U bood nuxurka
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Suuradda 2

Al-Baqara

Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.

Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22

Aayadda 228

وَٱلْمُطَلَّقَـٰتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَـٰثَةَ قُرُوٓءٍ ۚ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَن يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ ٱللَّهُ فِىٓ أَرْحَامِهِنَّ إِن كُنَّ يُؤْمِنَّ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ ۚ وَبُعُولَتُهُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِى ذَٰلِكَ إِنْ أَرَادُوٓا۟ إِصْلَـٰحًا ۚ وَلَهُنَّ مِثْلُ ٱلَّذِى عَلَيْهِنَّ بِٱلْمَعْرُوفِ ۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ ۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ 228

{228} Yani wanawake ambao waume zao wamewapa talaka “wazizuie nafsi zao.” Yani wangoje na wakae eda kwa muda wa “Quruu tatu,” yani hedhi. Au tahara kulingana na tafauti ya wanazuoni juu ya kile kinachokusudiwa kwa hilo, ijapokuwa la sahihi ni kwamba Quruu ni hedhi. Na eda (muda wa kungojea) hii ina hukumu kadhaa, zikiwemo: Kuujua utupu wa tumbo la uzazi. Quruu tatu zikimrudia, basi itajulikana kuwa hakuna mimba katika tumbo lake la uzazi, kwa hivyo haitasababisha kuchanganyika kwa nasaba. Na kwa sababu hiyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu amewawajibishia kueleza “alichoumba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao ya uzazi.” Na akawaharamishia kuyaficha hayo, sawa iwe mimba au hedhi. Kwa sababu, kuficha hilo kunapelekea kwenye maovu mengi. Huko kuificha mimba kunalazimu kwamba atamnasibisha na asiyekuwa wake, kwa kumtaka na kuharakisha kuimaliza eda. Kwa hivyo, akimnasibisha na asiyekuwa baba yake, itatokea kukata ukoo na urithi, na kuwazuia naye maharimu na jamaa zake. Na huenda hata akawaoa maharimu wake, na ikatokea katika hilo kumnasibisha na asiyekuwa baba yake na kupatikana yanayofuatana na hilo kama vile kumrithi, na yeye kurithi, na kuwafanya jamaa za yule aliyenasibishwa nao kuwa jamaa zake. Na katika hilo kuna uovu na ufisadi ambao haujui isipokuwa Mola Mlezi wa waja. Na lau kuwa haingekuwa katika hilo isipokuwa kukaa kwake (mwanamke huyu mtalikiwa) pamoja na yule aliyemuoa kwa namna iliyo batili juu yake. Ambalo ndani yake kuna kusisitiza kuendelea kufanya dhambi kubwa, ambalo ni zinaa, basi hilo lingetosha kuwa uovu mkubwa. Na ama kuificha hedhi, kwa namna kwamba aliiharakisha na kusema kuwa ameipata hali ya kuwa yeye ni mwongo. Basi ndani yake kuna kuitatiza haki ya mume wake juu yake, na kuiruhusu kwa asiyekuwa mumewe, na shari inayotokana na hilo kama tulivyotaja. Na akidanganya na kusema kwamba hakuna hedhi, ili airefushe eda. Ili achukue kutoka kwake matumizi yasiyokuwa lazima juu yake. Bali hiyo ni mali haramu juu yake, iliyoharamishwa kwa njia mbili: Kwa sababu haistahiki, na kwa sababu aliyanasibisha na hukumu ya kisheria hali ya kuwa ni mwongo (katika hilo). Na huenda akamrudia mkewe baada ya kwisha kwa eda yake. Kwa hivyo unakuwa uhusianao usiokuwa wa maadili, kwa sababu yeye (mke) haruhusiwi kwake tena. Na ndio maana Mola Mtukufu akasema: “Wala sio halali kwao kuficha alichoumba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao ya uzazi, ikiwa wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho”. Na kutokea kwa tendo la kuficha kutoka kwao ni dalili ya kutomuamini kwao Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Sivyo, wangemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na wakajua kwamba watalipwa kwa matendo yao, basi kisingetokea kutoka kwao kitu katika hayo. Na katika hilo, kuna ushahidi wa kukubalika kwa habari za mwanamke, kuhusu yale anayoeleza juu ya nafsi yake; katika mambo ambayo hakuna mtu mwingine asiyekuwa yeye anayeyajua. Kama vile ujauzito, hedhi na mengineyo. