Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Matumizi.

Hadithi 5

Chukua katika mali yake kwa wema, kiasi kinachokutosha wewe na wanao

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمنينَ رَضيَ اللهُ عنها قَالَت: دَخَلَتْ هِنْدٌ بِنْتُ عُتْبَةَ امْرَأَةُ أَبِي سُفْيَانَ عَلَى رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللهِ، إِنَّ أَبَا سُفْيَانَ رَجُلٌ شَحِيحٌ، لَا يُعْطِينِي مِنَ النَّفَقَةِ مَا يَكْفِينِي وَيَكْفِي بَنِيَّ إِلَّا مَا أَخَذْتُ مِنْ مَالِهِ بِغَيْرِ عِلْمِهِ، فَهَلْ عَلَيَّ فِي ذَلِكَ مِنْ جُنَاحٍ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «خُذِي مِنْ مَالِهِ بِالْمَعْرُوفِ مَا يَكْفِيكِ وَيَكْفِي بَنِيكِ».
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliingia Hindu binti Utba mke wa Abuu Sufiani kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika Abuu Sufiani ni mwanaume bahili sana, hanipi matumizi yanayonitosha mimi na wanangu isipokuwa kiasi ninachokichukua katika mali yake pasina yeye kujua, je kwa hilo nina tatizo? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Chukua katika mali yake kwa wema, kiasi kinachokutosha wewe na wanao".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alitaka kujua Hindu binti Utba radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mume wake Abuu Sufiani radhi za Allah ziwe juu yake, na kwamba yeye ni mwanaume bahili mwenye pupa sana na mali yake, hampi katika matumizi kiasi kinachomtosha yeye na wanaye, mpaka achukue katika mali yake kwa siri hali yakuwa hajui, je ana dhambi juu yake katika hilo?. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Chukua kwa ajili yako na watoto wako katika mali yake kiasi kinachojulikana katika mazingira ya kawaida na kwamba hicho ndicho kitakachomtosheleza hata asipojua.

Mafunzo
  1. Uwajibu wa kutoa mahitaji kwa mke na watoto.
  2. Amesema bin Hajari: Na makusudio ya kauli yake: "Chukua katika mali yake kiasi kinachokutosha kwa wema", akamuelekeza katika wema kwa kiasi ambacho hakina kiwango katika sheria.
  3. Amesema bin Hajari: Hadithi hii imetumika kama ushahidi wa kuruhusu kumtaja mtu kwa yale asiyoyapenda ikiwa katika mfumo wa kuuliza na kulalamika na mfano wake, na hii ni moja kati ya sehemu ambazo hi halali ndani yake kusengenya.
  4. Amesema Qurtubi: Hindu hakukusudia kumsifia Abuu Sufiani kwa ubahili kwa hali zote, bali alieleza hali yake akiwa naye na kwamba yeye alikuwa akimtiadhiki yeye na wanaye, na hii haimaanishi ubahili wa moja kwa moja, kwani viongozi wengi hufanya hivyo kwa familia zao na huwaathiri sana upande wa kujenga mapenzi nao.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 79) (2211). صحيح مسلم (3/ 1338) (1714). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص700). الإعلام بفوائد عمدة الأحكام، لابن الملقن (10/ 12).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ وَهُوَ عَلَى المِنْبَرِ، وَذَكَرَ الصَّدَقَةَ، وَالتَّعَفُّفَ، وَالمَسْأَلَةَ: «اليَدُ العُلْيَا خَيْرٌ مِنَ اليَدِ السُّفْلَى، فَاليَدُ العُلْيَا: هِيَ المُنْفِقَةُ، وَالسُّفْلَى: هِيَ السَّائِلَةُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema huku akiwa juu ya Mimbari, na akataja sadaka, na kujizuia kuomba, na kuombaomba: "Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini, mkono wa juu: Ni ule unaotoa, na mkono wa chini: Ni ule unaoomba".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitaja sadaka, na kujizuia kuombaomba, aliyasema hayo wakati akihutubia katika Mimbari; kisha akasema: Mkono wa juu wenye kutoa sadaka ni bora na unapendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko mkono wa chini wenye kuomba.

Mafunzo
  1. Hapa kuna fadhila za ukarimu na utoaji katika njia za kheri, na ubaya wa kuombaomba.
  2. Hapa kuna himizo la kujizuia kuomba, na kuwaepuka watu, na himizo la kufanya mambo matukufu, na kuacha yenye udhalili, na Mwenyezi Mungu anapenda mambo ya juu zaidi.
  3. Mikono ina aina nne katika ubora, kama ifuatavyo: Wa juu zaidi ni ule unaotoa, kisha unaojizuia kuchukua, kisha unaopokea pasina kuomba, kisha unafuata wa chini kuliko hiyo, ule unaoomba.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 112) (1429). صحيح مسلم (2/ 717) (1033). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 590). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 465). التوضيح لشرح الجامع الصحيح، لابن الملقن (10/ 315). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 388). تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي، المباركفوري (3/ 288). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص212).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Toa ewe mwanadamu na mimi nikupe

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «قَالَ اللهُ: أَنْفِقْ يَا ابْنَ آدَمَ أُنْفِقْ عَلَيْكَ».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Toa ewe mwanadamu na mimi nikupe".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Toa ewe mwanadamu -katika matumizi ya wajibu na ya hiyari- nikukunjulie na nikupe badala ya hicho na nikubariki ndani yake.

