Tsallaka zuwa abin da ke ciki
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ta 2

Al-Baqara

Wannan fassarar tafsirin as-Saʿdī ce, kamar yadda IslamHouse.com ke wallafa ta a saadi.islamenc.com, an karanta ta daga shafukan wannan shafin yanar gizo. Shafin bai faɗi wanda ya fassara ta ba, ko wane bugu da aka buga take bi, kuma bai bayyana sharuɗɗa na ɗaukar rubutunta ba, saboda haka ba a tabbatar da haƙƙin nuna ta ba. Babu wanda ya kwatanta ta da littafin da aka buga, kuma babu malami da ya duba ta. Kowane sashe yana kusa da ayoyin da yake bayani a kansu, waɗanda rubutun Alƙur’ani ne na Tanzil, kamar yadda yake a can; aya da shafin bai ba ta bayani na kanta ba tana tare da sashen da ya gabace ta, kuma jerin yana ambaton kowace irin wannan aya. Sabīl bai rubuta wani abu daga cikinta ba, kuma bai fassara ta ba.

Rubutu dagasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)an ɗauka 2026-10-22

Aya ta 62

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَٱلَّذِينَ هَادُوا۟ وَٱلنَّصَـٰرَىٰ وَٱلصَّـٰبِـِٔينَ مَنْ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَعَمِلَ صَـٰلِحًا فَلَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ 62

Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema akihukumu kati ya makundi ya waliopewa kitabu:

(62) Na hukumu hii ni ya Watu wa Kitabu hususan, kwa sababu Wasabai wapo sahihi ya kwamba wao ni miongoni mwa makundi ya Kikristo. Basi Mwenyezi Mungu akatoa habari kuwa Waumini wa huu Ummah, na Mayahudi, na Wakristo na Wasabai, mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu [miongoni mwao] na Siku ya Mwisho na wakawasadiki Mitume wao. Basi watapata malipo makubwa na amani, wala haitakuwa hofu juu yao, wala hawatahuzunika. Na ama mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu miongoni mwao, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho, basi yeye yuko kinyume na hali hii; hivyo, hofu na huzuni vitakuwa juu yake. Na sahihi ni kwamba hukumu hii baina ya haya makundi ni kuhusiana na jinsi walivyo, sio kuhusiana na kumuamini Muhammad. Kwa sababu, huku ni kuwazungumzia kabla ya utume wa Muhammad. Na hivi ndivyo zilivyo hali zao. Na hii ndiyo njia ya Qur-ani inapoingia katika baadhi ya nafsi – wakati wa kusimulia Aya – baadhi ya fikira potofu, basi huwa hakuna budi kwamba utapata kinachoondoa fikira hiyo potofu. Kwa sababu (Qur-ani hii) ni uteremsho kutoka kwa yule anayeyajua mambo kabla hayajatokea, na yule ambaye rehema zake zimeenea kila kitu. Na hilo - na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi - ni kwamba, alipowataja Wana wa Israili na kuwakashifu, na akataja dhambi zao na maovu yao, huenda ikaingia katika baadhi ya nafsi kwamba wote pia wanaingia katika kashfa hiyo. Kwa hivyo, Muumba Mtukufu alitaka kubainisha wale ambao hawaingii katika kashfa hiyo miongoni mwao kwa kueleza sifa zake. Na pindi alipowataja Wana wa Israili hasa, ikaleta fikira kuwa hilo ni mahususi kwao. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja hukumu ya jumla inayojumuisha makundi yote. Ili ukweli ubainike na fikira upotovu na mkanganyiko viondoke. Basi ametakasika yule ambaye ameweka katika Kitabu chake yale yanayoangaza akili za wenye elimu.