Yusuf
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
وَمَآ أُبَرِّئُ نَفْسِىٓ ۚ إِنَّ ٱلنَّفْسَ لَأَمَّارَةٌۢ بِٱلسُّوٓءِ إِلَّا مَا رَحِمَ رَبِّىٓ ۚ إِنَّ رَبِّى غَفُورٌ رَّحِيمٌ 53
53. Kisha pindi maneno hayo yalipokuwa na aina fulani ya kujitakasa nafsi, na kwamba hakufanya dhambi yoyote kuhusiana na Yusuf, akarekebisha hilo, akasema, “Nami sijitoi lawamani.” Yaani, sijitoi katika kule kumtaka kimapenzi, na azimio yangu kubwa juu ya hilo, na kuwania kwangu kukubwa juu yake, na njama zangu katika hilo. "Kwa hakika nafsi ni yenye kuamrisha mno mabaya.” Yaani, uchafu na dhambi nyingine zote. Kwa maana nafsi ni kipando cha Shetani, na kupitia hiyo ndiyo anamuingilia mwanadamu "isipokuwa yule aliyerehemewa na Mola wangu Mlezi.” Kwa hivyo akamuepusha na nafsi yake yenye kuamrisha mabaya mpaka nafsi yake ikawa tulivu kwa Mola wake Mlezi, na yenye kufuata mwenye kulingania kwenye uwongofu, na kumuasi mwenye kulingania kwenye maangamizo. Na hilo halitoki kwa nafsi yenyewe, bali ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema yake kwa mja wake. "Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu mno, Mwenye kurehemu sana.” Yaani, Yeye ni Mwenye kuwasamehe mno kwa yule anayethubutu kufanya madhambi na maasia akitubu na kurudi kwake, na ni Mwenye kurehemu sana kwa kuitikia toba yake na kumuwezesha kufanya matendo mema. Na hili ndilo lililo sahihi, kwamba haya ni katika maneno ya mke wa mheshimiwa huyo, na si katika maneno ya Yusuf. Kwa maana, muktadha uko katika maneno yake, naye Yusuf wakati huo alikuwa bado yuko gerezani kabla ya kufika hapo.