Al-Muminoon
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
أَيَعِدُكُمْ أَنَّكُمْ إِذَا مِتُّمْ وَكُنتُمْ تُرَابًا وَعِظَـٰمًا أَنَّكُم مُّخْرَجُونَ 35 هَيْهَاتَ هَيْهَاتَ لِمَا تُوعَدُونَ 36
{35-36} Basi, walipoupinga ujumbe wake na kuukataa, wakakataa yale aliyokuja nayo kuhusu ufufuo baada ya kifo na malipo juu ya matendo, na wakasema, "Hivi anawaahidi ati mtakapokufa na mkawa udongo na mifupa, kuwa hakika mtatolewa?" "Hayawi! Hayawi hayo mnayoahidiwa," ya kufufuliwa baada ya kukatikakatika na kuwa udongo na mifupa. Kwa hivyo, wakawa wametazama kwa mtazamo mpungufu, na wakaliona hili kwa mujibu wa uwezo wao kwamba haliwezekani. Wakawa wamepima uwezo wa Muumba kwa uwezo wao. Ametukuka Mwenyezi Mungu na hilo. Kwa hivyo wakapinga uwezo wake wa kufufua wafu, na wakamfanya asiyeweza kabisa, na wakasahau kwamba yeye ndiye aliyewaumba mara ya kwanza, na kwamba yule aliyewaumba baada ya kutokuwepo, ni jepesi zaidi kwake kuwarudisha baada ya kuoza kwao. Na mawili hayo yote ni rahisi zaidi kwake. Kwa hivyo, kwa nini wasikatae uumbaji wao wa kwanza na wakatae mambo ya kihisia na waseme kwamba: Sisi tutaendelea kuishi, ili kusalimike kukataa kwao ufufuo, na ili sasa iwe rahisi kuwasimamishia hoja hiyo hiyo juu ya kudhibitisha uwepo wa Muumba Mkuu? Na hapa kuna ushahidi mwingine, ambao ni kwamba yule aliyeifufua ardhi baada ya kufa kwake, basi hakika huyo anaweza kuwafufua wafu, kwani Yeye hakika ni Muweza wa kila kitu. Na tena kuna ushahidi mwingine, ambao ndio ule aliowajibu nao wale wanaokadhibisha ufufuo kwa kauli yake, "Bali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao, na wakasema makafiri: Hiki ni kitu cha ajabu." "Ati tutakapokufa na tukawa udongo...? Kurejea huko kuko mbali!" Basi akasema katika kuwajibu, "Hakika Sisi tunajua kiasi cha kila kinachopunguzwa na ardhi kutokana nao. Na kwetu kipo Kitabu kinachohifadhi vyema yote."