Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakuacha Jibrili kuniusia kuhusu jirani, mpaka nikadhania kuwa atamrithisha

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَا زَالَ يُوصِينِي جِبْرِيلُ بِالْجَارِ، حَتَّى ظَنَنْتُ أَنَّهُ سَيُوَرِّثُهُ».
Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuacha Jibrili kuniusia kuhusu jirani, mpaka nikadhania kuwa atamrithisha".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Jibrili akikariri kwake na akimuamrisha kumjali jirani, ambaye ni wakaribu kimakazi, sawa awe muislamu au kafiri, na sawa sawa awe ndugu wa karibu wa mbali, kwa kuhifadhi haki zake na kutomuudhi, na kumtendea wema na kuvumulia kero zake, mpaka akadhania -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kule kuitukuza kwake haki ya jirani na kitendo cha Jibrili kulirudiarudia hilo kwamba utakuja kuteremsha wahyi wa kumpa katika mali zake jirani yake atakayebakia baada ya kifo chake.

Mafunzo
  1. Ukubwa wa haki za jirani na uwajibu wa kulichunga hilo.
  2. Msisitizo juu ya haki za jirani kwa kutoa usia, hii inamaanisha ulazima wa kumkirimu na kujipendekeza kwake na kumtendea wema, na kumzuilia madhara, na kumtembelea wakati wa maradhi, na kumpongeza wakati wa furaha, na kumpa pole wakati wa msiba.
  3. Kila unavyozidi kuwa karibu mlango wa jirani ndivyo ambavyo haki yake inazidi kuwa na mkazo zaidi.
  4. Ukamilifu wa sheria katika yale iliyokuja nayo, katika yale yenye kuitengeneza jamii kama kumtendea wema jirani, na kumzuilia madhara.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 10) (6014)، (8/ 10) (6015). صحيح مسلم (4/ 2025) (2624)، (4/ 2025) (2625). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين (1/ 300). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 175).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Suluhisho na hukumu za ujirani.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com