An-Noor
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
قُل لِّلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا۟ مِنْ أَبْصَـٰرِهِمْ وَيَحْفَظُوا۟ فُرُوجَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَزْكَىٰ لَهُمْ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرٌۢ بِمَا يَصْنَعُونَ 30
{30} Yaani, waongoze Waumini na uwaambie: Wale walio na Imani, itawaepusha na kutokea jambo linalowavuruga imani yao. "Wainamishe macho yao," wasiangalie sehemu za siri, na wanawake wa kigeni, na waabudu, ambao fitina ya uasi hugopwa kwao, na mapambo ya dunia ambayo hujaribu na kufitinisha na hupelekea katika haramu. "Na wazilinde tupu zao" kutokana na kuingilia haramu katika tupu ya mbele au nyuma au vinginevyo, na kuweza kuigusa na kuitazama. "Hili" la kuhifadhi macho na tupu zao "ni takaso bora kwao." Ni safi zaidi, ni zuri zaidi, na ni ya juu zaidi ya kukuza vitendo vyao. Na anayelinda utupu wake na kuona kwake; hutakasika kutokana na uchafu ambao wenye kufanya mambo machafu wanajichafua nao, na matendo yake hutakasika kwa sababu ya kuacha jambo lililoharamishwa ambalo nafsi inatamani na kulitaka. Yeyote anayeacha kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; Mwenyezi Mungu atamfidia kilicho bora kuliko hicho alichokiwacha, na anayeinamisha macho yake kutoka kwenye haramu, basi Mwenyezi Mungu atamng'arishia kuona kwake, na kwa sababu ikiwa mja atachunga na kuhifadhi utupu wake na macho yake kutokana na haramu na utangulizi wake pamoja na madai ya matamanio. Basi uhifadhi wake wa wengine ulikuwa wa ufasaha zaidi, na ndiyo sababu aliuita Mwenyezi Mungu hifadhi; kwani kitu kilichohifadhiwa ikiwa hatajitahidi mwenye kukihifadhi katika kukichunga na kukihifadhi, hakina bidii katika kukiangalia na kukihifadhi na kufanya kila sababu zenye kulazimu za kukihifadhi kwake; basi haihifadhiki. Vile vile, kuona (macho) na sehemu za siri ikiwa mja hatajitahidi kuzihifadhi zitamtia yeye katika majaribu na dhiki. Zingatia jinsi alivyoamrisha ulinzi wa sehemu za siri kwa ujumla, kwa sababu haijuzu katika hali yoyote ile. Na ama kuona, akasema, "wanainamisha macho yao." Alitumia kitendakazi ama neno "min" (katika), lenye kuonyesha baadhi ya jambo; kwani hakika inaruhusiwa kuangalia katika baadhi ya hali kutokana na haja. Kama vile mtazamo wa shahidi, mfanyakazi, mchumba, na mfano wa hilo. Kisha akawakumbusha kwamba anajua matendo yao, ili wajitahidi kujihifadhi kutokana na mambo ya haramu.