Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلْمَلَإِ مِنۢ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ مِنۢ بَعْدِ مُوسَىٰٓ إِذْ قَالُوا۟ لِنَبِىٍّ لَّهُمُ ٱبْعَثْ لَنَا مَلِكًا نُّقَـٰتِلْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۖ قَالَ هَلْ عَسَيْتُمْ إِن كُتِبَ عَلَيْكُمُ ٱلْقِتَالُ أَلَّا تُقَـٰتِلُوا۟ ۖ قَالُوا۟ وَمَا لَنَآ أَلَّا نُقَـٰتِلَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَقَدْ أُخْرِجْنَا مِن دِيَـٰرِنَا وَأَبْنَآئِنَا ۖ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيْهِمُ ٱلْقِتَالُ تَوَلَّوْا۟ إِلَّا قَلِيلًا مِّنْهُمْ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِٱلظَّـٰلِمِينَ 246 وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ ٱللَّهَ قَدْ بَعَثَ لَكُمْ طَالُوتَ مَلِكًا ۚ قَالُوٓا۟ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ ٱلْمُلْكُ عَلَيْنَا وَنَحْنُ أَحَقُّ بِٱلْمُلْكِ مِنْهُ وَلَمْ يُؤْتَ سَعَةً مِّنَ ٱلْمَالِ ۚ قَالَ إِنَّ ٱللَّهَ ٱصْطَفَىٰهُ عَلَيْكُمْ وَزَادَهُۥ بَسْطَةً فِى ٱلْعِلْمِ وَٱلْجِسْمِ ۖ وَٱللَّهُ يُؤْتِى مُلْكَهُۥ مَن يَشَآءُ ۚ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ 247
{246 - 247} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawasimulia watu kisa hiki ili wakizingatie na wapate moyo wa kufanya jihadi, na wasiwe na uoga juu yake. Kwa maana, wale wanaosubiri walipata matokeo ya kusifiwa katika dunia na Akhera, nao wenye uoga walipata hasara ya mawili hayo. Kwa hivyo, Mola Mtukufu akajulisha kwamba watu wenye maoni miongoni mwa Wana wa Israili na watu wa neno lenye taathira, walijadiliana kuhusu jambo la jihadi. Na wakaafikiana juu ya kwamba wamuombe Nabii wao awawekee mfalme, ili mzozo huo ukatike kwa yeye kumteua. Na upatikane utiifu kamili, na ili mwenye kusema asibaki na la kusema. Na kwamba Nabii wao huyo alichelea kwamba kuomba kwao huko ni mazungumzo matupu tu, yasiyokuwa na matendo pamoja nao. Basi wakamjibu Nabii wao kwa dhamira thabiti, na kwamba watashikamana na hilo kushikamana kukamilifu. Na kwamba kupigana vita kulikuwa ni lazima juu yao; kwani, ilikuwa ndiyo njia ya kuzirudisha maboma yao, na kurejea kwao katika makazi yao na nchi yao. Na kwamba Nabii wao aliwateulia Taluti kuwa mfalme wa kuwaongoza katika jambo hili, ambalo lazima liwe na kiongozi ambaye ni mzuri katika uongozi. Na kwamba walishangazwa na uteuzi wake wa Taluti licha ya kuwepo yule anayestahiki zaidi kwa sababu ya (heshima ya ki) nyumba na mwenye mali zaidi yake. Basi Nabii wao akawajibu: Hakika Mwenyezi Mungu amemteua juu yenu kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu alimpa ya nguvu ya elimu ya kuongoza, na nguvu za mwili, ambazo mbili hizo ndizo zana za ujasiri, na kupeana msaada, na uedeshaji mambo vizuri, na kwamba ufalme si kwa wingi wa mali, wala kwa sababu tu kwamba mwenye ufalme ni miongoni mwa wale ambao ufalme na utukufu uko katika nyumba zao. Kwani, Mwenyezi Mungu humpa ufalme wake amtakaye. Kisha Nabii huyo mtukufu hakutosheka na kuwashawishi na yale aliyoyataja kuhusu umahiri wa Taluti na kukutana kwa sifa zinazohitajika ndani yake mpaka alipowaambia: