Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Surah 2

Al-Baqara

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 260

وَإِذْ قَالَ إِبْرَٰهِـۧمُ رَبِّ أَرِنِى كَيْفَ تُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰ ۖ قَالَ أَوَلَمْ تُؤْمِن ۖ قَالَ بَلَىٰ وَلَـٰكِن لِّيَطْمَئِنَّ قَلْبِى ۖ قَالَ فَخُذْ أَرْبَعَةً مِّنَ ٱلطَّيْرِ فَصُرْهُنَّ إِلَيْكَ ثُمَّ ٱجْعَلْ عَلَىٰ كُلِّ جَبَلٍ مِّنْهُنَّ جُزْءًا ثُمَّ ٱدْعُهُنَّ يَأْتِينَكَ سَعْيًا ۚ وَٱعْلَمْ أَنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ 260

{260} Na ama ule ushahidi mwingine, basi, Ibrahim alisema akimwomba Mwenyezi Mungu amwonyeshe jinsi anavyowafufua wafu. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamwambia, “kwani huamini?” Ili amuondolee mwandani wake fikira potofu. “Akasema” Ibrahim, “Hasha!” ewe Mola mlezi, nilikwisha amini kuwa wewe ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu, na kwamba unahuisha wafu na utawalipa waja. Lakini ninataka moyo wangu utulie na ufikie kiwango cha yakini. Basi Mwenyezi Mungu akaitikia dua yake kwa ajili ya kumtukuza na kuwafanyia rehema waja wake. “Akasema: Basi wachukue wanne katika ndege” lakini hakubainisha ni ndege wagani hao, kwani ishara hiyo inaweza tokea kwa aina yoyote ile kati yake. Na hilo ndilo lililokusudiwa “Na uwazoeshe kwako” yani wawake karibu sana na wewe, kisha wachinje na uwakatekate. “Kisha weka juu ya kila kilima sehemu katika hao, kisha waite, watakujia mbio. Na ujue kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.” Basi akafanya hivyo, na akatenganisha sehemu zao juu ya milima iliyomzunguka na akawaita kwa majina yao, nao wakamjia, yani mbio. Kwa sababu neno ‘assa’y’ linamaanisha kwenda mbio. Na haikukusudiwa kwamba walimjia kwa miguu yao. Bali walikuja kwa kupaa wakiwa katika hali ya ukamilifu zaidi ya uhai. Na aliwachagua ndege hususan kwa ajili ya hilo, kwa sababu kuhuishwa kwao ni kukamilifu zaidi kuko wazi zaidi kuliko wengineo. Na pia aliondoa katika hilo kila fikira mbovu ambayo huenda ikaingia ndani ya nafsi zinazofuata batili. Na aliwafanya kuwa wanne tofauti tofauti, na akawakatakata wote. Na akawaweka juu ya vilele vya milima, ili jambo hilo liwe dhahiri lenye kuonekana hadharani, anaweza kulitazama aliye karibu na wa mbali. Na kwamba aliwaweka mbali sana na yeye mwenyewe ili isifikiriwe kwamba alikuwa anafanya hila. Na pia alimwamrisha awaite, basi wakaja mbio. Kwa hivyo, ikawa ishara hii ndio ushahidi mkubwa mno juu ya ukamilifu wa Nguvu ya Mwenyezi Mungu na hekima yake. Na ndani yake kuna tanbihi kwamba ufufuo, ndani yake unawadhihirishia waja ukamilifu wa Nguvu za Mwenyezi Mungu, na hekima yake. Na ukuu wake, na upana wa mamlaka yake, na ukamilifu wa uadilifu wake na fadhila yake.