عَن عَلِيٍّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: أَخَذَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَرِيرًا بِشِمَالِهِ، وَذَهَبًا بِيَمِينِهِ، ثُمَّ رَفَعَ بِهِمَا يَدَيْهِ، فَقَالَ: «إِنَّ هَذَيْنِ حَرَامٌ عَلَى ذُكُورِ أُمَّتِي، حِلٌّ لِإِنَاثِهِمْ».
Kutoka kwa Ally bin Abii Twaalib radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alichukua Mtume rehema na amani ziwe juu yake Hariri kwa mkono wake wa kushoto, na dhahabu kwa mkono wake wa kulia, kisha akazinyanyua kwa mikono yake, akasema: "Hakika vitu hivi viwili ni haramu kwa wanaume wa umma wangu, ni halali kwa wanawake wao".
Imepoekelewa na Abu Daud, Nasai na Ibn MajahDarajaSahihi
Maelezo
Alichukua Mtume rehema na amani ziwe juu yake nguo ya hariri au kipande chake, kwa mkono wake wa kushoto, na akachukua pambo la dhahabu au mfano wake kwa mkono wake wa kulia, kisha akasema: Hakika hariri na dhahabu ni haramu kuvivaa kwa wanaume, ama wanawake hivyo ni halali kwao.
Mafunzo
- Amesema As- Sanadi: (Haram): Makusudio yake ni kuvitumia kwa kuvaa; na matumizi mengine ni ruhusa kwa wote, kama kubadilishana, kuvitoa sadaka na kuuza, na kutumia dhahabu kwa kufanya vyombo na kuvitumia ni haramu kwa wote.
- Sheria ya Uislamu imepanua wigo kwa wanawake kwakuwa wao wanahitaji zaidi mapambo na mfano wake.
Marejeo
سنن أبي داود (6/ 165) (4057).
سنن النسائي (8/ 160) (5144).
سنن ابن ماجه (4/ 594) (3595).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 613).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 99).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن أبي هريرة رضي الله عنه قال: لعن رسول الله صلى الله عليه وسلم الرجل يلبس لِبْسَةَ المرأة، والمرأة تلبس لِبْسَةَ الرجل.
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amemlaani Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume anayevaa vazi la mwanamke, na mwanamke anayevaa vazi la mwanaume.
Imepokelewa na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah kwa maana yake na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Aliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema za Mwenyezi Mungu kwa kila mwanaume atakayejifananisha na mwanamke katika mavazi maalumu kwa ajili ya wanawake; sawa sawa iwe katika muonekano au rangi au jinsi au namna ya uvaaji na kujipamba. Au kwa mwanamke kujifananisha na mavazi maalumu kwa wanaume vile vile, nalo ni dhambi katika madhambi makubwa.
Mafunzo
- Amesema Shaukani: Kumeharamishwa wanawake kujifananisha na wanaume na wanaume kujifananisha na wanawake; kwa sababu laana huwa haiwi ila kwa kufanya jambo lililoharamishwa.
- Amesema bin Uthaimiin: Zile wanazoshirikiana kati yao, mfano kama jezi au shati ambazo wanazivaa wanaume na wanawake hizi hazina tatizo, yaani hakuna tatizo akizivaa mwanaume na mwanamke; kwa sababu wanashirikiana.
Marejeo
سنن أبي داود (6/ 195) (4098).
السنن الكبرى للنسائي (8/ 297) (9209).
سنن ابن ماجه (3/ 95) (1903).
مسند أحمد (14/ 61) (8309).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1122).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (19/ 337).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 150).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 370).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما قال: لعن النبي صلى الله عليه وسلم الوَاصِلَةَ والمُسْتَوْصِلَةَ، والوَاشِمَةَ والمُسْتَوشِمَةَ.
Imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- amesema: Kamlaani Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuunga nywele na mwenye kuungwa, na mwenye kuchora chata na mwenye kuchorwa.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Dua ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kulaaniwa na kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa makundi ya aina nne: La kwanza: Mwanamke mwenye kuunga nywele zake au za mwenzake kwa nywele zingine. La pili: Na mwenye kutaka kuungwa nywele, kwa kumuomba mwenzake amuunganishe nywele zake kwa nywele zingine. La tatu: Mwenye kupiga chata, na anayejichoma sindano katika sehemu ya mwili wake, kama uso au kiganja au kifua, na kuweka wanja au mfano wake, ili kubakie alama ya bluu, au kijani; kwa kutaka kujipamba au uzuri. La nne: Mwenye kutaka kupigwa chata, ni yule anayeomba kupigwa chata. Na matendo haya ni katika madhambi makubwa.
Mafunzo
- Amesema bin Hajari: Ni kwamba linalozuiwa katika hilo kuunga nywele kwa nywele, na ama akiunga nywele kwa kitu kingine kisichokuwa nywele kama kitambaa au kinginecho haitoingia katika katazo.
- Katazo la kusaidizana katika madhambi.
