Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Hadid
Sura ya 57

Al-Hadid

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 8

وَمَا لَكُمْ لَا تُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ ۙ وَٱلرَّسُولُ يَدْعُوكُمْ لِتُؤْمِنُوا۟ بِرَبِّكُمْ وَقَدْ أَخَذَ مِيثَـٰقَكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ 8

{8} Kisha akataja sababu itakayowafanya kuamini na kutokuwepo kizuizi cha hilo, akasema: "Na mna nini hata hamumuamini Mwenyezi Mungu na hali Mtume anakuiteni mumuamini Mola wenu Mlezi? Naye amekwisha chukua ahadi yenu, ikiwa nyinyi ni Waumini." Yaani, ni nini kinakuzuieni kuamini, na hali Mtume Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, mbora wa Mitume na mlinganiaji mtukufu zaidi kwa Mwenyezi Mungu anakuiteni? Hili ni katika mambo yanayosababisha kuchukua hatua ya kuitikia wito wake na kuitikia haki aliyokuja nayo, na amechukua ahadi juu yenu na agano madhubuti kwamba mtaamini ikiwa nyinyi ni Waumini.