاتِ البَيْنِ، فَإِنَّ فَسَادَ ذَاتِ البَيْنِ هِيَ الحَالِقَةُ».
Kutoka kwa Abuu Dardai -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hivi nisikuelezeni lililo bora kuliko daraja ya swaumu na swala na sadaka?" Wakasema: Tueleze, akasema: "Kusuluhisha kati ya watu, kwani kuharibika kwa mahusiano baina ya watu hilo hunyoa".
Imepokelewa na Abu Daud na TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo
Aliwauliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake: Je, nikuelezeni lililo bora kuliko kuzidisha ibada za sunna kama swaumu na swala na sadaka? Wakasema: Ndio. Akasema: Ni kuwapatanisha waliogombana kwani ugomvi huleta mfarakano na kujitenga na kuchukiana na kupeana migongo kati ya watu, kwani yanayoambatana na kuharibika kwa mahusiano baina ya watu miongoni mwa chuki ndio jambo ambalo katika tabia zake huangamiza na kuing'oa dini na dunia kama wembe unavyong'oa nywele.
Mafunzo
- Muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kuwauliza Maswahaba zake na kuwatia shauku ya kujua jawabu.
- Amesema Al-Twayyibi: Himizo na hamasa ya kusuluhisha baina ya watu na kujiepusha na kuwavuruga; kwa sababu kutengemaa ndio sababu ya kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu na kutofarakana baina ya Waislamu, na kuharibu mahusiano ni pengo katika dini, na atakeyejitosa kulirekebisha na kuondoa uharibifu wake atapata daraja la juu zaidi ya lile analolipata mfungaji mwenye kusimama usiku mwenye kujishughulisha na nafsi yake pekee.
Marejeo
سنن أبي داود (7/ 280) (4919).
سنن الترمذي (4/ 244) (2509).
تحفة الأحوذي (7/ 179).
شرح سنن أبي داود للعباد (559/ 32).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com