Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Mujaadila
Surah 58

Al-Mujaadila

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 8–9

أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ نُهُوا۟ عَنِ ٱلنَّجْوَىٰ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا نُهُوا۟ عَنْهُ وَيَتَنَـٰجَوْنَ بِٱلْإِثْمِ وَٱلْعُدْوَٰنِ وَمَعْصِيَتِ ٱلرَّسُولِ وَإِذَا جَآءُوكَ حَيَّوْكَ بِمَا لَمْ يُحَيِّكَ بِهِ ٱللَّهُ وَيَقُولُونَ فِىٓ أَنفُسِهِمْ لَوْلَا يُعَذِّبُنَا ٱللَّهُ بِمَا نَقُولُ ۚ حَسْبُهُمْ جَهَنَّمُ يَصْلَوْنَهَا ۖ فَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ 8 يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا تَنَـٰجَيْتُمْ فَلَا تَتَنَـٰجَوْا۟ بِٱلْإِثْمِ وَٱلْعُدْوَٰنِ وَمَعْصِيَتِ ٱلرَّسُولِ وَتَنَـٰجَوْا۟ بِٱلْبِرِّ وَٱلتَّقْوَىٰ ۖ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ٱلَّذِىٓ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ 9

Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema:

{8 - 9} Kunong’onezana kunaweza kuwa kwa heri au kwa uovu. Basi Mwenyezi Mungu akawaamrisha Waumini kunong’onezana kwa wema. Nao ni jina linalojumuisha kila heri, utiifu, na kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake, na ucha Mungu. Nao hapa ni jina linalijumuisha kuacha vitendo na dhambi yote yaliyoharamishwa. Kwa hivyo, Muumini anatekeleza amri hii ya kimungu. Hutamkuta akinong’ona wala akizungumza ila kwa yale yanayomuweka karibu na Mwenyezi Mungu na yanamweka mbali na ghadhabu yake. Naye mwovu, anazembea katika kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na ananong’ona kwa dhambi, uadui na kumuasi Mtume. Kama wanafiki ambao hii ndiyo ada yao na hali yao wanapoamiliana na Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: “Na wakikujia, hukuamkua sivyo anavyokuamkua Mwenyezi Mungu.” Yaani wanafanya adabu mbaya katika kukuamkua. “Na husema katika nafsi zao” wakisema: 'Mbona Mwenyezi hatuadhibu kwa haya tuyasemayo?' Maana yake ni kuwa wanaona kwamba hilo ni dogo, na wanalitumia kutoharakishiwa adhabu kuwa ni ushahidi kwamba wanayoyasema si haramu. Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema kwamba Yeye hupeana muda na wala hapuuzi: “Basi Jahannamu itawatosha; wataingia humo! Na hayo ndiyo marejeo maovu yaliyoje!” Yaani, Jahannamu itawatosha, ambayo imewakusanyia adhabu na dhiki zote. Itawazingira na kuwatesa kwayo. Basi hayo ndiyo marejeo maovu yaliyoje! Na hawa waliotajwa ima ni watu kutoka kwa wanafiki wenye kuonesha imani na wanamwongelesha Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kwa maneno haya ambayo kwayo wanawafanya watu waamini kuwa wana nia njema, lakini ni waongo katika hilo. Au ni watu miongoni mwa Watu wa Kitabu ambao wanapomsalimu Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - wanasema: ‘Saam alaikum, ewe Muhammad (yaani, tunakuombea kifo).