Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nahl
Surah 16

An-Nahl

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 125

ٱدْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِٱلْحِكْمَةِ وَٱلْمَوْعِظَةِ ٱلْحَسَنَةِ ۖ وَجَـٰدِلْهُم بِٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِٱلْمُهْتَدِينَ 125

{125} Yaani, na kuwe kulingania kwako viumbe, Mwislamu wao na kafiri wao katika njia ya Mola wako Mlezi, iliyonyooka inayojumuisha elimu yenye manufaa na matendo mema "kwa hekima." Yaani, kila mtu kulingana na hali yake, ufahamu wake , kukubali kwake na kufuata kwake. Na katika hekima ni kulingania kwa elimu si kwa ujinga, na kuanza na kilicho muhimu zaidi kisha kilicho muhimu zaidi, na kilicho karibu zaidi na akili na ufahamu, kile kinachokubalika zaidi kikamilifu, na kwa upole na ulaini. Kwa hivyo, akifuata kwa sababu ya hekima, basi ni sawa. Vinginevyo, na asonge naye katika kumlingania kwa mawaidha mazuri, nayo ni kuamrisha na kukataza yanayofungamana mawili hayo na kutia moyo na kutishia. Ima kwa kutaja manufaa yaliyomo katika maamrisho na kuyahesabu, na makatazo na madhara yake na kuyahesabu. Au ima kwa kutaja kukirimiwa kwa yule aliyesimamisha dini ya Mwenyezi Mungu, na kudunishwa kwa yule ambaye hakuisimamisha. Au kwa kutaja yale ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia watiifu miongoni mwa malipo ya haraka na ya baadaye na yale aliyowaandalia waasi miongoni mwa adhabu ya haraka na ya baadaye. Na kama yule anayelinganiwa anaona kwamba yeye ndiye aliye katika haki, au kwamba analingania kwenye batili, basi huyo atajadiliwa kwa njia iliyo nzuri zaidi. Nazo ni njia ambazo zitachangia zaidi aitikie kiakili na kimaandiko matakatifu. Na katika hayo ni kumuekea hoja kwa ushahidi ule ule aliokuwa akiuitakidi kwani hilo ni karibu zaidi katika kufikia makusudio, na kwamba mjadala huo usizae mzozo au kutukanana utakaopoteza makusudio yake wala haitapatikana faida yake. Bali na yawe makusudio yake ni kuongoza viumbe kwenye haki na siyo kushindana, na mifano yake. Na kauli yake, "Hakika Mola wako Mlezi ndiye anayemjua zaidi yule aliyeipotea Njia yake." Alijua sababu iliyompoteza, na alijua matendo yake yaliyotokana na upotovu wake, na atamlipa kwa hayo. "Na Yeye ndiye anayewajua zaidi wale walioongoka." Alijua kwamba wao wanafailia kuongoka, kwa hivyo akawaongoa, kisha akawaneemesha, kwa hivyo akawachagua.