Tsallaka zuwa abin da ke ciki
Tafsir As-Saadi - Swahili · Az-Zumar
Sura ta 39

Az-Zumar

Wannan fassarar tafsirin as-Saʿdī ce, kamar yadda IslamHouse.com ke wallafa ta a saadi.islamenc.com, an karanta ta daga shafukan wannan shafin yanar gizo. Shafin bai faɗi wanda ya fassara ta ba, ko wane bugu da aka buga take bi, kuma bai bayyana sharuɗɗa na ɗaukar rubutunta ba, saboda haka ba a tabbatar da haƙƙin nuna ta ba. Babu wanda ya kwatanta ta da littafin da aka buga, kuma babu malami da ya duba ta. Kowane sashe yana kusa da ayoyin da yake bayani a kansu, waɗanda rubutun Alƙur’ani ne na Tanzil, kamar yadda yake a can; aya da shafin bai ba ta bayani na kanta ba tana tare da sashen da ya gabace ta, kuma jerin yana ambaton kowace irin wannan aya. Sabīl bai rubuta wani abu daga cikinta ba, kuma bai fassara ta ba.

Rubutu dagasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)an ɗauka 2026-10-22

Aya ta 73

وَسِيقَ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوْا۟ رَبَّهُمْ إِلَى ٱلْجَنَّةِ زُمَرًا ۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءُوهَا وَفُتِحَتْ أَبْوَٰبُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا سَلَـٰمٌ عَلَيْكُمْ طِبْتُمْ فَٱدْخُلُوهَا خَـٰلِدِينَ 73

{73} Kisha akasema kuhusu watu wa Peponi: "Na wale waliomcha Mola wao Mlezi" kwa kumpwekesha na kumtii, "wataongozwa" kwa njia ya heshima, utukufu kama wageni huku wamepanda vipando bora zaidi "kwenda Pepo kwa makundi" kwa furaha na kushangilia. Kila kundi litakuwa pamoja na kundi linaloafikiana nalo katika matendo yake na kufanana nalo. "Mpaka watakapofika" kwenye maeneo hayo mapana na majumba mazuri, na upepo wake ukawapuliza, na wakati wa umilele wake na furaha yake ukafika, "nayo milango yake imekwisha funguliwa" kwa ajili yao ili kuwatukuza viumbe watukufu. "Walinzi wake watawaambia" wakiwapongeza na kuwakaribisha: "Amani iwe juu yenu," kutokana na kila taabu, ovu na hali yoyote mbaya. "Mmetahirika" nyoyo zenu kwa kumjua Mwenyezi Mungu, kumpenda na kumcha. Na pia ndimi zenu zimetahirika kwa kumtaja Yeye. Na pia viungo vyenu vimetahirika kwa kumtii. "Basi" kwa sababu ya kutahirika kwenu "ingieni humu mkae milele" kwa sababu ndiyo ni nyumba safi, na wala hawaifailii isipokuwa walio safi. Na akasema kuhusiana na Jahannamu: "Itafunguliwa milango yake" na akasema kuhusiana na Pepo "nayo milango yake imekwisha funguliwa." Hili linaashiria kwamba watu wa Motoni, mara watakapoifikia, milango yake itafunguliwa bila ya kungojewa wala kupewa muhula, na ili adhabu yake na joto lake liwe kubwa zaidi kwao inapofunguliwa mbele ya nyuso zao pindi watakapoifikia. Ama Pepo, hayo ni makazi ya juu na ya thamani kubwa, ambayo hayawezi kufikiwa isipokuwa wale ambao walifanya visababu vya kuyafikia. Na pamoja na hayo, ili kuingia humo, watahitaji uombezi wa mbora wa waombezi. Kwa hivyo, haikufunguliwa pindi walipoifikia, bali wataomba uombezi kwa Mwenyezi Mungu kupitia Muhammad – rehema na amani ziwe juu yake, naye atafanya uombezi huo, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ataukubali. Katika Aya hii kuna ushahidi kwamba Jahannam na Pepo zina milango inayofunguka na kufungwa, na kwamba kila moja yake ina walinzi. Nayo ni makazi ambayo ni wale wanaoyastahiki tu wataingia humo.