U bood nuxurka
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Suuradda 2

Al-Baqara

Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.

Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22

Aayadda 144

قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِى ٱلسَّمَآءِ ۖ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَىٰهَا ۚ فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ ۚ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّوا۟ وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُۥ ۗ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ لَيَعْلَمُونَ أَنَّهُ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَـٰفِلٍ عَمَّا يَعْمَلُونَ 144

(144) Mwenyezi Mungu anamwambia Nabii wake: ”Kwa yakini, tuliona unavyougeuza geuza uso wako mbinguni.” Yani kuangalia katika pande zote kwa wingi akiwa na shauku na kungojea wahyi uteremke wenye kuamrisha kuielekea Al-Ka'aba. Na alisema “uso wako”, wala hakusema ‘macho yako’, kwa sababu ya hamu yake kubwa, na kwa sababu kugeuza uso kunalazimu kugeuza macho. “Basi tutakuelekeza kwenye Kibla unachokiridhia” yani ukipendacho, nayo ni Al-Ka'aba. Na katika hili, kuna kubainisha fadhila yake na heshima yake (Mtume) rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anaharakisha kumridhisha. Kisha akamwambia waziwazi kuielekea, akasema: “Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu.” Na Al-Wajh ni upande wa mbele wa mwili wa mwanadamu. “Na popote mnapokuwa,” yani kwenye nchi kavu na baharini, mashariki na magharibi, kusini na kaskazini, “zielekezeni nyuso zenu upande wake” yani huo mwelekeo wake. Na ndani yake, kuna sharti la kuielekea Al-Ka'aba katika swala zote za faradhi na za sunna. Na kwamba ikiwezekana kuielekea yenyewe, ni sawa, vinginevyo, inatosheleza kuelekea upande wake na mwelekeo wake. Na kwamba kugeuka kwa mwili wote kunabatilisha swala. Kwa sababu, kuamrisha jambo fulani, ni kukataza kinyume chake. Na pale Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja - katika yaliyotangulia - wale waliopinga hilo miongoni mwa Watu wa Kitabu na wengineo, na akataja jibu alilowajibu kwalo, alitaja hapa kwamba Watu wa Kitabu na wenye elimu miongoni mwao wanajua kwamba wewe katika hilo upo kwenye haki iliyo wazi, kwa sababu ya yale wanayoyakuta katika vitabu vyao. Kwa hivyo, wanapinga kwa ukaidi na kwa dhuluma tu. Basi ikiwa wanajua kosa lao, wewe usilijali hilo. Kwani, mwanadamu huwa na dhiki kwa sababu ya upinzani wa mwenye kumpinga ikiwa jambo hilo silo lenye uwazi, na ikawa inawezekana kwamba (mpinzani) yuko sahihi. Lakini ikiwa ana yakini kwamba usahihi na ukweli uko pamoja na anayepingwa, na kwamba mwenye kupinga ni mkaidi tu na anaujua ubatilifu wa kauli yake, basi hilo si mahali pa kujali. Bali anangojewa mwenye kupinga kupata adhabu ya kidunia na ya Akhera. Kwa hivyo, ndio maana Mola Mtukufu akasema: “Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale wanayoyatenda”. Bali anawahifadhia matendo yao, na atawalipa juu yake. Na ndani yake kuna onyo la adhabu kwa wanaopinga, na kupeana faraja kwa Waumini.