Langsung ke konten
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Kahf
Surah 18

Al-Kahf

Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.

Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22

Ayat 44

هُنَالِكَ ٱلْوَلَـٰيَةُ لِلَّهِ ٱلْحَقِّ ۚ هُوَ خَيْرٌ ثَوَابًا وَخَيْرٌ عُقْبًا 44

{44} "Huko ulinzi ni wa Mwenyezi Mungu wa Haki tu. Yeye ndiye mbora zaidi wa malipo, na wa mwisho ulio bora zaidi." Yaani, katika hali ile ambayo Mwenyezi Mungu alimuadhibu yule aliyeasi na akapendelea uhai wa dunia hii, na akamkirimu yule aliyeamini na akatenda mema na akamshukuru Mwenyezi Mungu na akawalingia wengine kufanya hivyo, ilibainika na ikawa wazi kwamba ulinzi wa kweli ni wa Mwenyezi Mungu pekee. Kwa hivyo, Mwenye kumuamini na akawa mchamungu, basi Yeye atakuwa mlinzi wake, na atamtukuza kwa kila aina za kutukuza, na atamwondolea maovu na adhabu za kupigiwa mifano. Na yule asiyemuamini Mola wake Mlezi na kumfanyia urafiki, atahasiri dini yake na dunia yake. Basi thawabu zake za kidunia na kiakhera ndizo thawabu bora zinazotarajiwa na kutumainiwa. Basi katika kisa hiki kikubwa kuna mazingatio ya hali ya yule ambaye Mwenyezi Mungu alimneemesha neema za kidunia, lakini zikamsahaulisha akhera, na zikamfanya kuvuka mipaka na akamuasi Mwenyezi Mungu katika neema hizo, kwamba mwisho wake ni kuisha na kutoweka. Na kwamba hata ikiwa anafurahia kwazo kidogo, basi atanyimwa hizo kwa muda mrefu, na kwamba mja anafaa anapopenda kitu katika mali yake au mtoto wake, basi na azifungamanishe neema hizo kwa Yule aliyempa, na aseme, atakacho Mwenyezi Mungu huwa, hakuna nguvu yoyote isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu ili awe mwenye kumshukuru [Mwenyezi Mungu] na kufanya neema zake hizo ziendelee kubaki. Kwa kauli yake, "Na lau kuwa ulipoingia kitaluni kwako, ungelisema: MashaAllah (Alitakalo Mwenyezi Mungu huwa). Hapana nguvu isipokuwa kwa Mungu.” Na ndani yake kuna mwongozo wa kujiliwaza dhidi ya starehe za dunia na matamanio yake kwa heri iliyoko kwa Mwenyezi Mungu. Kwa kauli yake, "Ikiwa unaniona mimi nina mali kidogo na watoto kuliko wewe. Basi huenda Mola wangu Mlezi akanipa kilicho bora kuliko kitalu chako." Na ndani yake kuna kwamba mali na watoto havifai kitu ikiwa havisaidii katika kumtii Mwenyezi Mungu, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, “Na si mali zenu wala watoto wenu watakaowaweka karibu nasi mkawa karibu, isipokuwa mwenye kuamini na akatenda mema.” Na ndani yake kuna kuomba dua ili iangamizwe mali ya yule ambaye mali yake ni sababu ya kuvuka kwake mipaka, kukufuru, na kuhasiri, hasa ikiwa atajifadhilisha kwa sababu yake juu ya waumini na anajifahirisha kwao. Na ndani yake kuna kwamba natija ya ulinzi wa Mwenyezi Mungu na kutokuwepo kwake huwa wazi pale tu vumbi inapotoweka na malipo yakaja, na watendao wakapata malipo yao. Basi “huko ulinzi ni wa Mwenyezi Mungu wa Haki tu. Yeye ndiye mbora zaidi wa malipo, na wa mwisho ulio bora zaidi.”