Al-An'aam
Wannan fassarar tafsirin as-Saʿdī ce, kamar yadda IslamHouse.com ke wallafa ta a saadi.islamenc.com, an karanta ta daga shafukan wannan shafin yanar gizo. Shafin bai faɗi wanda ya fassara ta ba, ko wane bugu da aka buga take bi, kuma bai bayyana sharuɗɗa na ɗaukar rubutunta ba, saboda haka ba a tabbatar da haƙƙin nuna ta ba. Babu wanda ya kwatanta ta da littafin da aka buga, kuma babu malami da ya duba ta. Kowane sashe yana kusa da ayoyin da yake bayani a kansu, waɗanda rubutun Alƙur’ani ne na Tanzil, kamar yadda yake a can; aya da shafin bai ba ta bayani na kanta ba tana tare da sashen da ya gabace ta, kuma jerin yana ambaton kowace irin wannan aya. Sabīl bai rubuta wani abu daga cikinta ba, kuma bai fassara ta ba.
Rubutu dagasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)an ɗauka 2026-10-22
أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ هَدَى ٱللَّهُ ۖ فَبِهُدَىٰهُمُ ٱقْتَدِهْ ۗ قُل لَّآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْعَـٰلَمِينَ 90
{90} "Hao" waliotajwa "ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaongoa. Basi fuata uongofu wao." Yaani, tembea, ewe Mtume mtukufu, nyuma ya Manabii hawa walio bora zaidi, na ufuate mila yao. Naye Nabii - swalah na salamu za Mwenyezi Mungu zimshukie – alitekeleza, na akafuata uwongofu wa Mitume wa kabla yake, na akajumuisha kila ukamilifu ulio ndani yao. Kwa hivyo, zikakusanyika ndani yake fadhila na sifa maalum alizopita kwazo walimwengu wote, na akawa bwana wa Mitume, na imamu wa wachamungu swalah na salamu zimshukie yeye na wote. Kwa kuzingatia mazingatio haya, aliyachukuwa kuwa ushahidi yule aliyeyachukua miongoni mwa Maswahabah juu ya kwamba, Mtume wa Mwenyezi Mungu – Rehema na Amani zimshukie – ndiye mbora wa Mitume wote. "Sema," uwaambie wale walioupa mgongo ulinganizi wako, "Mimi siwaombi ujira wowote juu yake;" yaani, siwaombi gharama, wala mali kama malipo juu ya kuwafikishia kwangu nyinyi na kuwalingania kwangu nyingi, ndiyo iwe katika sababu za kukataa kwenu. Malipo yangu ni kwa Mwenyezi Mungu tu. "Haya si isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu wote." Wanakumbuka kwayo yale yanayowanufaisha, basi wanayatenda, na yale yanayowadhuru, basi wanayaacha. Na kwayo wanakumbuka kumjua Mola wao Mlezi kwa majina yake na sifa zake. Na wanakumbuka kwayo maadili mema na njia zinazofikisha kwayo, na maadili mabaya na njia zinazofikisha kwayo. Basi kama ukumbusho ni kwa walimwengu wote, unakuwa ndio neema kubwa zaidi ambayo Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwayo; kwa hivyo ni juu yao kuikubali na kushukuru juu yake.