Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakika vitu hivi viwili ni haramu kwa wanaume wa umma wangu, ni halali kwa wanawake wao

عَن عَلِيٍّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: أَخَذَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَرِيرًا بِشِمَالِهِ، وَذَهَبًا بِيَمِينِهِ، ثُمَّ رَفَعَ بِهِمَا يَدَيْهِ، فَقَالَ: «إِنَّ هَذَيْنِ حَرَامٌ عَلَى ذُكُورِ أُمَّتِي، حِلٌّ لِإِنَاثِهِمْ».
Kutoka kwa Ally bin Abii Twaalib radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alichukua Mtume rehema na amani ziwe juu yake Hariri kwa mkono wake wa kushoto, na dhahabu kwa mkono wake wa kulia, kisha akazinyanyua kwa mikono yake, akasema: "Hakika vitu hivi viwili ni haramu kwa wanaume wa umma wangu, ni halali kwa wanawake wao".
Imepoekelewa na Abu Daud, Nasai na Ibn MajahDarajaSahihi
Maelezo

Alichukua Mtume rehema na amani ziwe juu yake nguo ya hariri au kipande chake, kwa mkono wake wa kushoto, na akachukua pambo la dhahabu au mfano wake kwa mkono wake wa kulia, kisha akasema: Hakika hariri na dhahabu ni haramu kuvivaa kwa wanaume, ama wanawake hivyo ni halali kwao.

Mafunzo
  1. Amesema As- Sanadi: (Haram): Makusudio yake ni kuvitumia kwa kuvaa; na matumizi mengine ni ruhusa kwa wote, kama kubadilishana, kuvitoa sadaka na kuuza, na kutumia dhahabu kwa kufanya vyombo na kuvitumia ni haramu kwa wote.
  2. Sheria ya Uislamu imepanua wigo kwa wanawake kwakuwa wao wanahitaji zaidi mapambo na mfano wake.
Marejeo

سنن أبي داود (6/ 165) (4057). سنن النسائي (8/ 160) (5144). سنن ابن ماجه (4/ 594) (3595). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 613). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 99).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Mavazi na Mapambo.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com