Kutoka kwa Ubai bin Ka'ab radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alitusalisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala ya asubuhi, akasema: "Hivi fulani yupo", Wakasema: Hapana, akasema: "Na je fulani yupo?", Wakasema: Hapana: Akasema: "Hakika swala hizi mbili, ni swala nzito sana kwa wanafiki, na lau kama mngejua malipo yaliyomo basi mngezijia, hata kwa kutambaa kwa magoti, na hakika safu ya kwanza iko katika mithili ya safu ya Malaika, na laiti mngejua ni zipi fadhila zake basi mngezijia haraka mno, na hakika swala ya mtu na mwenzie ni safi zaidi kuliko swala yake peke yake, na swala yake akiwa na watu wawili ni nzuri zaidi kuliko swala yake na mtu mmoja, na wingi unavyozidi ndio unaopendeka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu".
Pale ambapo Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa (HadeethEnc.com) ina maandishi yaleyale ya hadithi, tafsiri yake huonyeshwa chini ya hadithi hiyo pamoja na jina la chanzo. Zimeoanishwa na programu, kwa Kiarabu pekee: maandishi yote ya hadithi katika ensaiklopidia, pamoja na Sahaba anayetajwa ndani yake, ndiyo mwisho wa hadithi hiyo herufi kwa herufi. Hakuna aliyekagua uoanishaji huu, na wahakiki wa Sabīl hawajaichunguza tafsiri. Kiarabu ndiyo maandishi yenyewe.
Maandishi ya Kiarabu, namba, majina ya vitabu na madaraja vinaonyeshwa sawasawa na vilivyo katika seti ya data iliyo wazi (hadith-api). Sabīl bado haijathibitisha usahihi wake wala haki zake, na uhakiki wake wa wanazuoni haujaanza. Hadi hapo, linganisha hadithi na toleo lililochapishwa kabla ya kuitegemea.