Al-An'aam
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
قُل لَّآ أَقُولُ لَكُمْ عِندِى خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعْلَمُ ٱلْغَيْبَ وَلَآ أَقُولُ لَكُمْ إِنِّى مَلَكٌ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَىَّ ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِى ٱلْأَعْمَىٰ وَٱلْبَصِيرُ ۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ 50
{50} Yeye Mtukufu anamwambia Nabii wake – rehema na amani ziwe juu yake – juu ya wale waliompendekezea Aya mbalimbali, au wale wanaomwambia: Wewe hakika unatuita tu ili tukufanye wewe kuwa mungu pamoja na Mwenyezi Mungu. "Mimi siwaambii kuwa ninazo hazina za Mwenyezi Mungu;" yaani, funguo za riziki yake na rehema yake, "Wala sijui ghaibu." Lakini hayo yote yako kwa Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye rehema ambayo anawafungulia watu, hapana wa kuizuia. Na kile anachokizuia, hapana wa kukiachilia isipokuwa Yeye tu. Na Yeye peke yake ndiye anayejua ghaibu na yanayoshuhudiwa. Kwa hivyo, hamdhihirishii yeyote ghaibu yake isipokuwa yule anayemridhia miongoni mwa Mitume. "Wala siwaambii kuwa mimi ni Malaika" ili niwe mwenye kutekeleza amri yangu, mwenye nguvu, wala sidai kuwa juu ya daraja yangu ambayo Mwenyezi Mungu ameniteremsha kwayo. "Mimi sifuati isipokuwa yanayofunuliwa kwangu;" yaani, hiki ndicho kikomo changu na mwisho wa jambo langu, na la juu lake zaidi. Mimi sifuati isipokuwa yanayofunuliwa kwangu, kwa hivyo ninayafanyia kazi mimi mwenyewe, na ninawalingania viumbe vyote kufanya hivyo. Kwa hivyo ikiwa daraja yangu inajulikana; basi ni kwa kitu gani mtafutaji anatafuta kwangu, au anataka kutoka kwangu jambo ambalo silidai? Na je ,mtu anapaswa kulazimishwa kitu kingine zaidi ya yale aliyoyakusudia? Na ni kwa kitu gani nikiwalingania kwa yale niliyoteremshiwa, mnanilazimisha kwamba mimi ninajidaisha mwenyewe isiyokuwa daraja yangu? Na je, hii si isipokuwa dhuluma kutoka kwenu, na ukaidi na uasi? Waambie katika kubainisha tafauti baina ya mwenye kukubali wito wangu na akafuata yale niliyoteremshiwa, na yule asiyekuwa hivyo. "Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na mwenye kuona. Basi hamfikiri?" Kwa hivyo mkaviteremsha vitu katika daraja zake, na mchague kile kinachostahili zaidi kuchaguliwa na kupendelewa.