Al-Maaida
Wannan fassarar tafsirin as-Saʿdī ce, kamar yadda IslamHouse.com ke wallafa ta a saadi.islamenc.com, an karanta ta daga shafukan wannan shafin yanar gizo. Shafin bai faɗi wanda ya fassara ta ba, ko wane bugu da aka buga take bi, kuma bai bayyana sharuɗɗa na ɗaukar rubutunta ba, saboda haka ba a tabbatar da haƙƙin nuna ta ba. Babu wanda ya kwatanta ta da littafin da aka buga, kuma babu malami da ya duba ta. Kowane sashe yana kusa da ayoyin da yake bayani a kansu, waɗanda rubutun Alƙur’ani ne na Tanzil, kamar yadda yake a can; aya da shafin bai ba ta bayani na kanta ba tana tare da sashen da ya gabace ta, kuma jerin yana ambaton kowace irin wannan aya. Sabīl bai rubuta wani abu daga cikinta ba, kuma bai fassara ta ba.
Rubutu dagasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)an ɗauka 2026-10-22
لَا يُؤَاخِذُكُمُ ٱللَّهُ بِٱللَّغْوِ فِىٓ أَيْمَـٰنِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ ٱلْأَيْمَـٰنَ ۖ فَكَفَّـٰرَتُهُۥٓ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَـٰكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَـٰثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّـٰرَةُ أَيْمَـٰنِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَٱحْفَظُوٓا۟ أَيْمَـٰنَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمْ ءَايَـٰتِهِۦ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ 89
{89} Yaani, katika viapo vyenu ambavyo mlivifanya kama njia ya mchezo. Navyo ni vile viapo ambavyo mwenye kuapa aliapa kwavyo bila ya nia wala kukusudia, au alivitilia nia akidhani kuwa yeye ni mkweli, lakini yakadhihirika yaliyo kinyume na hilo. Lakini atawachukulia dhambi kwa mnavyoapa kweli kweli kwa kukusudia; yaani, vile mlivyoviazimia na nyoyo zenu zikaviapa kwelikweli. Kama alivyosema katika Aya nyengine, "Bali anawachukulia ubaya kwa yale zinayoyachuma nyoyo zenu." "Basi kafara yake," yaani kafara ya kiapo mlichokifanya kwa nia yenu; "ni kuwalisha masikini kumi," na kulisha huko ni "kwa chakula cha wastani mnachowalisha ahali zenu, au kuwavisha." Yaani, kuwavisha masikini kumi na kuvisha ni kule kunakoruhusika kwa ajili ya Swala, "au kumuachilia huru mtumwa;" [yaani, kumkomboa mtumwa] mwanamke muumini, kama ilivyofungiwa hivyo katika pahali pasipokuwa mahali hapa. Basi pindi atakapofanya moja kati ya haya matatu; basi kiapo chake kitakuwa kimefunguka. "Na asiyepata" moja katika haya matatu, "basi na afunge siku tatu. Hii" iliyotajwa "ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapoapa," inavifunika, na kuvifuta, na kuzuia kufanya dhambi. "Na hifadhini viapo vyenu," kutokana na kuapa kwa Mwenyezi Mungu kwa uongo, na kutokana na viapo vingi. Na vilindeni mnapoapa kutokana na kuvivunja, isipokuwa ikiwa kuvunja huko ni heri. Basi utimilifu wa kuhifadhi ni kwamba afanye heri hiyo wala kisiwe kiapo chake hicho sababu ya kuizuia heri hiyo. "Namna hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anawabainishia Aya zake," zinazobainisha halali, na haramu, zenye kuweka wazi hukumu mbalimbali; "ili mshukuru," mwenyezi Mungu; kwa kuwa aliwafundisha yale ambayo hamkuwa mnayajua. Basi ni juu ya Mja kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya yale aliyomneemesha kwayo miongoni mwa kujua hukumu za kisheria, na kuzibainisha.