Al-Baqara
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
أَوْ كَٱلَّذِى مَرَّ عَلَىٰ قَرْيَةٍ وَهِىَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا قَالَ أَنَّىٰ يُحْىِۦ هَـٰذِهِ ٱللَّهُ بَعْدَ مَوْتِهَا ۖ فَأَمَاتَهُ ٱللَّهُ مِا۟ئَةَ عَامٍ ثُمَّ بَعَثَهُۥ ۖ قَالَ كَمْ لَبِثْتَ ۖ قَالَ لَبِثْتُ يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ ۖ قَالَ بَل لَّبِثْتَ مِا۟ئَةَ عَامٍ فَٱنظُرْ إِلَىٰ طَعَامِكَ وَشَرَابِكَ لَمْ يَتَسَنَّهْ ۖ وَٱنظُرْ إِلَىٰ حِمَارِكَ وَلِنَجْعَلَكَ ءَايَةً لِّلنَّاسِ ۖ وَٱنظُرْ إِلَى ٱلْعِظَامِ كَيْفَ نُنشِزُهَا ثُمَّ نَكْسُوهَا لَحْمًا ۚ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُۥ قَالَ أَعْلَمُ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ 259
{259} Hizi ni dalili mbili kubwa na zinazoonekana katika dunia hii kabla ya Akhera juu ya ufufuo na malipo. Moja, Mwenyezi Mungu aliifanya kwa mkono wa mwanamume aliyekuwa na shaka juu ya ufufuo, nayo ndiyo kauli sahihi kulingana na inavyoonyesha Aya tukufu juu yake. Nayo nyingine ilikuwa juu ya mkono wa rafiki mwandani wake Ibrahim, kama alivyoifanyisha dalili ya Tauhid iliyopita hapo awali juu ya mkono wake. Mtu mwanamume alipita karibu na kijiji kilichokuwa kimeharibiwa kuharibika kukubwa kikatokomea kabisa. Watu wake walikuwa wamekwisha kufa na mijengo yake ikawa imekwisha haribika. Kwa hivyo, akasema kwa namna ya shaka na kuona kwamba hilo haliwezekani. "Vipi Mwenyezi Mungu ataufufua mji huu baada ya kufa kwake?" Yani, hilo liko mbali hali ya kuwa uko (mji huu) katika hali hii, akimaanisha miji mingine mfano wake kulingana na kile kilichokuwa ndani ya moyo wake saa ile. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akataka kumrehemu na kuwarehemu watu. Kwani Mwenyezi Mungu alimfisha kwa miaka mia moja, na alikuwa na punda pamoja naye, kwa hivyo akamfisha pamoja naye. Na alikuwa na chakula na kinywaji pamoja naye. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akaviacha vilivyokuwa kwa mida yote hii mirefu. Na miaka hiyo mia moja ilipopita, Mwenyezi Mungu akamhuisha na akasema: "Je umekaa muda gani? Akasema: (Labda) nimekaa siku moja au sehemu ya siku." Na hayo ni kulingana na vile alivyodhania. Basi Mwenyezi Mungu akasema, "Bali umekaa miaka mia moja." Na lililo dhahiri zaidi ni kwamba majibu haya yalikuwa kutoka kwa baadhi ya manabii watukufu. Na katika utimilifu wa rehema ya Mwenyezi Mungu kwake na kwa watu ni kwamba alimwonyesha Aya kwa macho yake ili apate kuridhika nayo. Na baada ya kujua kuwa alikufa, kisha Mwenyezi Mungu akamfufua, akaambiwa: Angalia, "chakula chako na kinywaji chako, havikuharibika!" Yani havikubadilika katika mida hii mirefu. Na hayo ni katika dalili za uwezo wa Mwenyezi Mungu. Kwani chakula na kinywaji, hasa walichokitaja wafasiri kuwa matunda na juisi havikai muda isipokuwa vinakuwa vimeshabadilika. Na Mwenyezi Mungu huyu alivihifadhi kwa muda wa miaka mia moja. Na akaambiwa, "Mwangalie punda wako." Tazama! Alikuwa amekwisha katikakatika na akaachanika ameshakuwa mifupa iliyooza. "Na iangalie mifupa yake hii jinsi tunavyoinyanyua." Yani tunavyoiinua baadhi yake juu ya nyingine na kuunganisha baadhi yake juu ya nyingine baada ya kutawanyika na kuachanika. "Kisha tuivishe" baada ya kushikana "nyama." Kisha tunarudisha uhai ndani yake. "Basi yalipombainikia" kwa mtazamo wa macho usiokubali shaka yoyote kwa namna yoyote; "ninajua kwamba kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu." Kwa hivyo akakiri uwezo wa Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu, na akawa ishara kwa watu. Kwa sababu walijua kifo chake na kifo cha punda wake, na walikijua kisa chake, kisha wakashuhudia ishara hii kubwa. Na hayo ndiyo yaliyo sahihi kuhusu mwanamume huyu. Na ama kauli ya wengi miongoni mwa wafasiri kuwa, mwanamume huyu ni Muumini au Nabii miongoni mwa Manabii. Ima Ezra au mtu mwingine, na kwamba kauli yake: "Vipi Mwenyezi Mungu ataufufua mji huu baada ya kufa kwake?" Inamaanisha: Vipi kijiji hiki kitaimarishwa upya baada ya kuharibika. Na kwamba Mwenyezi Mungu alimfisha ili amwonyeshe kile atakachorudishia kijiji hiki cha kukiimarisha kwa viumbe. Na kwamba kiliimarishwa katika muda huu na watu wakakirudia, na kikawa kimeimarika baada ya kuwa kimeharibika. Hili haliashiriwi na matamshi ya aya, bali yanalipinga, na wala maana yake hayaliashirii. Ni ishara gani na uthibitisho gani uliopo katika miji iliyoharibika kurudi ikaimarika, ilhali hiki hakijaacha kushuhudia ujenzi wa vijiji na makazi; kisha kinaharibika mara ya pili? Lakini ishara kubwa ni katika ufufuo wake baada ya kufa kwake, na ufufuo wa punda wake. Na kukihifadhi chakula chake na kinywaji chake ambavyo havikuoza wala kubadilika. Kisha kauli yake: "Na ilipombainikia" ni wazi kwamba, haikumbainikia isipokuwa mpaka baada ya kuona hali hii inayoashiria ukamilifu wa uwezo wake kwa macho.