Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Suluhisho na hukumu za ujirani.

Hadithi 3

Hakuacha Jibrili kuniusia kuhusu jirani, mpaka nikadhania kuwa atamrithisha

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَا زَالَ يُوصِينِي جِبْرِيلُ بِالْجَارِ، حَتَّى ظَنَنْتُ أَنَّهُ سَيُوَرِّثُهُ».
Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuacha Jibrili kuniusia kuhusu jirani, mpaka nikadhania kuwa atamrithisha".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Jibrili akikariri kwake na akimuamrisha kumjali jirani, ambaye ni wakaribu kimakazi, sawa awe muislamu au kafiri, na sawa sawa awe ndugu wa karibu wa mbali, kwa kuhifadhi haki zake na kutomuudhi, na kumtendea wema na kuvumulia kero zake, mpaka akadhania -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kule kuitukuza kwake haki ya jirani na kitendo cha Jibrili kulirudiarudia hilo kwamba utakuja kuteremsha wahyi wa kumpa katika mali zake jirani yake atakayebakia baada ya kifo chake.

Mafunzo
  1. Ukubwa wa haki za jirani na uwajibu wa kulichunga hilo.
  2. Msisitizo juu ya haki za jirani kwa kutoa usia, hii inamaanisha ulazima wa kumkirimu na kujipendekeza kwake na kumtendea wema, na kumzuilia madhara, na kumtembelea wakati wa maradhi, na kumpongeza wakati wa furaha, na kumpa pole wakati wa msiba.
  3. Kila unavyozidi kuwa karibu mlango wa jirani ndivyo ambavyo haki yake inazidi kuwa na mkazo zaidi.
  4. Ukamilifu wa sheria katika yale iliyokuja nayo, katika yale yenye kuitengeneza jamii kama kumtendea wema jirani, na kumzuilia madhara.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 10) (6014)، (8/ 10) (6015). صحيح مسلم (4/ 2025) (2624)، (4/ 2025) (2625). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين (1/ 300). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 175).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ewe Abuu Dhari utakapopika mchuzi basi zidisha maji yake, na umkumbuke jirani yako

عَنْ أَبِي ذَرٍّ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يَا أَبَا ذَرٍّ إِذَا طَبَخْتَ مَرَقَةً فَأَكْثِرْ مَاءَهَا، وَتَعَاهَدْ جِيرَانَكَ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Ewe Abuu Dhari utakapopika mchuzi basi zidisha maji yake, na umkumbuke jirani yako".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alimhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Abuu Dhari Al-Ghifaari radhi za Allah ziwe juu yake atakapopika mchuzi basi azidishe maji yake na mchuzi wake, na amkumbuke na amtafute jirani yake.

Mafunzo
  1. Himizo la kuwa na mahusiano mazuri na jirani.
  2. Sunna ya kupeana zawadi kati ya majirani wawili; kwa sababu hilo linaleta mapenzi na mahaba, na kunakuwa na mkazo zaidi kupeana zawadi huku pindi chakula kinapokuwa na harufu nzuri, na ikajulikana hali ya jirani.
  3. Himizo la kutenda wema na kila kinachowezekana hata kikiwa kidogo, na kuingiza furaha kwa waislamu.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2025) (2625). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 386). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 175). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 301).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini", wakasema: Na ni nani huyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ambaye hapati amani jirani yake kwa kero zake

عَنْ أَبِي شُرَيْحٍ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ، وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ، وَاللَّهِ لاَ يُؤْمِنُ»، قِيلَ: وَمَنْ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: «الَّذِي لاَ يَأْمَنُ جَارُهُ بَوَايِقَهُ».
Kutoka kwa Abuu Shuraihi radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini", wakasema: Na ni nani huyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ambaye hapati amani jirani yake kwa kero zake".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Aliapa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akasisitiza kiapo chake mara tatu, akasema: Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Maswahaba wakamuuliza: Na ni nani ambaye hawezi kuamini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ambaye jirani anahofia usaliti wake na dhulma zake na shari zake.

Mafunzo
  1. Kukanushwa imani kwa yule ambaye jirani yake hapati amani kutokana na dhulma zake na shari zake hili linaonyesha kuwa ni katika madhambi makubwa, na kwamba mfanyaji wake anaupungufu wa imani.
  2. Himizo la msisitizo juu ya kumtendea wema jirani na kuacha kumuudhi kwa kauli au kitendo.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 10) (6016). التوضيح لشرح الجامع الصحيح (28/ 321). النهاية في غريب الحديث والأثر (93).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com