An-Naml
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ٱلْغَيْبَ إِلَّا ٱللَّهُ ۚ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ 65
{65} Mwenyezi Mungu anajulisha kwamba Yeye peke yake ndiye anayejua siri za mbingu na ardhi, kama alivyosema, "Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye isipokuwa Yeye tu. Na Yeye anajua kilicho nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani isipokuwa analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha." Na kama alivyosema, "Hakika kuijua Saa (ya Kiyama) kuko kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ndiye anayeiteremsha mvua. Na anavijua vilivyo ndani ya matumbo ya uzazi..." hadi mwisho wa sura. Basi hizi ghaibu na mifano yake, Mwenyezi Mungu anazijua Yeye tu, na Malaika yeyote aliyekaribu naye wala Mtume aliyetumwa hazijui. Na ikiwa Yeye peke yake ndiye ajuaye hayo, na ambaye elimu yake inajua siri na mambo ya ndani na yaliyofichika, basi ni yeye ambaye haifai kumfanyia ibada yeyote yule isipokuwa Yeye tu. Kisha Yeye Mtukufu akajulisha juu ya udhaifu wa elimu ya hao wanaokadhibisha Akhera, huku akitoka katika kitu hadi katika kitu ambacho ni kikubwa zaidi kuliko hicho, akasema "Wala wao hawajui ni lini watafufuliwa" kutoka makaburini, basi ndiyo maana hawakujiandaa.