Al-Israa
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
وَإِن كَادُوا۟ لَيَسْتَفِزُّونَكَ مِنَ ٱلْأَرْضِ لِيُخْرِجُوكَ مِنْهَا ۖ وَإِذًا لَّا يَلْبَثُونَ خِلَـٰفَكَ إِلَّا قَلِيلًا 76 سُنَّةَ مَن قَدْ أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ مِن رُّسُلِنَا ۖ وَلَا تَجِدُ لِسُنَّتِنَا تَحْوِيلًا 77
{76 - 77} "Na walitaka kukukera ili wakutoe nchini." Yaani, kwa sababu ya kuchukia kwao kuishi kwako pamoja nao, walikuwa karibu zaidi kukutoa nchini na kukuhamisha kutoka humo. Na kama wangefanya hivyo, wasingalikaa humo baada yako isipokuwa muda mfupi tu kabla ya kujiwa na adhabu, kama ilivyo desturi ya Mwenyezi Mungu ambayo haigeuki wala haibadiliki katika umma zote, kila umma uliomkadhibisha Mtume wake na ukamfukuza, Mwenyezi Mungu aliwaharakishia adhabu. Na wale waliokufuru walipompangia njama na wakamfukuza, hawakukaa isipokuwa muda mfupi tu kabla ya Mwenyezi Mungu kuwaadhibu huko Badr, na akawaua wakuu wao, na akatawanya umoja wao. Basi sifa njema zote ni zake. Na katika aya hizi, kuna ushahidi juu ya uhitaji mkubwa zaidi wa mja juu ya kuimarishwa na Mwenyezi Mungu, na kwamba [anapaswa] kuendelea kumuomba Mola wake Mlezi kwamba amuimarishe katika imani, akijitahidi kufanya kila sababu inayofikisha katika hilo. Kwa sababu Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – pamoja na kwamba yeye ndiye mkamilifu zaidi wa viumbe - Mwenyezi Mungu alimwambia, "na lau kuwa hatukukuweka imara, ungelikaribia kuwaegemea kidogo." Basi vipi kuhusu watu wengine? Na ndani yake pia Mwenyezi Mungu anamkumbusha Mtume wake neema yake juu yake na humkinga kwake kutokana na maovu. Kwa hivyo, hilo likaashiria kuwa Mwenyezi Mungu anapenda kwamba waja wake wawe na habari ya neema zake juu yao pindi zinapopatikana sababu za maovu kwa kutafuta kinga kutoka kwake na kukaa imara katika imani. Na ndani yake kuna kwamba kulingana na cheo cha mja na wingi wa kumshukia neema juu yake kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ndiyo dhambi zake zinakuwa kubwa na uhalifu wake unaongezeka maradufu ikiwa akifanya anacholaumiwa juu yake. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alimkumbusha Mtume wake kwamba kama angefanya hivyo - na aepushwe na hilo - kwa kwa kauli yake, “bila ya shaka, tungelikuonjesha adhabu maradufu ya uhai, na adhabu maradufu ya kifo. Kisha usingepata yeyote wa kukunusuru kutokana nasi.” Na ndani yake kuna kwamba Mwenyezi Mungu akitaka kuuangamiza umma, uhalifu wake huongezeka na kuwa mkubwa zaidi na zaidi, kwa hivyo ukawa unastahiki neno la adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kwa hivyo anauadhibu kama ilivyo desturi yake katika umma zote wanapomfukuza Mtume wao.