Al-Maaida
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
يَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ قَدْ جَآءَكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ ٱلْكِتَـٰبِ وَيَعْفُوا۟ عَن كَثِيرٍ ۚ قَدْ جَآءَكُم مِّنَ ٱللَّهِ نُورٌ وَكِتَـٰبٌ مُّبِينٌ 15
{15} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja yale aliyochukua kwa Watu wa Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Manasara, na kwamba waliyavunja hayo isipokuwa wachache miongoni mwao, akawaamrisha wote kumwamini Muhammad – rehema na amani ziwe juu yake – na akatumia dhidi yao hoja ya uhakika yenye kuashiria usahihi wa unabii wake. Nayo ni kuwa anawabainishia mengi katika yale wanayowaficha watu mpaka watu wa kawaida miongoni mwa watu mila yao. Basi ikiwa wao ndio waliorejelewa katika elimu na hakuna aliyekuwa na elimu wakati huo isipokuwa yale waliyo nayo, basi Mwenye bidii katika elimu hana njia ya kuipata isipokuwa kutoka kwao. Kwa hivyo Kuja kwa Mtume – Rehema na Amani zimshukie – na hii Qur-ani tukufu, ambayo kwayo alibainisha yale waliyokuwa wakiyaficha wao kwa wao, na ilhali yeye hajui kusoma wala kuandika, ni katika ishara zilizo wazi kabisa za uhakika wa utume wake. Na hayo ni kama vile sifa za Muhammad katika vitabu vyao, na kuwepo kwa bishara juu yake katika vitabu vyao, na kuibainisha Aya ya kupigwa mawe (kwa mzinzi)... na mfano wa hayo. "Na anayaacha mengi," yaani, anaacha kueleza kile ambacho hekima haihitaji yaelezwe. "Bila shaka imekwisha wajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu nuru." Nayo ni Qur-ani ambayo inatumika kama mwangaza katika giza mbalimbali za ujinga na upofu wa upotovu. "Na Kitabu kilicho wazi" kwa kila wanachokihitajia viumbe miongoni mwa mambo ya dini yao na ya dunia yao kama vile kumjua Mwenyezi Mungu, na majina Yake, na Sifa Zake, na vitendo Vyake, na miongoni mwa kuzijua hukumu Zake za kisheria na hukumu Zake za adhabu.