An-Nisaa
Wannan fassarar tafsirin as-Saʿdī ce, kamar yadda IslamHouse.com ke wallafa ta a saadi.islamenc.com, an karanta ta daga shafukan wannan shafin yanar gizo. Shafin bai faɗi wanda ya fassara ta ba, ko wane bugu da aka buga take bi, kuma bai bayyana sharuɗɗa na ɗaukar rubutunta ba, saboda haka ba a tabbatar da haƙƙin nuna ta ba. Babu wanda ya kwatanta ta da littafin da aka buga, kuma babu malami da ya duba ta. Kowane sashe yana kusa da ayoyin da yake bayani a kansu, waɗanda rubutun Alƙur’ani ne na Tanzil, kamar yadda yake a can; aya da shafin bai ba ta bayani na kanta ba tana tare da sashen da ya gabace ta, kuma jerin yana ambaton kowace irin wannan aya. Sabīl bai rubuta wani abu daga cikinta ba, kuma bai fassara ta ba.
Rubutu dagasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)an ɗauka 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَأْكُلُوٓا۟ أَمْوَٰلَكُم بَيْنَكُم بِٱلْبَـٰطِلِ إِلَّآ أَن تَكُونَ تِجَـٰرَةً عَن تَرَاضٍ مِّنكُمْ ۚ وَلَا تَقْتُلُوٓا۟ أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا 29
{29} Yeye Mtukufu anawakataza waja wake Waumini kuliana mali zao baina yao kwa batili. Na hili linajumuisha kuzila kwa kuchukua kwa nguvu, na wizi, na kuzichukua kwa kamari, na kwa mapato mabaya. Bali inaweza kuingia ndani yake kuila mali yako mwenyewe kwa namna ya kiburi na ubadhirifu. Kwa sababu, hili ni katika batili, na siyo katika haki. Kisha ilipoharamishwa kuzila kwa batili, akawaruhusu kuzila kwa biashara na mapato yasiyokuwa na vikwazo, ambayo yana masharti yake kama vile kuridhiana na mengineyo. “Wala msijiue.” Yani nyinyi msiuane nyinyi kwa nyinyi, wala mtu asijiue mwenyewe. Na inaingia katika hilo kujitia mwenyewe katika maangamizo na kufanya mambo hatari yanayopelekea kwenye uharibifu na maangamizo. “Hakika, Mwenyezi Mungu kwenu ni Mwenye rehema juu yenu.” Na katika rehema yake ni kwamba alizihifadhi nafsi zenu na mali zenu, na akawakataza kuzipoteza na kuziharibu, na akaweka juu ya hayo yale aliyoweka miongoni mwa adhabu maalum. Na tafakarini ufupisho huu na kuunganisha katika kauli yake: “Msizile mali zenu” na “Wala msijiue” namna alivyojumuisha mali za watu wengine na mali yako mwenyewe, na kujiua na kumuua mwengine kwa maneno mafupi zaidi, kuliko kauli yake: Wasile baadhi yenu mali ya wenzenu, na wala baadhi yenu wasiwaue wenzenu, pamoja na kwamba maneno haya yanajifunga tu na mali ya wengine na nafsi ya wengine. Na pia kufungamisha mali na nafsi na Waumini kwa ujumla ndani yake kuna ushahidi kwamba Waumini katika kupendana kwao, na kurehemeana kwao, na kuhurumiana kwao na masilahi yao ni kama mwili mmoja. Ambapo imani inawaunganisha pamoja juu ya masilahi yao ya kidini na ya kidunia. Na alipokataza kula mali kwa batili ambayo ina madhara makubwa zaidi kwao kwa mlaji na yule ambaye mali yake alichukuliwa, akawaruhusu yale ambayo yana masilahi yao miongoni mwa aina za mapato, na biashara, na aina za kazi na kuajiri. Na akasema, “Isipokuwa kama ni biashara kwa kuridhiana wenyewe” yani, inaruhusika kwenu. Na sharti la kuridhiana pamoja na kwamba ni biashara ni ili kuashiria kwamba ni sharti kwamba mkataba usiwe mkataba wa riba, kwa sababu riba siyo katika biashara, bali ni kinyume na makusudio yake. Na kwamba ni lazima kila mmoja wa wahusika wa mkataba aridhie na afanye hivyo kwa hiari. Na ukamilifu wa kuridhia ni kwamba kile kinachofanyiwa mkataba kiwe kinajulikana. Kwa sababu ikiwa sivyo, basi kuridhia hakufikiriwi kuweza kukisalimisha. Kwa sababu kile hakuna uwezo juu yake ni sawa na kuuza kamari. Kwa hivyo, uuzaji wa udanganyifu (Gharar) kwa aina zake zote hauna ridhaa ndani yake, kwa hivyo mkataba huo hautekeleki. Na ndani yake kuna kwamba mikataba inahitimishwa kwa kile kinachoionyesha katika maneno au vitendo. Kwa sababu Mwenyezi Mungu ameweka sharti la ridhaa, kwa kuridhika kukitokea kwa njia yoyote ile, mkataba unahitimika kwayo. Kisha akahitimisha Aya hiyo kwa kauli yake, “Hakika, Mwenyezi Mungu kwenu ni Mwenye kurehemu.” Na katika rehema yake ni kwamba amezilinda damu zenu na mali zenu na akavihifadhi, na akawakataza kuvivunja.