Yusuf
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
وَجَآءُو عَلَىٰ قَمِيصِهِۦ بِدَمٍ كَذِبٍ ۚ قَالَ بَلْ سَوَّلَتْ لَكُمْ أَنفُسُكُمْ أَمْرًا ۖ فَصَبْرٌ جَمِيلٌ ۖ وَٱللَّهُ ٱلْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ 18
{18} "Na" katika yale waliyoyasisitiza kwayo kauli yao hiyo ni kwamba, "walikuja na shati lake likiwa lina damu ya uongo." Wakadai kuwa, ni damu ya Yusuf mbwa mwitu alipomla, lakini baba yao hakuwaamini kwa hilo, na "akasema, bali nafsi zenu zimewashawishi kutenda kitendo." Yaani, nafsi zenu ziliwapambia jambo baya ili kunitenganisha naye. Kwa sababu aliona baadhi ya ushahidi na hali mbalimbali, na pia katika ndoto ya Yusuf ambayo alimsimulia ambayo ilimuonyesha kile alichosema. "Lakini subira ni njema; na Mwenyezi Mungu ndiye wa kuombwa msaada kwa haya mnayoyaeleza." Yaani, ama mimi nitafanya hima katika kufanya kazi yangu, nayo ni kwamba nitajitahidi kujisubirisha katika majaribio haya subira nzuri iliyosalimika kutokana na hasira na kuwalalamikia viumbe, na nitatafuta msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika hili, siyo kwa nguvu zangu na uwezo wangu. Basi alijiahidi jambo hili, na akamlalamikia Muumba wake kwa kauli yake: "Hakika mimi ninamlalamikia shida yangu na huzuni wangu Mwenyezi Mungu tu." Kwa sababu kumlalamikia Muumba hakupingani na subira nzuri. Kwa sababu nabii anapoahidi, anatimiza.