Langsung ke konten
Tafsir As-Saadi - Swahili · Yunus
Surah 10

Yunus

Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.

Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22

Ayat 32

فَذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمُ ٱلْحَقُّ ۖ فَمَاذَا بَعْدَ ٱلْحَقِّ إِلَّا ٱلضَّلَـٰلُ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ 32

{32} “Basi huyo” ambaye alijieleza mwenyewe kwa yale aliyojieleza, “ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi.” Yaani, afanyiwaye uungu, muabudiwa, msifiwa, mlezi wa viumbe vyote kwa neema zake, naye ndiye wa “haki. Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu?”. Kwa maana, Yeye Mtukufu ndiye wa pekee tu katika kuumba, na kuendesha mambo ya vitu vyote, ambaye hakuna neema yoyote waliyo nayo waja isipokuwa ni kutoka kwake, wala haji na mazuri isipokuwa Yeye, wala hayazuii mabaya isipokuwa Yeye. Yeye ni Mwenye Majina mazuri zaidi na Sifa, kamilifu, kuu, tukufu na za heshima. "Basi ni vipi mnageuzwa” kutoka katika ́ibaada ya yule ambaye hizi ndizo sifa zake hadi kumuabudu yule asiyekuwa na chochote katika kuwepo kwake isipokuwa kutokuwepo, wala hajimilikii manufaa yoyote, wala madhara, wala mauti, wala uhai, wala ufufuo? Basi hana katika umiliki uzito wa chembe, wala hana ushirika kwa namna yoyote ile, wala hafanyi uombezi kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa idhini yake.