An-Nisaa
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ قِيلَ لَهُمْ كُفُّوٓا۟ أَيْدِيَكُمْ وَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ ٱلْقِتَالُ إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُمْ يَخْشَوْنَ ٱلنَّاسَ كَخَشْيَةِ ٱللَّهِ أَوْ أَشَدَّ خَشْيَةً ۚ وَقَالُوا۟ رَبَّنَا لِمَ كَتَبْتَ عَلَيْنَا ٱلْقِتَالَ لَوْلَآ أَخَّرْتَنَآ إِلَىٰٓ أَجَلٍ قَرِيبٍ ۗ قُلْ مَتَـٰعُ ٱلدُّنْيَا قَلِيلٌ وَٱلْـَٔاخِرَةُ خَيْرٌ لِّمَنِ ٱتَّقَىٰ وَلَا تُظْلَمُونَ فَتِيلًا 77
{77} Waislamu walipokuwa Makka, walikuwa wameamrishwa Swala na Zaka. Yani kuwafariji mafukara, sio Zaka kama inavyojulikana ambayo ina kiwango maalum cha chini (Niswab) na masharti yaliyowekwa. Hiyo haikufaradhishwa isipokuwa huko Madina. Na hawakuamrishwa kupigana Jihadi dhidi ya maadui kwa manufaa kadhaa: Miongoni mwake ni kwamba katika hekima za Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kwamba anawawekea sheria waja wake kwa njia ambayo si ngumu kwao, na aanze kwa kilicho muhimu zaidi, kisha muhimu zaidi, na kilicho rahisi zaidi, kisha rahisi zaidi. Miongoni mwake ni kwamba lau kuwa kupigana vita kungefaradhishwa juu yao licha ya uchache wao wa idadi na maandalizi, na wingi wa maadui zao, basi hilo lingepelekea kuporomoka kwa Uislamu. Kwa hivyo, ukaangaliwa upande wa masilahi makubwa zaidi juu ya yale yaliyo chini kuliko huo, na yasiyokuwa hayo miongoni mwa hekima. Na baadhi ya Waumini walikuwa wakipenda kwamba lau kuwa kupigana vita kungefaradhishwa juu yao katika hali hiyo ambayo havifai ndani yake. Bali kilichofaa ndani yake ni kufanya yale waliyoamrishwa kuyafanya wakati huo miongoni mwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu, na Swala, na Zaka na mfano wa hayo. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, “Na lau kama wangelifanya yale wanayowaidhiwa kwayo, basi ingelikuwa bora kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi”. Basi walipohamia Madina, na Uislamu ukawa na nguvu, wakaandikiwa kupigana vita katika wakati wake ufaao kufanya hivyo. Kwa hivyo, kundi miongoni mwa wale waliokuwa wakiharakisha waandikiwe kupigana vita kabla ya hayo kwa kuwaogopa watu, na kwa udhaifu na woga wakasema, “Mola Mlezi wetu! Kwa nini umetuamrisha kupigana vita?” Na katika hili kuna kutoridhia kwao na upinzani wao kwa Mwenyezi Mungu. Na lilikuwa linalowapasa ni kinyume cha hali hii, kusalimu amri ya Mwenyezi Mungu na kuwa na subira juu ya amri zake. Lakini wakafanya kinyume cha amri waliyotakiwa kufanya, na wakasema, “Lau ungetuahirisha kwa muda mfupi.” Yani kwa nini hungechelewesha kufaradhisha kupigana vita kwa muda wa baadaye kuliko wakati huu? Na hali hii mara nyingi hutokea kwa mtu asiye na kiasi na akakimbilia katika mambo kabla ya wakati wake. Uwezekano mkubwa zaidi, kwake ni kwamba hatakuwa na subira juu yake wakati wa kuja kwake, wala hasumbuki kuyabeba ipasavyo, bali anakuwa mchache wa subira. Kisha hakika Mwenyezi Mungu akawaidhi juu ya hali hii ambayo ndani yake kuna kusalia nyuma ya kupigana vita. Akasema, “Sema: Starehe ya dunia ni ndogo, na Akhera ni bora zaidi kwa mwenye kumcha Mungu.” Yani kufurahia ladha za dunia na starehe zake ni kuchache. Kwa hivyo, kustahimili kubeba mizigo katika kumtii Mwenyezi Mungu ndani ya muda mfupi ni katika yale yanayoirahisishia nafsi na kuifanyia kuwa mepesi. Kwa sababu zikijua kwamba dhiki ambazo zinazikumba hazitadumu kwa muda mrefu, inakuwa rahisi kwake kufanya hivyo. Basi itakuwaje ikiwa nafsi italinganisha baina ya dunia na Akhera, na kwamba Akhera ni bora kuiliko (dunia) yenyewe, na ladha zake, na muda wake? Na hiyo yenyewe ni kama alivyosema Nabii -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake– katika hadithi iliyothibiti kutoka kwake. “Hakika, pahali pa mjeledi katika Pepo ni bora kuliko dunia na vilivyomo ndani yake.” Na ladha zake ni safi kutokana na uchafu. Bali kila kitu kinachokuja akilini au kupita katika mawazo kuhusu mtazamo juu ya ladha yoyote ile, basi ladha ya Pepo ni juu ya hiyo. Kama alisema Yeye Mtukufu, “Basi nafsi yoyote haijui waliyofichiwa katika hayo yanayofurahisha macho.” Na Mwenyezi Mungu alisema kwa ulimi wa Nabii wake, “Nimewaandalia waja wangu wema yale ambayo jicho halijawahi kuyaona, wala sikio halijawahi kuyasikia, wala hayajawahi kupita katika moyo wa mwanadamu yeyote.” Ama ladha za dunia, hizo zimechanganywa na aina mbalimbali za dhiki ambazo, lau kuwa zitalinganishwa ladha zake na yale yanayofungamana nazo ya aina mbalimbali za uchungu, na wasiwasi, na huzuni, basi uwiano wowote haungejitokeza kwa namna yoyote ile. Na ama muda wake, basi Dunia hii inapita, na umri wa mtu kuhusiana na dunia ni jambo dogo. Na ama Akhera, hiyo ni yenye neema ya kudumu, na wakazi wake watakaa humo milele. Basi ikiwa mwenye akili atafikiria juu ya Nyumba mbili hizi, na akapata picha ya uhakika wake kwa haki ya kuona picha, atajua ni nini kinachostahiki zaidi kupendelewa, na kukifanyia kazi, kujitahidi kukitafuta. Na ndiyo maana akasema, “Na Akhera ni bora zaidi kwa mwenye kumcha Mungu.” Yani anayejiepusha na ushirikina na mambo mengine yaliyoharamishwa. “Wala hamtadhulumiwa hata chembe cha uzi wa kokwa ya tende.” Yani kuifanyia kazi kwenu Akhera, mtakukuta hali ya kuwa ni kukamilifu, kwingi, bila ya kupunguzwa chochote.