Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Naml
Surah 27

An-Naml

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 20

وَتَفَقَّدَ ٱلطَّيْرَ فَقَالَ مَا لِىَ لَآ أَرَى ٱلْهُدْهُدَ أَمْ كَانَ مِنَ ٱلْغَآئِبِينَ 20

{20} Kisha akataja mfano mwingine wa kuongea kwake na ndege, na akasema: "Na akawakagua ndege." Na hili lilionyesha ukamilifu wa azimio lake na mpangilio wake mzuri wa askari wake, na kuendesha kwake mwenyewe mambo madogo na makubwa kiasi kwamba hakulipuuza jambo hili, ambalo ni kuwakagua ndege, na kuangalia ikiwa wote wapo au kuna yule ambaye hayupo miongoni mwao? Na hii ndiyo maana ya aya hii. Hakufanya kitu yule ambaye alisema kuwa: aliwakagua ndege ili amuone hud-Hud ili amuonyeshe umbali na ukaribu wa maji. Pia walidai kwamba Hud-Hud huyo alikuwa na uwezo wa kuona maji chini ya ardhi ya chini mno. Kauli hii haiashiriwi na ushahidi wowote, bali ushahidi wa kiakili na wa kimatamshi unaonyesha ubatili wake: Ama wa kiakili ni kwamba ilishajulikana kwa mazoea, majaribio, na kuangalia kwamba wanyama hawa wote hakuna yeyote miongoni mwao ambaye ana uwezo wa kuona umbali huu usiokuwa wa kawaida, na kuona maji chini ya ardhi ya mbali. Na ikiwa ingeliwa hivyo, basi Mwenyezi Mungu angelitaja, kwa sababu ni miongoni mwa ishara kubwa zaidi. Na ama ushahidi wa kimatamshi, ikiwa ingekusudiwa maana hii, basi angesema: Alimtafuta Hud-Hud ili amtazamie maji, na alipomkosa, akasema hayo aliyosema. Au: Alimtafuta Hud-Hud, au mfano wa hayo. Badala yake, aliwakagua ndege ili ajue ni nani wao yupo na ni nani asiyekuwapo na uwepo wao katika sehemu na nafasi alizowaweka. Pia, Suleiman, amani ya Mwenyezi Mungu imshukie, hakuhitaji wala hakuwa na dharura ya maji ndiyo ahitaji uhandisi wa Hud-Hud. Kwani alikuwa na mashetani na mapepo wakubwa ambao walikuwa na uwezo wa kumchimbia maji, na hata yangefikia kina kirefu namna gani. Na Mwenyezi Mungu alimtiishia upepo, ambao safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Basi anawezaje pamoja na hayo kumhitaji Hud-Hud? Tafsiri hizi, ambazo zipo na ni maarufu katika maneno ambayo hayajulikani maneno mengine yasiyokuwa hayo yanasimuliwa kutoka kwa Banu Israili, lakini wenye kusimuliwa wanaghafilika kuona kwamba yanapingana na maana sahihi. Nayo yanaendelea kusimuliwa yakinukuliwa na watu wa kisasa kwa hoja ya kukubali maendelea ya kisasa ili idhaniwe kwamba ni haki; kwa hivyo yanaingia maneno mabaya katika tafsiri kwa njia hii. Lakini mtu mwenye akili nzuri, mwerevu anajua kwamba Qur-ani hii tukufu ya Kiarabu yenye kubainisha ambayo kwayo Mwenyezi Mungu aliwaongelesha viumbe wote, wajuao na wasiojua, na akawaamuru kutafakari maana yake na kuyatumia katika matamshi yake ya Kiarabu yanayojulikana maana zake ambazo Waarabu wenyewe hawakosi kuyajua. Na anapopata maneno yaliyonukuliwa si kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, anayarudisha kwa asili hii. Yakikubaliana nayo, anayakubali; kwa sababu matamshi yake yanayaashiria hayo. Na ikiwa yatahalifiana nayo katika matamshi na kwa maana, au katika matamshi au maana, anayarudisha na kuwa na yakini kwamba ni batili; kwa sababu ana asili inayojulikana inayopingana na nayo, ambayo ni yale anayoyajua katika maana za maneno na yale ambayo hayo maneno yanayaashiria. Na ushahidi wa aya hii ni juu ya suala kwamba Suleiman, amani iwe juu yake, katika kuwakagua ndege na kutompata Hud-Hud kunaonyesha ukamilifu wa azimio yake na uendeshaji wake mzuri wa ufalme wake yeye mwenyewe na ukamilifu wa akili yake nzuri, kiasi kwamba akamtafuta ndege huyu mdogo, "Imekuwaje, mbona simwoni Hud-hud, au amekuwa miongoni mwa wasiokuwepo?" Yaani: Je, kushindwa kwangu kumuona ni kwa sababu siwezi kumtambua kwa sababu amejificha miongoni mwa makundi haya mengi? Au ni kweli kwamba hakuwepo bila ya idhini yangu wala amri yangu?