Al-An'aam
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَجَعَلَ ٱلظُّلُمَـٰتِ وَٱلنُّورَ ۖ ثُمَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ 1
{1} Huku ni kujulisha kuhusu kuhimidiwa kwake na kusifiwa kwake kwa sifa za ukamilifu, na sifa za ukuu na utukufu kwa ujumla, na kwa mambo haya yaliyotajwa hasa. Basi akajisifu kwa kuumba Yeye mbingu na ardhi, yenye kuashiria ukamilifu wa uwezo wake, na upana wa elimu yake, na rehema yake, na ujumla wa hekima yake, na upekee wake katika kuumba na kuendesha mambo. Na katika kufanya kwake giza mbalimbali na nuru, na hilo linajumuisha yanayohisiwa katika hayo kama vile usiku na mchana, jua na mwezi, na yasiyohisiwa kama vile giza mbalimbali za ujinga, na shaka, na ushirikina, na uasi, na kughafilika, na nuru ya elimu, na imani, na yakini, na utiifu. Na yote haya yanaashiria ishara ya uhakika kwamba Yeye Mtukufu ndiye anayestahiki kuabudiwa na kumfanyia dini Yeye tu; na pamoja na ushahidi huu na hoja iliyo wazi. "Kisha wale waliokufuru wanawafanya wengine kuwa sawa na Mola wao Mlezi." Wanawafanya kuwa sawa na Yeye katika ibada na utukufu, ijapokuwa hawakumsawazisha Mwenyezi Mungu (na wao) katika chochote cha ukamilifu. Na wao ni masikini, wasiojiweza, na wenye upungufu wa kila namna.