Al-Baqara
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
كَانَ ٱلنَّاسُ أُمَّةً وَٰحِدَةً فَبَعَثَ ٱللَّهُ ٱلنَّبِيِّـۧنَ مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَأَنزَلَ مَعَهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ بِٱلْحَقِّ لِيَحْكُمَ بَيْنَ ٱلنَّاسِ فِيمَا ٱخْتَلَفُوا۟ فِيهِ ۚ وَمَا ٱخْتَلَفَ فِيهِ إِلَّا ٱلَّذِينَ أُوتُوهُ مِنۢ بَعْدِ مَا جَآءَتْهُمُ ٱلْبَيِّنَـٰتُ بَغْيًۢا بَيْنَهُمْ ۖ فَهَدَى ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لِمَا ٱخْتَلَفُوا۟ فِيهِ مِنَ ٱلْحَقِّ بِإِذْنِهِۦ ۗ وَٱللَّهُ يَهْدِى مَن يَشَآءُ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ 213
{213} (Watu walikuwa) inamaanisha [walikuwa kitu kimoja kwenye uwongofu, na hilo lilikuwa kwa karne kumi baada ya Nuhu, amani iwe juu yake. Basi walipohitilafiana katika Dini, kwa hivyo kundi moja katika wao likakufuru na lile kundi lingine likabaki katika Dini, na mabishano yakatokea. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawatuma Mitume ili wahukumu kati ya viumbe na wasimamishe hoja juu yao. Na ilisemwa bali walikuwa kitu kimoja kwenye ukafiri, upotovu, na ukaidi. Hawakuwa na nuru wala imani. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akawarehemu kwa kuwatumia Mitume “wenye kupeana habari njema.” Kwa wale wanaomtii Mwenyezi Mungu kwa matunda ya utiifu kama vile riziki, nguvu katika mwili na moyo, maisha mema, na juu zaidi ya hayo, kupata radhi za Mwenyezi Mungu na Pepo. “Na waonyaji” kwa wanaomuasi Mwenyezi Mungu kwa matunda ya maasia kama vile kunyimwa riziki, udhaifu, kudunishwa, maisha finyu, na mbaya zaidi ya hayo ni ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na Moto. “Na akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki” ambayo ni habari za kweli, na maamrisho ya uadilifu. Hivyo basi, kila ambacho kitabu kimejumuisha ni haki yenye kupambanua baina ya wanaohitilafiana katika misingi na matawi. Na hili ndilo jambo la wajibu panapokuwa na hitilafu na mvutano kwamba hitilafu hiyo irejeshwe kwa Mwenyezi Mungu na kwa Mtume wake. Na lau kuwa si kwamba katika Kitabu chake na Sunnah za Mtume wake kuna upambanuzi wa mvutano, basi hangeamrisha kuvirejelea viwili hivyo. Na alipotaja neema yake kubwa kwa kuteremsha vitabu kwa Watu wa Kitabu, na hili likawa linalazimu kuafikiana kwao juu yake na kuwa kwao kitu kimoja. Kwa hivyo Mola Mtukufu akajulisha kwamba walihusudiana wao kwa wao, na mizozo na ugomvi vikatokea, na kuhitilafiana kwa wingi. Basi wakahitilafiana katika Kitabu ambacho wanapaswa wawe wa kwanza wa watu wote kuungana juu yake. Na hilo lilikuwa baada ya wao kukijua na kuwa na yakini na Aya zake zilizo wazi, na hoja zisizo na shaka, kwa hivyo wakapotea kwa hilo kupotea kwa mbali. “Ndipo Mwenyezi Mungu akawaongoa walioamini” katika Umma huu “katika yale waliyohitilafiana ndani yake ya haki.” Basi kila walichohitilafiana ndani yake watu wa Kitabu, na wakakosea humo haki na yaliyo sahihi. Mwenyezi Mungu akauongoza huu umma kuiendea haki “kwa idhini yake” yeye Mtukufu, na kuwarahisishia kwake na rehema zake. “Na Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye kwenye Njia iliyonyooka.” Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu akawalingania viumbe wote kwenye njia iliyonyooka kwa sababu ya uadilifu wake, na kusimamisha hoja juu ya viumbe, wasije wakasema: “Hatukujiwa na mpeanaji wa habari njema yeyote wala waonyaji”. Na akaongoa - kwa fadhila zake, rehema zake, usaidizi wake, na upole wake - amtakaye katika waja wake. Na hii ndiyo fadhila yake na wema wake, na huo ndio uadilifu wake na hekima yake Mwenye baraka, Mtukufu.