Mafunzo
  1. Himizo la kutoa sadaka na kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu.
  2. Kutoa katika njia za heri ni miongoni mwa sababu kubwa za kupata baraka katika riziki na kuzidishwa kwake, na Mwenyezi Mungu kumpa badala mja katika kile alichokitoa.
  3. Hadithi hii ni katika zile anazozipokea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mola wake Mlezi, na huitwa Hadithil Qudsi au Hadithil Ilahi, nayo ni ile ambayo tamko lake na maana yake inatoka kwa Allah, isipokuwa haina upekee kama wa Qur'ani inaojipambanua nayo kwa vingine, ikiwa kisomo chake kutumika katika ibada, na kuwa twahara kabla ya kusoma, na kuwashinda watu kwa changamoto zake, na mengineyo.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 62) (5352). صحيح مسلم (2/ 690) (993). شرح النووي على مسلم (7/ 79). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 603).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Dinari moja unayoitoa kwenye njia ya Allah, na dinari moja unayoitoa kwa mtumwa, na dinari moja unayoitoa sadaka kwa masikini, na dinari moja unayoitoa kwa familia yako, yenye malipo makubwa kuliko yote ni ile unayoitoa kwa familia yako

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قالَ: قالَ رَسُولُ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليْه وسلَّمَ: «دِينَارٌ أَنْفَقْتَهُ فِي سَبِيلِ اللهِ، وَدِينَارٌ أَنْفَقْتَهُ فِي رَقَبَةٍ، وَدِينَارٌ تَصَدَّقْتَ بِهِ عَلَى مِسْكِينٍ، وَدِينَارٌ أَنْفَقْتَهُ عَلَى أَهْلِكَ أَعْظَمُهَا أَجْرًا الَّذِي أَنْفَقْتَهُ عَلَى أَهْلِكَ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Dinari moja unayoitoa kwenye njia ya Allah, na dinari moja unayoitoa kwa mtumwa, na dinari moja unayoitoa sadaka kwa masikini, na dinari moja unayoitoa kwa familia yako, yenye malipo makubwa kuliko yote ni ile unayoitoa kwa familia yako".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ametaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya aina za utoaji, akasema: Dinari uliyoitoa katika Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari uliyoitoa katika shingo ya mtumwa, na dinari uliyoitoa sadaka kwa masikini mwenye uhitaji, na dinari uliyoitoa kwa watu wako na familia yako, kisha akaeleza kuwa yenye malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu ni ile uliyoitoa kwa watu wako na familia na wale wanaokulazimu kuwahudumia.

Mafunzo
  1. Wingi wa milango ya kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu.
  2. Kutanguliza kilicho bora katika mlango wa kutoa panapokuwa na msongamano wa mambo, na miongoni mwake ni kutoa kwa familia uwezo unapokosekana wa kuyatekeleza yote.
  3. Amesema Nawawi katika kitabu cha Sharhe Muslim: Himizo la kutoa matumizi kwa familia, na kumebainishwa ukubwa wa thawabu ndani yake; kwa sababu wako miongoni mwao wanaomlazimu kuwahudumia kwa sababu ya ukaribu wa udugu, na yuko miongoni mwao inakuwa ni sunna na inakuwa ni sadaka na kuunga udugu, na yuko ambaye inakuwa wajibu kwa kummiliki kwa sababu ya ndoa au umiliki wa kuume (kama mateka na vijakazi), na hii yote ni fadhila iliyohimizwa, nayo ni bora kuliko sadaka ya hiyari.
  4. Amesema As-Sanadi: Kauli yake "Dinari anayoitoa kwa familia yake", Yaani: Atakaponuia kupata radhi za Allah na akakusudia kutoa katika familia kwa mfano haki.
  5. Amesema Abuu Qilaba: Na ni mtu gani mwenye malipo makubwa kuliko mtu anayetoa matumizi kwa familia ndogo anayowasitiri au Mwenyezi Mungu anawanufaisha kwayo na kuwatosheleza?!
Marejeo

صحيح مسلم (2/ 692) (995). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 156). نزهة المتقين بشرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 291). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 374). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص209).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakapotoa matumizi mtu kwa familia yake kwa kutaraji malipo, basi hiyo kwake ni sadaka

عن أبي مسعود رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «إِذَا أَنْفَقَ الرَّجُلُ عَلَى أَهْلِهِ يَحْتَسِبُهَا فَهُوَ لَهُ صَدَقَةٌ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapotoa matumizi mtu kwa familia yake kwa kutaraji malipo, basi hiyo kwake ni sadaka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakapotoa mtu matumizi kwa familia yake, wale anaolazimika kuwahudumia kama mke wake na watoto wake na wengineo huku akijikurubisha kwa Allah Mtukufu kwa hilo, na akitaraji malipo kwake kwa yale anayowahudumia basi atakuwa na malipo ya sadaka.

Mafunzo
  1. Hupatikana malipo na thawabu kwa kuihudumia familia.
  2. Muumini hutaraji radhi za Allah katika amali yake na yale yaliyoko kwake katika malipo na thawabu.
  3. Ni lazima kuhudhurisha nia njema katika kila amali, na katika amali hizo ni wakati wa kuhudumia familia.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 20) (55). صحيح مسلم (2/ 695) (1002). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (5/ 334). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 157). نزهة المتقين بشرح رياض الصالحين، لمصطفى الخن وغيره (1/ 293). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، سليم الهلالي (1/ 375).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com