- katazo la kubadili umbile la Mwenyezi Mungu; kwa sababu kufanya hivyo ni udanganyifu na ni ghushi.
- Kufaa kumlaani aliyelaaniwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa mfumo wa ujumla.
- Inaingia katika kuunga nywele katika zama zetu hizi kuvaa mawigi, nalo ni jambo la haramu, kwakuwa kuna kujifananisha na makafiri na udanganyifu na ghushi na uongo.
- Amesema Khattwabi: Hakika imekuja ahadi ya adhabu kali katika mambo haya; kwakuwa ndani yake kuna ghushi na udanganyifu, na lau lingeruhusiwa lolote katika haya ingelikuwa njia ya kuhalalisha mengine katika aina za ghushi, na kwakuwa ndani yake kuna kubadili maumbile, na katika hilo kuna ishara ya hadithi ya bin Masudi kwa kauli yake: "Wenye kubadili maumbile ya Mwenyezi Mungu", na Allah ndiye mjuzi zaidi.
- Amesema Nawawi: Nalo ni jambo la haramu kwa mfanyaji na mwenye kufanyiwa, na sehemu aliyochorwa inakuwa najisi, ikiwa ataweza kuiondoa kwa tiba basi ni wajibu kwake kufanya hivyo na isipowezekana basi aiondoa kwa upasuaji, ikiwa atahofia kuharibika au kukosa kiungo au matumizi yake au chochote kibaya katika kiungo kinachoonekana basi haitokuwa wajibu kwake kuiondoa, na akitubia hatobaki na madhambi, na asipohofia chochote katika hayo basi ni lazima kwake, na atakuwa ameasi akichelewesha kuiondoa. Mwisho.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 167) (5947).
صحيح مسلم (3/ 1677) (2124).
توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (5/ 373).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (3/ 157).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (7/ 354).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا تَمْنَعُوا إِمَاءَ اللَّهِ مَسَاجِدَ اللَّهِ، وَلَكِنْ لِيَخْرُجْنَ وَهُنَّ تَفِلَاتٌ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiwazuie vijakazi wa Mwenyezi Mungu kwenda katika misikiti ya Mwenyezi Mungu, lakini wakitaka kutoka watoke wakiwa hawajajipamba".
Imepokelewa na Abu DaudDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake msimamizi wa mwanamke na muhusika wake kuwakataza wanawake kwenda Msikitini, na akawaamrisha wanawake wakati wa kutoka kwenda Msikitini watoke bila kujipuliza manukato na wasitoke kwa kujiachia kwa mapambo; ili wasiwe sababu ya fitina kwa wanaume.
Mafunzo
- Kumpa ruhusa mwanamke ya kwenda kuswali Msikitini atapokuwa na uhakika wa kutopata fitina, na akatoka bila mapambo wala manukato.
- Wameitumia hadithi hii kama ushahidi kuwa mwanamke hatoki nyumbani kwake isipokuwa kwa idhini yake, kwakuwa amri ya idhini imeelekezwa kwa wanaume.
- Uislamu umewapa kipaumbele wanawake, na kutowazuia kwa mambo ambayo yanaweza kuwa ni heri kwao kama kutoka kwenda kutafute elimu na mfano wake.
- Kuthibiti kwa usimamizi wa mwanaume juu ya mwanamke na kumchunga.
Marejeo
سنن أبي داود (1/ 423) (565).
شرح سنن أبي داود للعباد (78/ 6).
شرح أبي داود للعيني (3/ 50).
النهاية في غريب الحديث والأثر ص(109).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَا أَسْفَلَ مِنَ الكَعْبَيْنِ مِنَ الإِزَارِ فَفِي النَّارِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kilichoshuka chini ya kongo mbili katika kikoi hicho ni motoni".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kushusha chini zaidi ya miguu kila kinachositiri kuanzia chini ya mwili wake kama nguo au suruali au kinginecho, na kinachokuwa zaidi ya kongo mbili katika miguu miongoni mwa kikoi kinachoburuza basi hicho ni motoni ikiwa ni adhabu kwake kwa kitendo hicho.
Mafunzo
- Katazo la kurefusha nguo mpaka chini ya kongo mbili kwa wanaume, nakwamba hilo ni katika madhambi makubwa.
- Amesema bin Hajari: Na kinaondolewa katika kuburuza kikoi moja kwa moja kila alichokiburuza kwa dharura; kama atakayekuwa na jeraha katika kongo mbili zake kwa mfano ikiwa nzi watamuudhi kama hatulifunika kwa kikoi chake, kwa kutopata kitu kingine cha kufunika.
- Hukumu hii ni maalumu kwa wanaume; kwa sababu wanawake wameamrishwa washushe nguo zao chini ya kongo mibili kiasi cha dhiraa moja (inchi 18).
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 141) (5787).
إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (8/ 418).
ذخيرة العقبى في شرح المجتبى (23/ 76).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com