Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Naml
Sura ya 27

An-Naml

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 7

إِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِأَهْلِهِۦٓ إِنِّىٓ ءَانَسْتُ نَارًا سَـَٔاتِيكُم مِّنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ ءَاتِيكُم بِشِهَابٍ قَبَسٍ لَّعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ 7

{7} Anamaanisha: Kumbuka hali hii bora tukufu katika hali za Musa bin Imran, mwanzo wa ufunuo kumteremkia, kuteuliwa kwake kuwa Mtume, na kuongeleshwa kwake na Mwenyezi Mungu. Hayo ni kwamba alipokaa Madyani kwa miaka kadhaa, na akasafiri pamoja na familia yake kutoka Madyani wakienda Misri, na alipokuwa njiani, akapotea, na ulikuwa usiku wa giza na wenye baridi. Akawaambia, "Hakika nimeona moto" kwa mbali, "nitakwenda niwaletea habari kutoka huko" kuhusu barabara, "au nitawaletea kijinga kinachowaka ili mpate kuota moto." Na huu ni ushahidi kwamba alikuwa amepotea njia na kwamba alikuwa nahisi baridi sana, yeye na familia yake.