Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 219

يَسْـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلْخَمْرِ وَٱلْمَيْسِرِ ۖ قُلْ فِيهِمَآ إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَـٰفِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَآ أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا ۗ وَيَسْـَٔلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ ٱلْعَفْوَ ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمُ ٱلْـَٔايَـٰتِ لَعَلَّكُمْ تَتَفَكَّرُونَ 219

{219} Yani wanakuuliza – ewe mtume - Waumini juu ya hukumu za mvinyo na kamari. Na vilikuwa vikitumika katika zama za kabla ya Uislamu na mwanzoni mwa Uislamu. Na ni kana kwamba kulitokea tatizo katika mawili hayo, ndio maana wakauliza juu ya hukumu yake. Kwa hivyo, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akamwamrisha Nabii wake awabainishie manufaa yake na madhara yake, ili liwe hilo ni utangulizi wa kuviharamisha na kuviacha kabisa. Basi akajulisha kwamba dhambi zake na madhara yake, na yale yanayowatokea ya kupotea kwa akili na mali, na kuzuia kumtaja Mwenyezi Mungu, na swala, na uadui, na chuki, ni makubwa kuliko yale wanayofikiri katika manufaa yake. Kama vile kuchuma mali kwa kufanya biashara ya mvinyo, na kuipata kwa kucheza kamari na kufurahisha nafsi wakati wa kuvitumia. Basi ubainisho huu ukawa wa kuzikataza nafsi dhidi yake. Kwa sababu, mtu mwenye akili timamu hupitisha yale yenye uwezekano mkubwa wa manufaa, na hujiepusha na yale yenye uwezekano mkubwa wa kudhuru. Lakini pindi walipokuwa wamevizoea, na ikawa vigumu kukataza kuviwacha kabisa katika mara ya kwanza, akatanguliza Aya hii kama utangulizi wa kuviharamisha, ambavyo alivitaja katika kauli yake. “Enyi mlioamini, hakika mvinyo, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu tu katika kazi ya shetani.” Hadi kauli yake “mmeacha?” Na hili ni kutokana na upole wake, na rehema yake, na hekima yake. Na ndiyo maana ilipoteremka, Umar Mwenyezi Mungu amwiye radhi akasema, “Tumeacha, tumeacha”. Ama mvinyo, hiyo ni kila kileo chenye kuifunika akili cha aina yoyote ile. Na ama kamari, hiyo ni kila mashindano yote ambayo ndani yake kuna malipo kutoka pande zote mbili, kama vile kete, chesi. Na kila mashindano ya kikauli au ya kivitendo kwa malipo isipokuwa mashindano ya farasi, ngamia, na mishale. Hiyo inaruhusika, kwa sababu yanasaidia katika kufanya jihadi. Ndio maana Mweka sheria akayaruhusu. (219) Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Kilichozidi mahitaji. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowabainishia Aya zake ili mpate kufikiri. Katika mambo ya dunia na mambo ya Akhera. Na hili ni swali kuhusu kiasi wanachopaswa kutoa katika mali zao. Basi Mwenyezi Mungu akawafanyia wepesi katika jambo hilo. Na akawaamrisha kutoa cha ziada ambacho ni kile chepesi katika mali zao. Ambacho hakihusiani na mahitaji yao ya kawaida na mahitaji yao ya dharura. Na hili linarudi kwa kila mtu kulingana na yeye, kuanzia tajiri, fakiri, na wa wastani, kila mmoja ana uwezo wa kutoa kile kilichozidi mahitaji yake katika mali yake, hata kama ni kwa nusu ya tende. Ndio maana Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kwamba achukue katika tabia nzuri watu. Na sadaka katika kilichozidi mahitaji, na wala asiwabebeshe kile ambacho ni kigumu kwao. Haya ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu hakutuamrisha kile alichotuamrisha kwa sababu ya haja yake kutoka kwetu. Au kutuamrisha [yale ambayo ni magumu], bali alituamrisha yale ambayo yana furaha yetu. Ambayo ni mepesi kwetu, na yenye manufaa kwetu na kwa ndugu zetu, kwa hivyo anastahiki kusifiwa kikamilifu kwa hilo. Na pale Mwenyezi Mungu alipobainisha huku kubainisha kwenye kuponya, na akawaonyesha waja siri za sheria yake. Akasema, “hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anawabainishia Aya zake.” Yani zenye kuonyesha haki, zenye kuleta elimu yenye manufaa na upambanuzi, “ili mpate kutafakari. Katika mambo ya dunia na mambo ya Akhera” yani ili mtumie fikira zenu katika siri za sheria yake, na ili mjue kuwa amri zake zina masilahi ya duniani na Akhera. Na pia ili muweze kufikiri juu ya dunia na uharaka wa kuisha kwake, ndio muikatae. Na juu ya Akhera na kubaki kwake, na kwamba ndiyo nyumba ya malipo, ndiyo muiimarishe.