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Na waume wao wana haki zaidi ya kuwarejesha katika muda huo." Yani madamu bado wamengojea katika eda hiyo au wawarudishe katika ndoa zao "kama wanataka kufanya suluhu." Yani kwa kuwataka, na kuwaweka karibu, na mapenzi. Na maana isiyokuwa ya moja kwa moja ya Aya ni kwamba, ikiwa hawataki kufanya suluhu, basi hawastahiki kuwarejesha. Kwa hivyo, haiwawii halali kuwarejesha kwa lengo la kuwadhuru, na kurefusha (muda wa) eda. Na je, analimiliki hilo (la kustahiki kumrejesha) pamoja na nia hiyo? Kuna kauli mbili: Wengi wa wanachuoni wanaona kuwa analimiliki hilo pamoja na uharamu. Lakini mtazamo sahihi ni kwamba ikiwa hataki suluhu, basi halimiliki hilo, kama inavyodhihirika katika Aya tukufu. Na hii ni hekima nyingine katika kungojea huku, ambayo ni kwamba pengine mumewe huenda akajuta kutengana naye, basi akapewa muda huu ili afikiri juu ya jambo hilo na afanye uamuzi. Na hili linaashiria kupenda kwake Mola Mtukufu kuwepo kwa ukaribu baina ya wanandoa na kuchukia kwake kutengana. Kama Nabii rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alivyosema: "Halali inayochukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni talaka." Na hili ni mahususi katika talaka anayoweza mume kumrejesha mkewe. Na ama talaka ambayo mke anaachika kabisa (yani mumewe hawezi kumrejesha isipokuwa kwa nikaa mpya), basi mume hana haki zaidi ya kumrejesha. Bali wakikubaliana kurudiana, basi ni lazima wafunge nikaa mpya yenye kujumuisha masharti yote. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema, "Nao wanawake wanayo haki sawa na ile haki iliyo juu yao kwa wema." Yani wanawake wana haki na mahitaji juu ya waume zao, sawa na zile za waume zao zilizo juu yao miongoni mwa haki za lazima na zile zinazopendekezwa. Na marejeo ya haki kati ya wanandoa ni kulingana na ada iliyo katika nchi hiyo na katika wakati huo. Kwa mfano wake mke na kwa mfano wa mume. Na hili linatofautiana kulingana na nyakati, mahali, hali, watu, na ada. Na katika hili kuna dalili ya kwamba matumizi, mavazi, kuishi pamoja kwa uzuri, makazi, na vile vile kujamiiana, hayo yote yanarejelea ada. Na huu ndio msingi ambao mkataba wa ndoa wa kawaida umejengeka juu yake. Na ama ule ambao una masharti fulani, basi itakuwa kulingana na masharti hayo, isipokuwa sharti linalohalalisha kilchoharamishwa au kuharamisha kilichohalalishwa. "Na wanaume wana daraja zaidi juu yao." Yani katika kunyanyuliwa, uongozi, na kuongezwa (mume) haki juu yake (mke), kama alivyosema Mtukufu. "Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amefadhilisha baadhi yao juu ya baadhi, na kwa kile wanachotoa katika mali zao." Na nafasi ya unabii, uhakimu, uimamu mdogo na mkubwa, na vyeo vinginevyo ni [mahsusi] kwa wanaume. Naye ana mara mbili ya waliyo nayo katika mambo mengi, kama vile mirathi na mengineyo. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima." Yani ana nguvu za ushindi na mamlaka makuu, ambaye vitu vyote vimeingia chini ya hukumu yake. Lakini yeye pamoja na nguvu zake ni mwenye hekima katika kuendesha kwake mambo. Na wanatokana na ujumla wa Aya hii wanawake wajawazito. Hao eda yao inaisha kwa kuzaa. Na wale ambao hawakuingiliwa na waume zao, kwani hawana eda. Na wajakazi, kwani eda yao ni hedhi mbili, kama ilivyo kauli ya Maswahaba, Mwenyezi Mungu awawie radhi. Na muktadha wa Aya unaashiria kwamba anayekusudiwa nayo ni mwanamke huru.